Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa

Pascal Mayalla,
Naona Kama unataka kutukosesha na mabilioni ya world bank,yaani unatufanya tukose za watalii waliotufanya tusifunge mipaka yetu na hizo za world bank za kubust uchumi. Kama wagonjwa wetu wanachangamana na wananzengo na still hawaambukizi watakuwa ni China products nini? Mkuu dadavua hapo
 
Pascal Mayalla,
Mkuu sisi ni dona kantri,tena siyo nchi maskini,wala hatuhitaji msaada wa
mabeberu wa America&Ulaya.

Kama tumeweza kufanya miradi mikubwa kwa pesa za ndani,Corona
tutaiweza,tutembee kifua mbere!
 
Nnakumbuka kipindi kile Mmarekani alipoibukia kiuchumi wakati nchi zingine zikipambana, sasa hivi nchi nyingi wanajifungia ndani, uzalishaji unapungua, sisi kama watanzania tuliopewa hii neema, angalau Covid-19 haijasambaa, ingekuwa fursa kwetu, kuangalia hawa watu waliojifungia huko ndani katika nchi zao, watakutana na hali ngumu mtaani hasa katika chakula.

Mvua bado zipo, tungelima sana sasa hivi, chakula kitauzika sana nje, wabongo tumelifikiria hili kweli, huu ndio wakati wetu wa kupanda kiuchumi SWOT Analysis, tukishindwa kutumia advantage ya corana basi tena.

(Ni wachache sana wananielewa) ninarudia tena ( huwezi nielewa kama unauwezo mdogo wa kufikiri)

Hivyo yaani!
 
We need to apply SWOT analysis kwa haraka sana
goldcall,
NA kweli aiseee hapa ni akili kumkichwa ya kuambiwa changanya na yako. KWenye SWOT hapo kila mmoja atakuja na hoja tofauti ila kwa uelewa watu unatakiwa kuiapply kwa akili yako na mazingira yako ulipo usitake mpk fulani afanye ndio uige wakati mazingira na fursa ni tofauti utafakuri yakinifu wahitajika ila muda ni mali
 
Mkuu kwa ulivoongea angekuwa karibu nadhani ungempiga bonge la kibao
 
Corona Update Jumatatu Machi 30, 2020.
Tuna wagonjwa 19
Kati ya hao 16 wamekuja nayo kutoka inje.
3 wameambukizwa direct na hao waliotoka nje kutokana na close interactions
So far bado hakuna Maambukizi yoyote ya Corona locally, yaani local to local transmissions, Corona yote nchini kwetu ni imported.
Ki epidemiology vurusi vya Corona bado havijaweza kufanya mutation locally, hivyo Watanzania tuendelee kufuata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga na tuendelee kufuata ushauri wa rais wetu Magufuli, tusitishane, Watanzania tuendelee kuchapa kazi.

Fursa zinaendelea.
P
 
Fursa hizi ni za aina mbili, fursa za kimataifa kwa Tanzania kama nchi kuchangamkia fursa hii ya World Bank
World Bank Group Increases COVID-19 Response to $14 Billion To Help Sustain Economies, Protect Jobs

P.
Hii ni fursa.
Haya sasa, hapa ni unaangalia tarehe ya bandiko hili, unaangalia tulishauri nini, na lini, kisha unatembelea hapa,
Tanzania yaomba Mkopo wa USD mil 198 kupambana na Corona. Yahisi hali mbaya ya kiuchumi - JamiiForums
Unasoma hiyo tarehe ya barua,
Then unajiuliza kama rais Magufuli angeitumia jf kama sehemu ya washauri wake Tanzania tungekuwa wapi?.
This is "A stich in time saves nine!".
Tulishauri humu, tusisubiri madhara ndipo tuombe misaada, baada ya kuons kwa wenzetu, sisi tujiongeze kwa kuwa more preparedness before its too late na sio tusubiri hadi tuathirike.

Angalau sasa serikali yetu imefanya the right thing kwenye hili and it's not too late kufanya hayo mengine yanayoshauriwa humu katika kukabiliana na Corona.

P
 
Mkuu Michael Makene, asante nimekisikia, na karibu mitaa hii.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…