Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Hapo sasa ngoja wafia dini waje na mapovu ,kuwepo kwa mungu ni story za kusadikika tuu ipo siku wataelewa tuu
Qur-an sura ya
16:22. Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wasio iamini Akhera(siku ya kiama) nyoyo zao zinakataa, nao wanajivuna.

Wewe ni kipi kinachokupa kusema hivyo kuwa Mungu ni story za kusadikika?
 
Kwa mujibu wa mungu au kwa mujibu wa vitabu vilivyoandika habari za mungu?
 
Qur-an sura ya
16:22. Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wasio iamini Akhera(siku ya kiama) nyoyo zao zinakataa, nao wanajivuna.

Wewe ni kipi kinachokupa kusema hivyo kuwa Mungu ni story za kusadikika?
Thibitisha mungu yupo
 
Fanya Toba. Mungu hachunguziki. Kwanza wewe ni kama nani? Kuhoji uwezo wa Mungu? Yaan ata aibu Haya na soni umekosa kweli? Amaa kweli kizazi cha laana
Hata spiderman hachunguziki

Thibitisha mungu yupo
 
Nacheka sana, swali gani sijajibu kijana, kwanza nimeonyesha maswali yako yote ya uongo. Pili, nikajujibu maswali yako.

Tofautisha kati ya mtazamo wako na uhalisia, kitu unachokifanya wewe ni kutaka mitazamo iwe ukweli huu, ujinga nauona sana kwenu.

Unapoambiwa Allah ni muweza wa kila kitu, maswali yote kuhusu udhaifu ni ya uongo na hayaingii kwake, sasa sababu umezoea kujifariji endelea kujifariji kijana.

Mathalani, Mola wetu amejiharamishia kudhulumu, hili kwake halipo. Kinyume chake hakuna.

Nakukumbusha tu hujajibu maswali, yangu.
 
Thibitisha mungu yupo
Huwaoni wenye upofu au wenye ulemavu au wenye ububu,unadhani walichagua kuwa vile ilhali wengine ni wazima?
Ninani basi aumbaye vile Tumboni mwa Mama?
Huyo ndo Mungu
Je wamjua mwengine wewe asiyekuwa yeye?
 
Hata spiderman hachunguziki

Thibitisha mungu yupo
Leo hii kuna mvua mpaka inakera,lakini hakuna anayethubutu kuizuia,
Ninani huyo anayeleta Mvua, na wakati mwingine Kuzuia mvua na Kusababisha Ukame?
Niambie huyo afanyae hivyo ninani?
Huyo ndo Mungu asiefananishwa na yeyote katika viumbe.
 
Kama maswali kuhusu udhaifu ni ya uongo iweje uhusishe ubaya umeumbwa na yeye huoni kwamba ubaya nao ni udhaifu?

Umesema mungu angeumba ulimwengu ambao hauna mabaya huyo mungu asingekua muweza wa yote

Inamaama huyo mungu alishindwa kuumba ulimwengu usio na mabaya na bado akawa muweza wa yote? Kama alishindwa basi bado si muweza wa yote maana angeweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kujadilika

Kufa kuwe ni kubaya au kuzuri kwa minaajili ya mungu ambaye anasifa ya ubaya na uzuri lazima jambo hili ahusike. Mungu anaweza kujiua?

Mungu anaweza kuumba jiwe zito ambalo hawezi kulibeba?

Kama hawezi kuumba jiwe basi si muweza wa yote kwasababu kuna jiwe kashindwa kuliumba

Kama anaweza kuliumba bado si muweza wa yote kwasababu kuna jiwe kaliumba na hawezi kulibeba
 
Huwaoni wenye upofu au wenye ulemavu au wenye ububu,unadhani walichagua kuwa vile ilhali wengine ni wazima?
Ninani basi aumbaye vile Tumboni mwa Mama?
Huyo ndo Mungu
Je wamjua mwengine wewe asiyekuwa yeye?
Upofu na ububu unaonesha huu ulimwengu aujaumbwa na mungu ambaye muweza wa yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote anayesimuliwa kwenye vitabu vya dini

Wapofu na mabubu wapo kwasababu mungu mwenye huruma ambaye angeweza kuwanusuru na janga hilo hayupo
 
Kama maswali kuhusu udhaifu ni ya uongo iweje uhusishe ubaya umeumbwa na yeye huoni kwamba ubaya nao ni udhaifu?

Haya ndio matatizo ya kutokujibu maswali unapo ulizwa. Ndio maana huwa nakutaka ujibu maswali yangu, nilikwambia Allah hana sifa ya ubaya mzee, umeandika nini hapa ?

Kuna mdau alikuuliza swali zuri sana, kwamba ubaya unauelewa vipi wewe.

Tusipoteze muda jibu maswali niliyo kuuliza, maana naona unauliza mambo ambayo hayapo.
 
Leo hii kuna mvua mpaka inakera,lakini hakuna anayethubutu kuizuia,
Ninani huyo anayeleta Mvua, na wakati mwingine Kuzuia mvua na Kusababisha Ukame?
Niambie huyo afanyae hivyo ninani?
Huyo ndo Mungu asiefananishwa na yeyote katika viumbe.
Jangwani kuna mvua inayonyesha hadi inakera?

Hujui mazingira rafiki yanayopaswa kutunzwa ili mvua zinyeshe na kuepuka ukame?

Hakuna anayefanya hiyo ni nature ya ulimwengu, na ndio maana tunasisitiziwa kutokata miti hovyo hatuambiwi tusali mungu ili mvua inyeshe
 
Ayubu alikuwa mtumishi mwaminifu sana kwa Mungu lakini aliruhusu ajaribiwe na shetani kwa maganjwa kwa kipindi kisichopungua miaka 17, hivyo sio lazima iwe ivyo unavyodhani wakati Mwingine Mungu uruhusu jambo litokee kama Corona kwa kusudi maalum
 
Dawa imeanza kukuingia umeanza ku-quote kakifungu kamoja unakokaona unaweza kukajibu ili kukwepa maswali

Kama allah hana sifa ya ubaya unakubali kwa sifa hiyo hawezi kuumba ubaya?

Halafu umejisahau sana maswali yangu hujayajibu
Kwa uwezo wake wote alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya kuwepo? (Jibu lisiseme kifo ni sifa ya kiumbe maana kwa uwezo wote alionao hakuna lakumshinda)

Kama hafi basi si muweza wa yote kwasababu kuna mambo hayawezi kuyafanya yako nje ya uwezo wake

Kwa uwezo wake wote alionao anaweza kujiua?
 


Sikia nikuambie ukweli....hizi dini Uislam na Ukristu ni za kutengenezwa tu na watu ili jamii iwe controlled. Baba Mtakatifu kafunga na kuombea kinga ipatikane wapi, juzi juzi tu huko Nigeria kuna msanii kajitokeza (TB Joshua) kwa kusema corona itakwisha by mwisho wa mwezi uliopita lakini wapi watu ndiyo kwanza wanaongezeka kufa tu kila kukicha. HAKUNA baba mtakatifu wala Shehe yeyote aliyewahi kuombea janga lisitokee na ikawa hivyo, ni usanii tu.Waafrika tunakosea hapa tu, kuacha imani zetu na kujiamisha upuuzi wa watu wengine usio na tija kwetu hata kidogo. Cha kusikitisha ni kwamba hatutaki kukubali ukweli wakati kila kitu kipo wazi. Utashangaa atakuja mpuuzi hapa na kusema mimi nimetenda dhambi kwa kusema haya wakati dhambi anayo yeye kujikana na kukumbatia dini za watu zisizomsaidia chochote.
 
ungu Huumba apendavyo yeye, sio kwa utakavyo wewe kiumbe.
Kawaida binadamu hupenda apatwe na kheri tuu, lakini huo si katika mpango wake muumba.
Lakini Muundo wa Mungu una hekima kubwa Usio ijuwa wewe (Usie na Imani wala Nuru ya kuyajua hayo)
Jisomee Qur-an ufunguke macho ,falsafa itakuzamisha shimoni,na ukifa ndo kuna maisha mengine.
 
Ayubu alikuwa mtumishi mwaminifu sana kwa Mungu lakini aliruhusu ajaribiwe na shetani kwa maganjwa kwa kipindi kisichopungua miaka 17, hivyo sio lazima iwe ivyo unavyodhani wakati Mwingine Mungu uruhusu jambo litokee kama Corona kwa kusudi maalum
Mungu ambaye alikua tayari kumla majipu ayubu ili apime imani yake huyo ni mungu asiye na ujuzi wote

Mungu mjuzi wa yote na upendo wote hawezi kumjaribu mtu kwasababu kwa ujuzi wake alikwisha kujua future ya kiumbe hafi hatma yake kabla hata hicho kiumbe hakijazaliwa

Mungu ambaye aliua watoto wa kiume ili kum-prove farao kua yeye ni muweza wa yote, hana sifa ya umungu bali ana inferior kama sisi tu na point nzima ya uwepo wake ni hoax tu

Thibitisha mungu yupo
 
Kwani wewe una dini gani?
Je unaamini Uwepo wa Mungu?
 
Dawa imeanza kukuingia umeanza ku-quote kakifungu kamoja unakokaona unaweza kukajibu ili kukwepa maswali

Kama allah hana sifa ya ubaya unakubali kwa sifa hiyo hawezi kuumba ubaya?

Naona unarudia kosa lile lile, ametakasika na hilo. Ndio maana uliulizwa na nilikuuliza ubaya umeujuaje ?

Hujibu, kuhusu kuchagua haya ni maamuzi, tu mzee, na huwa siachi kitu.
 
Huyo Mungu unaye muhubiri wewe mbona ni wa kufikirika zaidi?
Mungu wa Upendo anayejuwa yote,asiyeleta mabaya ila mema tu.
Je wewe wamjuwa huyo?
Tutajie basi ni yupi huyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…