Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

UKwaiyo unakubali kua ugonjwa huu ni mpango wa allah kuwadhuru watu sio?

It's Scars
Nilikwambia lengo sio kuwadhuru, bali lengo ni kuwapa mtihani na kuwazindua ila ameruhusu ugonjwa uwadhuru watu.

Usirudie maswali ambayo umeshajibiwa.
 
Imeandikwa usimjaribu bwana Mungu wako. Wewe umeona corona ndio kipimio cha uwepo wa Mungu? Tafakari tena.
 
Ukiwa unasifa ya uwezo wote hauwezi kushindwa katika jambo lolote ikiwemo na kuumba ulimwengu usio ruhusu ubaya

Ukiwa na sifa ya upendo wote hauwezi kuruhusu ubaya uchangamane na viumbe ambavyo unavipenda

Ukiwa na ujuzi wote hautakiwi kuhukumu wala kukasirika katika jambo ambalo ulikwisha lijua kua litatokea kabla hata halijatokea

Sifa hizi kuhusu mungu zinatakiwa zilenge uhasilia wa kile ambacho amekiumba, kukiwa na damage katika uumbaji wake kunaondoa dhana ya uwepo wake

It's Scars
Sijaona nafasi ya yeye kuamua anavyotaka naona unaeleza lazima afanye hivi mara vile,hii ikoje?
 
Ukweli ni kwamba
Huijui DINI vile ambavyo inatakiwa uijue
Nadhani anaijua dini vizuri tu. Tena ukute ni konki wa imani. Alichoandika ni kweli kinafikirisha sana.

Kumbuka dunia ya leo tunao hadi wanaojiita Mitume na Manabii na wanachofanya mnakijua, sio kuhubiri habari njema.

Ninachoamini Mimi ingetokea hakuna michango na sadaka HAKIKA WANGEKUWEPO WATUMISHI WA KIROHO WA KWELI, ngazi ya kina Elia ya kumuambia Mfalme kabla hujafika kwako Mvua itashuka. Ya kumuambia Mfalme enenda kajitumbukize mtoni Mara 3 kisha ugonjwa wako utatoka.

Hata Mimi naona Kipindi hiki ndicho tungesikia kama wanavyofanya kuita wenye shida za uvimbe tumboni, ugumba, kukosa kazi, mume, gari, gesi tumboni nk. Halafu mwishoni msisitizo wa kumtolea bwana
 
Ni uthibitisho!
millardayo_B-BMGO4A-aJ.jpeg
 
Hauwezi kujua kwasababu hakuna jambo ambalo limewahi kufanikiwa kwa dua, na ndio maana unaona watu hawajishughulishi na dua katika kutafuta suluhu ya corona

Unafikiri kama dua ingekua inafanya kazi, kulikua na sababu yeyote mekka kupiga ban muingiliano wa watu huko, Huku akijuja kua watu wanaoenda kule asilimia kubwa ni kwaajili ya kuhij??

Unafikiri hawakufika angle hiyo unayoidhania wewe?

Kwanini wasitumie dua iwe kama kinga badala ya kufunga mipaka ambayo ni recommendation na shirika la afya??



Kwanini wazuie watu wasiingie kwao badala ya kuzuia ugonjwa usiwadhuru kwa kuomba dua??

Dua ingekua inafanya kazi leo hii isingetumika nguvu kubwa ya kufunga mipaka huko mekka

Kwasababu dua ingeweza kudhibiti ugonjwa usiweze kumdhuru mtu ambaye katoka umbali mrefu kuja pale kufanya ibada kwa ajili ya mungu

Yani badala ya kuzuia ugonjwa kwa kuomba dua, unazuia watu kwa kufunga mipaka halafu mkisalimika useme allah kawanusuru huo si zaidi ya ujinga?



It's Scars
Ndio maana nilikuuza unataka watu wasifanye kazi na badala yake waombe dua tu? Maana hapo ndiyo hoja yako ilipo,kama ulitaka watu wasijikinge na maradhi na badala yake wao waombe dua tu ni sawa na kutaka watu wasifanye kazi pia wala kushughulika na taaluma zao ila wakae tu na kuomba kwa kila jambo. Na ndio maana unaleta hoja ya watu kuacha kukaa na kuomba tu dua kwa ajiri ya corona wao wanatumia taaluma zao kutafuta suluhu ya corona.

Upo nje ya uhalisia hakuna dini inayofundisha kwamba watu wakae na kutegemea dua tu, hata hivyo walivyozuia watu kwenda kuhiji ni mafundisho ya dini yao pia hufundisha hivyo mbali na ushauri wa shirika la afya.

Kuhusu dua kujibiwa nilitoa mfano wa lile tatizo la magonjwa ya akili na nikakwambia hilo tatizo hutatuliwa kwa dua na watu wanapona. Lakini pia kuna watu wao kazi zao ni kuwafanyia watu dua,sasa ukiniambia kuwa dua huwa hazina majibu basi hawa watu wasingefanya kazi hizo maana hazina majibu na hivyo wasingekuwa na maclients.
 
Hili nimeshalijibu.
Hujajibu hili swali

Hali halisi ni nini?

Kwanini hali halisi ithibitishe mungu na sio kingine?

Unajuaje kua watu hawakutumia kichaka cha "hali halisi" ili kuweka ulaghai wao kama conspiracy theory??

It's Scars
 
Majanga yanayo tokea majini na baharini, yote anayaleta Allah na kuruhusu yatokee na ni chumo la mikono yetu.

Anasema Allah aliye juu :

41. Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu. (ar Rum : 41 )

Kabla ya kuweka hizo nukuu nambie hicho kitabu umejuaje kua kimesema ukweli?

It's Scars
 
Back
Top Bottom