Anabaki kua mungu katika dhana ya kufikirika na sio uhalisia
Ni sawa na mtu anayesema spiderman anabaki kua spiderman kusema kwake huko hakufanyi spiderman awepo kihalisia
It's Scars
SASA NAKUJULISHA SIFA ZA MUNGU WANGU NINAYE MUAMINI
Mwenyezi Mungu ameelezewa sana ndani ya Quran tukufu kwa maneno haya;
Mwenyezi Mungu ambaye ndiye muumba wa vitu vyote hafanani na chochote na wala hana mfano wake.
Hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hafanani na chochote. Yeye pekee ndiye anayestahili kuabudiwa na kuombwa msaada. Yeye hahitaji msaada wa mtu yeyote kwa sababu yeye ndiye muweza wa kila jambo.
Yeye hana sifa za wanadamu au viumbe vyenye uhai kama vile kula, kunywa, kulala, kupata uchovu na kadhalika.
Yeye ni Mwenyezi Mungu pekee asiyekuwa na miungu mingine.
Yeye ndiye mmiliki wa kila kitu, mlinzi wa viumbe vyote na anayejaalia riziki viumbe vyake duniani.
Yeye ndiye anayedhibiti kila kitu alichokiumba na hakuna yeyote anayeweza kufikia sifa zake kamwe.
Yeye pekee ndiye anayetambua mwanzo na mwisho wa dunia. Yeye ndiye aliyeumba kila kitu kwa kipimo chake na kukiwezesha kuwa kama kinavyoonekana.
Yeye hufanya kitu kutokea kwa amri yake. Hakuna kitu chochote kinachowezekana pasi na Mwenyezi Mungu kutaka.
Hata jani kavu la mti haliwezi kudondoka bila ya amri yake yeye Mwenyezi Mungu.