Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
- Thread starter
- #841
Hii michambo mixer vitisho ilikua inaweza kuleta impact katika zama za ujinga tu ambao watu wakipindi hicho walikua tayari kukubali chochote kwa dhana ya vitishoUzima ndio unaokupa kiburi.
Hata mtoto mpumbavu akiwa na kiburi anaweza akamwambia mama yake usinisumbue hata Mimi ningetangulia ningekuzaa.
Umewahi kujiuliza maswali haya :-
Kwa nini sio kila mtu ni Daktari?
Kwa nini sio kila MTU ni Mchawi ?
Kwa nini sio kila MTU ni mwanamziki au Mchezaji au Mwana Sarakasi ?
Kwa nini sio kila MTU ni Mwanamazingaumbwe?
Kwa nini kila MTU sio Mwanajeshi au kwa nini sio kila mwanajeshi ni Komandoo?
Kwa nini wote hatuna akili sawa?
Kwa nini wengine ni Magenius na wengine sio?
Huoni tu kuwa kuna Mwenye Maarifa makubwa aliyewaumba hawa watu na kuwapa vipaji kwa kazi na wakati wakati wake?
Kama binadam ametengeneza magari ya aina tofauti na kila moja na ubora wake kama vile Benz ,Toyota, Mitsubishi, Nissan, Land Rover n.k. Kichaa na mpumbavu ndiye anayeweza akasema hayo magari yamejitengeneza yenyewe.
Binadam wameumbwa na kupewa akili ya kujisimamia .
Engineer wa Umeme akishawasha umeme anaondoka zake umeme unaendelea kuwaka kwa kiwango alichoweka. Ukikatika hata vishoka wanaweza kuunga tena.
Mungu ana Mambo Mengi na kazi kubwa ya kupambana na muasi Shetani sio kuhangaika na Korona walizozitafuta wafuasi wa Shetani kwa tamaa zao za kutajirika na kumiliki uchumi na madaraka ya dunia.
Dawa zinatoka kwa Mungu kama haujui.
Ndugu yako Shetani amekua akidanganya watu sana lakini ujanja wote wa dawa unatoka kwa Mungu ndio maana hata alama ya tiba dunia nzima ni Nyoka aliyejisokota kwenye mti.
Waganga wote wa asili wanarithishwa kwa imani ya mizimu namna ya kutambua miti ya dawa. Hii pia ni dini.
Waitali wameasi na kukufuru sana mana Makanisa mengi wameyageuza kumbi za starehe na club za Pombe na kufanya kila aina ya ufuska kwenye majengo ya Makanisa. Sasa Mungu ameamua kuudhihirisha ulimwengu kuwa kazi za mikono yao haziwezi kuwaokoa bila kutii amri zake.
Bado wewe zamu yako inakuja. Utamheshimu Mungu tu kabla hujafa.
Mana kama sio Corona itakupiga Sukari na kama sio sukari itakupiga Presha,kama sio Presha utakupiga Ukimwi na kama sio ukimwi utapigwa na ajali na kama sio ajali utapigwa na Kansa na kama sio kansa utapigwa na Mpafu na kama sio mapafu utapigwa na vidonda vya tumbo.
Utamkumbuka tuu aliyekuumba na kukupa pumzi na akili na sasa unasema hayupo . Utakapokuwa unachungulia kaburi utawaza kuwa mada haiwezi kuharibiwa lakini inaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine. Utaona unavyokaribia kubadilika kwenda kwenye hali usiyoijua ndipo utakapomkumbuka Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
It's Scars