battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,712
- 2,577
Sana tu ,naweza kukubali kuwa biblia ni kitabu cha mungu kwa vile ndani ya biblia ipo injili,Taurati,Zaburi na Vitabu vya manabii ambavyo hivyo vimetajwa ndani ya Qur-an wala havina shaka.Unajuaje kua akili yako haijakengeuka?
Mkristo akisema biblia ni kitabu cha kweli kwasababu akili yake imekubali, we utakubali kua biblia ni kitabu cha mungu kweli?
Ila kwa vile akili ninayo ,naweza kubaini vitabu vilivyochomekewa kwa maandiko ya wanadamu, na utavijuwa kwa kukengeuka kwake vitabu vyaa asili.
Hebu tazama haya mafundisho yanayofanana na Qur-an wala hayana shaka.
“Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili AKUTWEZE, KUKUJARIBU kuyajua YALIYO MOYONI MWAKO, kwamba UTASHIKA AMRI ZAKE, AU SIVYO. Akakutweza, AKAKUACHA UONE NJAA, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; APATE KUKUJULISHA YA KUWA MWANADAMU HAISHI KWA MKATE TU, BALI HUISHI KWA KILA LITOKALO KATIKA KINYWA CHA BWANA.” (Kumbu.8:3,4).
Unaona? Ni kusudi la Mungu tujaribiwe ili TUKUE katika imani, haki na utakatifu. Mambo mengi yanatokea, siyo kutuadhibu au kutuangamiza, ila kutupeleka TUKUE katika imani na katika Kristo Yesu. Ndio maana maandiko yanasema, “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.” (Yakobo 1:2-4). Na tena, “mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini.” (Warumi 5:3,4).
Kumbuka Mungu alimuacha Yohana auwawe na watu wale waovu,si kwa kushindwa,au kuto kuweza kuwadhibiti,laa bali ni kuonesha kwamba Kifo kwake si chochote si lolote,kwani hata haya misha ya dunia ni sehemu ya majaribu tuu ili urejeshwe kwenye ile Paradeso iliyopotea.ya Asili.