Virusi vya corona vimekuja kuthibitisha wazi kua maombi hayana msaada wowote kwenye maisha ya binadamu na wala dini haiwezi kuwaokoa binadamu na janga lolote la asili hivyo kuabudu na kufanya maombi ni kazi bure.
Juzi niliona Italy wakitembeza msalaba na sanamu la maria mama wa yesu angani ili kuwaokoa, kilichofuatia ni vifo vingi zaidi vya watu.
Jana niliona video clip Gwajima akisihi watu kunawa mikono, nikajiuliza ameshindwa kuombea watu hili gonjwa lipite au mungu wake anachagua magonjwa ya kuponya na ya kuacha yaue watu maana mara nyingine hua wanadai wanaombea na kuponya ukimwi, kansa, nk, je corona mungu haiwezi?
Corona imevamia Italy hadi vatcan imeua mapadri, viongozi wakubwa wa kidini vatcan(petro alipojenga kanisa-mwamba)wanakufa kwa corona, mwamba unaenda kuanguka, siku corona ikimvaa papa ndio tutajua hatujui.
Haya mambo ya dini, maombi na sala ni ya watu, hayawezi kumsaidia binadamu kwa chochote. Mungu anaeshindwa kuzuia majanga na magonjwa ataweezaje kuyaondoa kwa maombi ya binadamu kama yeye na malaika wameshindwa kuzuia kabla?
Tuendelee kuomba ndugu zangu[emoji3]