Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa

Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa

Hii misaada si ndio mtaigeuza kama ile ya kule Bukoba.. na baadae tutaambiwa " kwani mi ndiye nimeleta corona"
 
Wakuu nianze kwa kusema hivi ugonjwa huu inaweza kuwa season disease, nadiyo rahisi kumshsmbulia mtu mweusi kwa maans immunity ya black people ni strong. Kulingana na factor ya ukuaji. Nin maana yangu
Inaweza ikawa world economic crisis. Ila kwa sababu na sis waafrika tupo duniani tujiadhari tuu. Ila issues ya COVID- 19
Siyo kwa ajili ya mwaafrika. Otherwise hyo mwasfrika hawe na gane za watu weupe
Nawasilisha hoja wazeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa kinachoendelea Italia na Hispania haukupashwa kuandika hivi Mkuu wangu Your Majesty Mkuu sana P.
Kule ni ulaya, Corona sio tropical diseases.
Ni ugonjwa wa Wazungu. Uliisha wahi kusikia mswahili anakufa kwa mafua?.
P
 
Wanabodi,

Kuna msemo wa Kiswahili usemao "Kufa Kufaana", wakati watu wanahangaika na janga la Corona, wengine wanaangazia namna ya kutumia changamoto kuzibadili kiwa fursa, yaani turning problems, obstacles, challenges or adversaries into opportunities.

Tangu dunia na taifa letu kukumbwa na janga la ugonjwa wa Corona, Tanzania kama Taifa, tumepanic, kila mtu ni mtaalam wa Corona, Viongozi wa serikali wakiwemo wataalamu wetu wa afya wanatoa contradictory statements kwenye media tena mbele ya Waziri wa Afya, elimu ya jinsi ya kujikinga inayotolewa ni elimu duni, hatuna vifaa vya usafi kwenye public places zetu ni mwendo wa vitisho na panic kwa kwenda mbele huku hakuna elimu yoyote proper inayotolewa na chombo chochote cha habari zaidi ya uhamasishaji wa kinga ili kuzuia.

Bandiko langu sio la kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa Corona au jinsi ya kujikinga, bali mimi naangazia fursa za Corona.

Kwenye kila changamoto, pia huwa kunajitokeza fursa. Concentration kubwa sasa ni kinga watu wame panikishwa na kuiona Corona kama balaa kubwa la ajabu hivyo tuko kwenye chaos hivyo kazi yangu mimi ni kuwatuliza na kuwapa michongo ya fursa mbalimbali zinazoletwa na janga hilo la Corona kwa hoja kuws japo Corona ni janga, lakini pia ni fursa, Watanzania tusiishie tuu ku concentrate kwenye janga la Corona tukajisahau kabisa na kushindwa kuziangazia fursa za Corona. Janga la Corona linaandamana na fursa mbalimbali, mfano tayari Benki ya Dunia, WB imemwaga mihela ya kufa mtu kwa ajili ya kufidia mdororo wa Kiuchumi unaosababishwa na Corona.

Kwavile tangu kulipuka kwa ugonjwa huu wa Corona, so far hakuna Mtanzania yoyote aliyeambukizwa virusi vya Corona akiwa nchini Tanzania, waathirika wote 6 waliogungulika Tanzania so far, hakuna hata mmoja aliyeambukizwa Corona nchini Tanzania, wote wameambukizwa virusi vya Corona huko waliko ambukizwa, na kuvileta hapa nchini lakini licha ya ku interact na watu wote walio changamana nao, hakuna hata Mtanzania mmoja aliyeambukizwa virusi vya Corona, hivyo at this moment naweza kusema, ugonjwa wa Corona ni ugonjwa wa wazungu huko huko nchi za ulaya zenye baridi na hata mgeni akija Tanzania na virusi vyake, atabaki navyo mwenyewe, Watanzania hatuambukiziki, hivyo sasa tupunguze panic ya ugonjwa wa Corona, lets compose ourselves tuchangamkie fursa mbalimbali zinazoletwa na ugonjwa huu wa Corona.

Fursa hizi ni za aina mbili, fursa za kitaifa kama Tanzania as nchi kuchangamkia fursa hii ya World Bank
World Bank Group Increases COVID-19 Response to $14 Billion To Help Sustain Economies, Protect Jobs

Fursa nyingine ni kama hizi
Hapa sasa naomba Watanzania wenzangu wenye jicho la kiangazia fursa mbalimbali
  1. Fursa za uandaaji wa vipindi vya redio, television na online vya uelimishaji umma kuhusu ugonjwa wa Corona, yaani public information Programs, sasa ni kila mtu anasema lake, nilimshuhudia mtaalamu wa Afya, Daktari bingwa akiwa mbele ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akizungumzia uvaaji wa mask, kiukweli alichemsha na analiingiza chaka taifa zima, hivyo nikaona hapa kuna fursa, kama hata Waziri wa Afya hajui kuhusu masks na anaingizwa chaka, vipi kuhusu sisi akina kajamba nani?.
  2. Serikali inasisitiza kutumia running water lakini hatuna vifaa vya running water kwenye public places kama hivi​
  3. Hivyo ukitengeneza hivi na kuviuza, afisi zote, public palaces zote, maduka yote, vituo vyote vya mabasi, stendi zote, vituo vya dala dala, masokoni etc, what an opportunity?
  4. Watanzania tunahimizwa kutumia hand sanitizers, hatuna sanitizers za kutosha Watanzania wote. Hivyo hii ni fursa kwa simple home made sanitizers kutumika, the simplest ni maji ya chumvi, chumvi ya kawaida ina clorine, tengeneza maji ya chumvi, pack, piga pesa!.
  5. fursa ya watu kununua ma dumu makubwa ya real sanitizers na kuyapack kwenye vichupa vidogo na kuuzia watu, japo kwenye hili, huwezi zuia matapeli kujaza maji mengi na kuweka vitone tuu vya sanitizers kuweka harufu.
  6. Soon mtashuhudia wale wauza ukwaji wa Bhakresa wakiuza sanitizers.
  7. Tuendelee kuweka fursa mbalimbali nitakuwa nazi update hapa.
Kwa wale wa Ibada leo, Ijumaa Kareem,
Kwa wale wenzangu na mimi, nawatakia Furahi Dei njema, sisi wa maji makali, Corona haituhusu!.

Paskali.
Unaijua hii nchi kweli?
Wewe na ppr yako mpaka sasa umetulia,
Utatengeneza na serikali inaweza pata hela na isinunue wkazipeleka kujenga nyerere power plant

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paschal hatuna mswada mpaka sasa nawakati naigeri na south tayar wamepitisha Jana,
Unaenda kuomba huna wazo mezani, tayar Zanzibar hawapati fedha za utalii je tunawasaidiaje?


Taasisi za utalii zimeathirika tutalinda vipi ajira? Tunasubir kamati za kawaida ziendelee kukaa badala ya bunge zima,

Labda tumuulize Mpango kamati yake imemaliza tathimini? Na hili litakuwa sehemu ya pendekezo lao?

Hizi ni baadhi ya hoja tuone kama tunaweza pata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kule ni ulaya, Corona sio tropical diseases.
Ni ugonjwa wa Wazungu. Uliisha wahi kusikia mswahili anakufa kwa mafua?.
P

Hii sio sayansi ni ujinga. Mtu mzima kukumbatia ujinga proudly ni jambo la aibu, ingekuwa kwingine usinge jitambulisha kama mwandishi wa habari tena watu wakakusoma.
Mzungu asiye na elimu kama unayo wewe angesema publicly gonjwa X ni la weusi akimaanisha wasijihangaishe nalo, ungelia ubaguzi, rightfully. Lakini pamoja na elimu yako unajiwekea standard tofauti.
 
Mkuu Paskali,
kuna haja ya kuchukua tahadhari, maana Deputy President wa Bunge wa Bukinabe (Bukinafaso) katuacha kwa korona hii hii.

Burkina Faso reports Sub-Saharan Africa's first coronavirus death as WHO warns 'prepare for worst'

Kuna wengine kinga zao sio imara sana humu humu kwenye ngozi nyeusi yenye rutuba
Mkuu Freddie Matuja, huyu jamaa alikuwa na tatizo jingine la kiafya, hivyo Corona ikawa ni kama kumpiga tuu teke chura. Sisi Watanzania umeisha wahi kusikia mtu kafa kwa mafua?.
P
 
Hii sio sayansi ni ujinga. Mtu mzima kukumbatia ujinga proudly ni jambo la aibu, ingekuwa kwingine usinge jitambulisha kama mwandishi wa habari tena watu wakakusoma.
Mzungu asiye na elimu kama unayo wewe angesema publicly gonjwa X ni la weusi akimaanisha wasijihangaishe nalo, ungelia ubaguzi, rightfully. Lakini pamoja na elimu yako unajiwekea standard tofauti.
Ukiwa mkweli kupindukia ni tatizo!. Kuna magonjwa ni tropical diseases yanaua watu kuliko Corona ikiwemo malaria, Corona sio tropical disease hivyo tuendelee kuchukua tahadhari lakini so far as of now, hakuna Mtanzania yoyote ameambukizwa Corona from within, hivyo I'm right mpaka itakavyo kuja kuwa proved otherwise wise.
Mimi ni mkweli daima regardless ukweli huo utamfurahisha nani na kumuudhi nani.
Pole.
P
 
Ukiwa mkweli kupindukia ni tatizo!. Kuna magonjwa ni tropical diseases yanaua watu kuliko Corona ikiwemo malaria, Corona sio tropical disease hivyo tuendelee kuchukua tahadhari lakini so far as of now, hakuna Mtanzania yoyote ameambukizwa Corona from within, hivyo I'm right mpaka itakavyo kuja kuwa proved otherwise wise.
Mimi ni mkweli daima regardless ukweli huo utamfurahisha nani na kumuudhi nani.
Pole.
P

You are an educated fool.
Kusema hamna mtu aliyeambukizwa ni jambo moja, kusema hauambukizi watu wetu ndani ni wehu na sijui una nia gani.
 
Wote walio interact na yule first victim, wamechukuliwa sample na ikaletwa maabara Dar ikapimwa, so far bado hakuna maambukizi yoyote locally.
P
P na wewe Ni mfatiliaji wa habari za Corona kweli au umeikurupukia tu upande wa fursa?

Habari za Corona tunazozisikia Ni kuwa vipimo vinaweza kudetect virus baada ya mtu kuwa exposed 1-14 days, Sasa hata siku 7 bado tayari unavimba kifua hakuna contact aliyeambukizwa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofautisha kuiombea Corona ije, na kuchangamkia fursa za Corona.
P
Najitahidi kuiona tofauti lakini so far sijaipata..kuifanya Corona fursa na kuiombea Corona ije!

Hembu tupe reference ya bandiko lako la nyuma linaloelezea tofauti labda nitakuelewa mkuu paskali..

Kama Corona Ni fursa then si Ni sahihi kuiombea fursa ije??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hero, Chief Salute umeongea point kubwa..
Nadhani Kuna mahali blabla za bwana huyu zinaweza kufaa lakini sio kwenye maswala haya ya afya yenye kuhusisha zaidi uhai wa watu..

Leo siku ya 5 tu tayari mwanahabari huyu Mwenye utaalamu wa Mambo ya afya anatuambua huu ugonjwa sio wa watanzania maana hakuna mtanazania aliyeambukizwa Tanzania. Daah..

Paskali this is too low of you

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujiliwaza kuwa watu wasipaniki ni ujinga. Nchi zilizoendelea zinaadhirika sana kwa sababu watu wanaopanda ndege kwenda na kutoka oversees ni wengi, chukulia mfano wilaya ya kinondoni ni wangapi kwa mwezi mmoja wametua na kuruka oversees linganisha na wilaya kama hii Roma au Madrid utaona Kyle ni wengi na hapa ni wachache! Uwezekano wa waambukizi ni mkubwa Kyle kuliko nchi zetu, hasa Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu,Corona imekuwa blown out of proportion na vyombo vya habari,na sisi tumelibeba kama lilivyo.Hatujui au tumesahau kwamba wao wana agenda ya kuleta hofu.Hofu yenyewe ni silaha mbaya,kwa kuwa kwa hiyo unapata magonjwa na kwa hiyo you are easy to control and manipulate.
So habari ya vifo 450 kwa siku moja kutokana na Corona Ni propaganda za mabebero na washirika wao wanahabari eti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom