Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Usiwe mtu wa kuruka hoja, baadhi unajibia zingine unaacha. Hizo unazoziacha unatakiwa utolee majibu kama umeishiwa hoja kunja hema. Kama umekiri kuwa Kuna vitu huwezi kuvidiriki kwa upeo wako na akili,ni upi msingi wa swali lako la kutaka kuthibitishiwa kuwepo kwa mola muumba?
Na ukirudi kwenye comment yangu umeshindwa kunithibitishia uwepo wa akili kwenye kiwiliwili chako. Na pia haujaeleza msimamo wako kuhusu roho na utambuzi ulionao na wapi ilipo? Tokea majibu hoja hizo kwanza.
Hoja gani ambayo nimeiruka?

It's Scars
 
Ha ha!!

Jamaa maswali yako magumu sana.

Kuna miungu zaidi ya 3,000 watuambie kwanza yupi ni wa kweli? Kila mtu anasema wake ndio sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na katika hiyo miungu iliyo zaidi ya 3000 watueleze kwanini mungu wao ndio sahihi na kivipi

Kisha watuthibitishie hiyi miungu mingine haipo

It's Scars
 
Nimekuuliza ulitaka wasifanye kazi wala kushughlika na taaluma zao?
Ishu sio kufanya, ishu ni kufanya katika njia gani

Kama maombi yanaweza kusaidia kazi zao kufanyika kulikua na sababu yeykte wao kutofanya kwa njia hiyo?

It's Scars
 
Hoja zipi zinafanya madai yako ya kuwa hakuna Mungu kuwa kweli?
Uwepo tu wa huu ubishano unaonesha kua mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na upendo wote ambaye kila mahali yupo ni hadithi

Unaweza kuniambia ni hoja gani zinazofanya ukubali kua spiderman hayupo kweli?

It's Scars
 
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Inamaana wewe unataka watu waaamini kua mwenyezimungu hayupo kama ambavo wewe unaamini?
 
Kwenye ba
Kwenye bandiko lako unasema kua hakuna mungu
Kwenye post yako umesema mimi nimetaka watu waamini hakuna mungu

Halafu hapo umenionesha nimeandika "hakuna mungu"

Sasa huoni kwamba unajipinga?

It's Scars
 
Ningemsikia akisema, leo hii nisingewaganda hapa mthibitishe uwepo wake

Nimesoma vitabu vya dini vikidai kua binadamu hajakamilika anamadhaifu, unabidi uelewe kua nimejenga hoja kwa minaajili ipi

It's Scars
Sasa anaejidai kuwa Mungu kwa mujibu wa vitabu vya dini ndo huyo anasema kamuumbq binadamu kwa udhaifu.

Sasa huyo Mungu mwenyewe anasema kaumba kiumbe dhaifu.

Wewe kwa nini usijenge hoja kwa Mujibu wa vile alivyosema badala yake unajenga hoja kana kwamba yeye kaisema hoja hiyo..

Kwani waoi Mungu kasema kuwa amemuumba kiumbe akiwa hana udhaifu ni mkamilifu ?

Kama hajasema hivyo manake Mungu hajasema kuwa kaumba kiumbe mkamilifu wewe tu ndo unajjitia kumtangulia.

Mungu kasema kamuumba kiumbe ni dhaifu,na wewe unakubali kuwa sisi viumbe ni madhaifu sasa kwa hayo ya kiumbe mkamilifu umeyatoa wapi ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa anaejidai kuwa Mungu kwa mujibu wa vitabu vya dini ndo huyo anasema kamuumbq binadamu kwa udhaifu.
Kwanza hayo maneno unahakika gani kua yamesemwa na huyo mungu?

Sasa huyo Mungu mwenyewe anasema kaumba kiumbe dhaifu.

Unajuaje kwamba watu walivyoshindwa kufanya vitu kwa matamanio yao waliamua kutengeneza uongo kupitia udhaifu wao huo kua wameumbwa na mungu thats why waka apply hiyi dhana kwenye vitabu vyao kua mungu kasema kua kaumba kiumbe dhaifu?

Wewe kwa nini usijenge hoja kwa Mujibu wa vile alivyosema badala yake unajenga hoja kana kwamba yeye kaisema hoja hiyo..
Nikijenga hoja hapa kuhusu spiderman na wewe ukiijadili, hiyo itafanya spiderman awepo?

Kwani waoi Mungu kasema kuwa amemuumba kiumbe akiwa hana udhaifu ni mkamilifu ?
Mungu muweza wa yote, mjuzi wa yote na upendo wote hawezi kuumba kiumbe dhaifu

Kuwepo kwa viumbe dhaifu kunainesha mungu huyu ni hadithi tu wala hayupo kihalisia


Kama hajasema hivyo manake Mungu hajasema kuwa kaumba kiumbe mkamilifu wewe tu ndo unajjitia kumtangulia.
Kwanini kutokusema kwake kusihusishwe na sababu ya kutokuwepo kwake?

Vipi kama hajasema kwasababu hayupo?

Mungu kasema kamuumba kiumbe ni dhaifu,na wewe unakubali kuwa sisi viumbe ni madhaifu sasa kwa hayo ya kiumbe mkamilifu umeyatoa wapi ?
Na kama vitabu hivyo hivyo vimesema mungu ni mjuzi wa yote, uwezo wote na upendo wote sasa kwanini kiumbe kiwe dhaifu?

Kama unaweza kukubali kuwepo kwa udhaifu wa kiumbe katika ulimwengu ambao mungu mjuzi wa yote, uwezo wote na upendo wote yupo, basi kwa sheria hiyo hiyo tunaweza kukubali kua watu ni dhaifu katika ulimwengu ambao mungu hayupo

It's Scars
 
Uwepo tu wa huu ubishano unaonesha kua mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na upendo wote ambaye kila mahali yupo ni hadithi

Unaweza kuniambia ni hoja gani zinazofanya ukubali kua spiderman hayupo kweli?

It's Scars
Huu ubishani unaoneshaje ya kwamba hakuna Mungu? Fafanua.
 
Wewe unajifanya unafata Qurani tu,huyo ibn majah kwa nini umtumie kumkataza Mtu kucheka anapojadili ?

Mbona usitumie Qurani tu kukataza jambo lako ?

Wapi Qurani imekataza kucheka ?

Aya ulotoa haijataja kucheka hapo

إِنَّهُ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْ عِبَادِي يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ

(AL - MUUMINUN - 109)
Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.

فَاتَّخَذْتُمُوهُمْ سِخْرِيًّا حَتَّىٰ أَنسَوْكُمْ ذِكْرِي وَكُنتُم مِّنْهُمْ تَضْحَكُونَ

(AL - MUUMINUN - 110)
Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka.

Wapi Qurani imekataza Mtu kucheka akiwa anajadili na kafiri ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe Wacha ujinga, Qur'an yenyewe inakwambia kuna ilm. Neno la Kwanza lilishushwa ni Soma.

Tatizo lako ni ilm finyu mpaka unaanza kuzuwa. Soma.
 
Sijakukataza usiamini, ila kuamini kwako hakufanya jambo hilo liwe kweli.

Kuna watu wanaamini ng'ombe ni mungu ambaye ameumba kila kitu, watu hao wakisema "ndiyo maana naamini" kusema kwao huko kutafanya ng'ombe awe mungu kweli?


Swali langu la msingi ni kutaka nithibitishiwe uwepo wa huyo mungu

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?


Hakuna relation yeyote kati ya neno "mnyonge" na matusi


Utasemaje huwezi kujadiliana, wakati mpaka muda huu tunaendelea kujadiliana?


Kivipi maisha unsyoishi yathibitishe unachokitukuza na sio kitu kingine?



It's Scars
Ww mshindi.
 
Ni ile ambayo imethibitisha mungu yupo kihalisia bila kuacha utata

Kuna dini gani ambayo imewahi kuthibitisha hilo?

It's Scars
Hilo swali natakiwa mie ndiyo nikuulize wewe maana wewe ndiyo mwenye kujua dini ya kweli na ndiyo maana unasema hizi zengine sio za kweli. Nitajie hiyo ya kweli.
 
Huu ubishani unaoneshaje ya kwamba hakuna Mungu? Fafanua.
Uwepo wa huu ubishano unaonesha kua mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na upendo wote ambaye kila mahali yupo ni hadithi

Angekuwepo kila mtu angemjua bila ubishi yupo katika dhana ya kufikirika tu na ndio maana hathibitishiki yupo

Wewe unaweza kuthibitisha yupo kihalisia?

It's Scars
 
Back
Top Bottom