Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

110. Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka. (al Muuminuun : 110)

Sasa bibi hii aya mbona iko wazi kabisa inawazungumzia makafiri baada ya kuacha ukumbusho na kuwacheka waja wema, onyesha ushahidi unao onyesha kumcheka mtu dhalimu muovu anapo andika vya kuchekesha.

Lakini aya imesema walikuwa wana wacheka na haija sema "walikuwa wanajichekesha"

Ahsante.
Kwa hiyo ndiyo maana unacheka cheka hovyo kama hao makafir?

Muislam hakatzwi kucheka na kufurahi lakini kumbuka unajichekesha wakati hakuna cha kucheka. Sisi tunasema huo ni ubaradhuli.
 
Hilo swali natakiwa mie ndiyo nikuulize wewe maana wewe ndiyo mwenye kujua dini ya kweli na ndiyo maana unasema hizi zengine sio za kweli. Nitajie hiyo ya kweli.

Hukutakiwa kuuliza wewe na ndio maana mimi nimekuuliza wewe

Mimi ukiniuliza hilo swali mbona jibu rahisi tu kua "hakuna dini ya kweli"

Unaweza kunitajia dini ambayo ni ya kweli iliyoweza kuthibitisha mungu yupo kihalisia bila kuacha utata nje ya hadithi za kufikirika?

It's Scars
 
Uwepo wa huu ubishano unaonesha kua mungu mjuzi wa yote, muweza wa yote na upendo wote ambaye kila mahali yupo ni hadithi

Angekuwepo kila mtu angemjua bila ubishi yupo katika dhana ya kufikirika tu na ndio maana hathibitishiki yupo

Wewe unaweza kuthibitisha yupo kihalisia?

It's Scars
Kwanini kila mtu angemjua? Ni kipi kinafanya useme hivyo?
 
Zisaidie kwa namna ambavyo zinafundishwa kua ukiomba unasaidiwa

It's Scars
Bado sijakuelewa,maana dua zinaombwa kama kawaida sasa sijui wewe utawezaje kujua kuwa jambo fulani limefanikiwa kutokana na athari za dua?
 
Kwanini kila mtu angemjua? Ni kipi kinafanya useme hivyo?
Nikwasababu anauwezo wote na upendo wote

Angekuwepo asingeruhusu watu wasimjue wakati anaupendo wote

Angekuwepo kila mtu angemjua kwasababu huyu mungu anasifa ya kuwepo kila mahali

Amgekuwepo asingeshindwa kuwafanya watu wamjue kwasababu ni mungu muweza wa yote

It's Scars
 
Bado sijakuelewa,maana dua zinaombwa kama kawaida sasa sijui wewe utawezaje kujua kuwa jambo fulani limefanikiwa kutokana na athari za dua?

Sijakataa kua dua haziombwi, nakataa kua hakuna respond zinazoweza kuletwa kwa kuomba dua.

Na ndio maana nimekuambia dua ingekua inafanya kazi kwa namna ambavyo unaaminishwa, leo hii tusingeona mekka wakipiga ban watu wasiende kuhiji kwa hofu ya kupata corona wakati wangeomba dua wangeweza kuepuka

It's Scars
 
Hukutakiwa kuuliza wewe na ndio maana mimi nimekuuliza wewe

Mimi ukiniuliza hilo swali mbona jibu rahisi tu kua "hakuna dini ya kweli"

Unaweza kunitajia dini ambayo ni ya kweli iliyoweza kuthibitisha mungu yupo kihalisia bila kuacha utata nje ya hadithi za kufikirika?

It's Scars
Dini ziko nyingi na kila mmoja anasema yake ndiyo ya kweli na ana sababu zake,wewe nae umekuja na sababu zako za dini ya kweli ila unasema hiyo dini yenyewe ya kweli haipo.

Je vp ambao mungu wao ng'ombe ambae anaonekana na kushikika? Je watu wenye dini hiyo bado utasema dini yao ni ya uongo?
 
Dini ziko nyingi na kila mmoja anasema yake ndiyo ya kweli na ana sababu zake,wewe nae umekuja na sababu zako za dini ya kweli ila unasema hiyo dini yenyewe ya kweli haipo.
Sijasema dini haziko nyingi, na kila mmoja kusema dini yake ni ya kweli hiyo haifanyi dini hiyo kuwa kweli

Katika hao watu waliosema dini zao ni za kweli, walishathibitisha mungu yupo kihalisia bila kuacha utata??

Kama wako kinyume na hapo, wapo kinyume na ukweli

Je vp ambao mungu wao ng'ombe ambae anaonekana na kushikika? Je watu wenye dini hiyo bado utasema dini yao ni ya uongo?

Kuonekana na kushikika bado sio dhana ya kufanya ukubali jambo lolote

nitawauliza huyo ng'ombe ni mjuzi wa yote, uwezo wote, muweza wa yote na upendo wote kiasi aweze kuumba ulimwengu na vilivyomo?

It's Scars
 
Sijakataa kua dua haziombwi, nakataa kua hakuna respond zinazoweza kuletwa kwa kuomba dua.

Na ndio maana nimekuambia dua ingekua inafanya kazi kwa namna ambavyo unaaminishwa, leo hii tusingeona mekka wakipiga ban watu wasiende kuhiji kwa hofu ya kupata corona wakati wangeomba dua wangeweza kuepuka

It's Scars
Hujajibu swali la msingi kwanza,utawezaje kujua kuwa jambo fulani limefanikiwa kwa sababu ya dua zilizoombwa? Kwa sababu kama huna tabu na watu kufanya shughuli zao na huku wakiomba dua,maana yake huwezi kushangaa kwa waliyozuia kuhiji maana ni sehemu ya kazi yao kuzuia maafa(na huna tabu wanadini kufanya kazi zao). Inabaki kipengele cha dua,utawezaje kujua kwamba jambo fulani limekuwa hivyo kwa athari za dua?
 
Sijasema dini haziko nyingi, na kila mmoja kusema dini yake ni ya kweli hiyo haifanyi dini hiyo kuwa kweli

Katika hao watu waliosema dini zao ni za kweli, walishathibitisha mungu yupo kihalisia bila kuacha utata??

Kama wako kinyume na hapo, wapo kinyume na ukweli

Kuonekana na kushikika bado sio dhana ya kufanya ukubali jambo lolote

nitawauliza huyo ng'ombe ni mjuzi wa yote, uwezo wote, muweza wa yote na upendo wote kiasi aweze kuumba ulimwengu na vilivyomo?

It's Scars
Ndio maana nilisema hizo dini kila mmoja ana sababu zake za kuona dini yake ni ya kweli na chengine dini hutofautiana maelezo,sio kila dini inasema Mungu ni mmoja na ndiyo aliyoumba kila kitu na ana upendo n.k.

Inabidi ueleze huo uhalisia ni upi?
 
Nikwasababu anauwezo wote na upendo wote

Angekuwepo asingeruhusu watu wasimjue wakati anaupendo wote

Angekuwepo kila mtu angemjua kwasababu huyu mungu anasifa ya kuwepo kila mahali

Amgekuwepo asingeshindwa kuwafanya watu wamjue kwasababu ni mungu muweza wa yote

It's Scars
Kuna kuwa na sifa au uwezo wa jambo fulani na kufanya hilo jambo au kutofanya,sasa sijajua hoja yako ni ipi hapa? Maana kila jambo lina sababu yake, ukisema angekuwepo asingeshindwa kumfanya kila mtu amjue inabidi ueleze sababu zingemfanya aamue hivyo na si kuamua tofauti na hivyo?
 
Ukiwa unasifa ya uwezo wote hauwezi kushindwa katika jambo lolote ikiwemo na kuumba ulimwengu usio ruhusu ubaya

Ukiwa na sifa ya upendo wote hauwezi kuruhusu ubaya uchangamane na viumbe ambavyo unavipenda

Ukiwa na ujuzi wote hautakiwi kuhukumu wala kukasirika katika jambo ambalo ulikwisha lijua kua litatokea kabla hata halijatokea

Sifa hizi kuhusu mungu zinatakiwa zilenge uhasilia wa kile ambacho amekiumba, kukiwa na damage katika uumbaji wake kunaondoa dhana ya uwepo wake

It's Scars
 
Hujajibu swali la msingi kwanza,utawezaje kujua kuwa jambo fulani limefanikiwa kwa sababu ya dua zilizoombwa?
Hauwezi kujua kwasababu hakuna jambo ambalo limewahi kufanikiwa kwa dua, na ndio maana unaona watu hawajishughulishi na dua katika kutafuta suluhu ya corona

Unafikiri kama dua ingekua inafanya kazi, kulikua na sababu yeyote mekka kupiga ban muingiliano wa watu huko, Huku akijuja kua watu wanaoenda kule asilimia kubwa ni kwaajili ya kuhij??

Unafikiri hawakufika angle hiyo unayoidhania wewe?

Kwanini wasitumie dua iwe kama kinga badala ya kufunga mipaka ambayo ni recommendation na shirika la afya??

Kwa sababu kama huna tabu na watu kufanya shughuli zao na huku wakiomba dua,maana yake huwezi kushangaa kwa waliyozuia kuhiji maana ni sehemu ya kazi yao kuzuia maafa(na huna tabu wanadini kufanya kazi zao). Inabaki kipengele cha dua,utawezaje kujua kwamba jambo fulani limekuwa hivyo kwa athari za dua?
Kwanini wazuie watu wasiingie kwao badala ya kuzuia ugonjwa usiwadhuru kwa kuomba dua??

Dua ingekua inafanya kazi leo hii isingetumika nguvu kubwa ya kufunga mipaka huko mekka

Kwasababu dua ingeweza kudhibiti ugonjwa usiweze kumdhuru mtu ambaye katoka umbali mrefu kuja pale kufanya ibada kwa ajili ya mungu

Yani badala ya kuzuia ugonjwa kwa kuomba dua, unazuia watu kwa kufunga mipaka halafu mkisalimika useme allah kawanusuru huo si zaidi ya ujinga?

It's Scars
 
IMG_20200324_145724_268.jpeg

It's Scars
 
Ukiona narudia swali ambalo kwako unahisi umelijibu basi lirudie jibu lako halafu lipime

Hali halisi ni nini?

Kwanini hali halisi ithibitishe mungu na sio kingine?

Unajuaje kua watu hawakutumia kichaka cha "hali halisi" ili kuweka ulaghai wao kama conspiracy theory??

It's Scars
Hili nimeshalijibu.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote amabaye amenukuliwa katika hivyo vitabu angekuwepo kusingetokea majanga ya magonjwa kama haya

Kuwepo kwa haya magonjwa kunaonesha mungu huyo hayupo na hivyo vitabu vilivyo andika habari zake ni vya uongo

It's Scars

Majanga yanayo tokea majini na baharini, yote anayaleta Allah na kuruhusu yatokee na ni chumo la mikono yetu.

Anasema Allah aliye juu :

41. Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu. (ar Rum : 41 )
 
Kabla ya kwenda huko

Wewe umekubali kua hoja yangu kutoafikiana na hoja yako haifanyi hoja yako kua jibu sahihi?

It's Scars
Acha kukimbia maswali, na huku kunathibitisha ya kuwa huna hoja zaidi ya kuruka kuruka.

Una deni toka kwangu.
 
Back
Top Bottom