UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Dini ya kweli ni ipi?Ni kwa sababu hizo dini zote si za ukweli, ni fabrications tu na ni man made, history is there to prove them wrong.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dini ya kweli ni ipi?Ni kwa sababu hizo dini zote si za ukweli, ni fabrications tu na ni man made, history is there to prove them wrong.
Hoja gani ambayo nimeiruka?Usiwe mtu wa kuruka hoja, baadhi unajibia zingine unaacha. Hizo unazoziacha unatakiwa utolee majibu kama umeishiwa hoja kunja hema. Kama umekiri kuwa Kuna vitu huwezi kuvidiriki kwa upeo wako na akili,ni upi msingi wa swali lako la kutaka kuthibitishiwa kuwepo kwa mola muumba?
Na ukirudi kwenye comment yangu umeshindwa kunithibitishia uwepo wa akili kwenye kiwiliwili chako. Na pia haujaeleza msimamo wako kuhusu roho na utambuzi ulionao na wapi ilipo? Tokea majibu hoja hizo kwanza.
Ha ha!!
Jamaa maswali yako magumu sana.
Kuna miungu zaidi ya 3,000 watuambie kwanza yupi ni wa kweli? Kila mtu anasema wake ndio sahihi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Inamaana wewe unataka watu waaamini kua mwenyezimungu hayupo kama ambavo wewe unaamini?Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?
Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?
Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.
Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?
Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.
Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.
Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.
Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?
Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?
Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?
Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?
Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?
Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
====
Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Kwenye bandiko lako unasema kua hakuna mungu
Sasa anaejidai kuwa Mungu kwa mujibu wa vitabu vya dini ndo huyo anasema kamuumbq binadamu kwa udhaifu.Ningemsikia akisema, leo hii nisingewaganda hapa mthibitishe uwepo wake
Nimesoma vitabu vya dini vikidai kua binadamu hajakamilika anamadhaifu, unabidi uelewe kua nimejenga hoja kwa minaajili ipi
It's Scars
Kwanza hayo maneno unahakika gani kua yamesemwa na huyo mungu?Sasa anaejidai kuwa Mungu kwa mujibu wa vitabu vya dini ndo huyo anasema kamuumbq binadamu kwa udhaifu.
Sasa huyo Mungu mwenyewe anasema kaumba kiumbe dhaifu.
Nikijenga hoja hapa kuhusu spiderman na wewe ukiijadili, hiyo itafanya spiderman awepo?Wewe kwa nini usijenge hoja kwa Mujibu wa vile alivyosema badala yake unajenga hoja kana kwamba yeye kaisema hoja hiyo..
Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na upendo wote hawezi kuumba kiumbe dhaifuKwani waoi Mungu kasema kuwa amemuumba kiumbe akiwa hana udhaifu ni mkamilifu ?
Kwanini kutokusema kwake kusihusishwe na sababu ya kutokuwepo kwake?Kama hajasema hivyo manake Mungu hajasema kuwa kaumba kiumbe mkamilifu wewe tu ndo unajjitia kumtangulia.
Na kama vitabu hivyo hivyo vimesema mungu ni mjuzi wa yote, uwezo wote na upendo wote sasa kwanini kiumbe kiwe dhaifu?Mungu kasema kamuumba kiumbe ni dhaifu,na wewe unakubali kuwa sisi viumbe ni madhaifu sasa kwa hayo ya kiumbe mkamilifu umeyatoa wapi ?
Huu ubishani unaoneshaje ya kwamba hakuna Mungu? Fafanua.Uwepo tu wa huu ubishano unaonesha kua mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na upendo wote ambaye kila mahali yupo ni hadithi
Unaweza kuniambia ni hoja gani zinazofanya ukubali kua spiderman hayupo kweli?
It's Scars
Wewe Wacha ujinga, Qur'an yenyewe inakwambia kuna ilm. Neno la Kwanza lilishushwa ni Soma.Wewe unajifanya unafata Qurani tu,huyo ibn majah kwa nini umtumie kumkataza Mtu kucheka anapojadili ?
Mbona usitumie Qurani tu kukataza jambo lako ?
Wapi Qurani imekataza kucheka ?
Aya ulotoa haijataja kucheka hapo
إِنَّهُ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْ عِبَادِي يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ
(AL - MUUMINUN - 109)
Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.
فَاتَّخَذْتُمُوهُمْ سِخْرِيًّا حَتَّىٰ أَنسَوْكُمْ ذِكْرِي وَكُنتُم مِّنْهُمْ تَضْحَكُونَ
(AL - MUUMINUN - 110)
Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka.
Wapi Qurani imekataza Mtu kucheka akiwa anajadili na kafiri ?
Sent using Jamii Forums mobile app
Ww mshindi.Sijakukataza usiamini, ila kuamini kwako hakufanya jambo hilo liwe kweli.
Kuna watu wanaamini ng'ombe ni mungu ambaye ameumba kila kitu, watu hao wakisema "ndiyo maana naamini" kusema kwao huko kutafanya ng'ombe awe mungu kweli?
Swali langu la msingi ni kutaka nithibitishiwe uwepo wa huyo mungu
Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
Hakuna relation yeyote kati ya neno "mnyonge" na matusi
Utasemaje huwezi kujadiliana, wakati mpaka muda huu tunaendelea kujadiliana?
Kivipi maisha unsyoishi yathibitishe unachokitukuza na sio kitu kingine?
It's Scars
Hilo swali natakiwa mie ndiyo nikuulize wewe maana wewe ndiyo mwenye kujua dini ya kweli na ndiyo maana unasema hizi zengine sio za kweli. Nitajie hiyo ya kweli.Ni ile ambayo imethibitisha mungu yupo kihalisia bila kuacha utata
Kuna dini gani ambayo imewahi kuthibitisha hilo?
It's Scars
Uwepo wa huu ubishano unaonesha kua mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na upendo wote ambaye kila mahali yupo ni hadithiHuu ubishani unaoneshaje ya kwamba hakuna Mungu? Fafanua.