Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,320
- 18,599
Acha propaganda za kitoto.Tusiposhikamana na kuamka sote, tatizo hili la Corona litatumaliza.
Moja kwa moja kwenye mada. Nimejipa wakati kuzungukia katika miradi kadhaa ambapo labda mabeberu nao walikuwa na mchango (makandarasi, washauri, wataalamu, wafanyakazi nk). Wote wameshamwaga mbio na kutuacha kurudi makwao.
Haiyumkiniki hata wale wa South Korea wa ku commission zile meli ambazo na pesa tulishawalipa, suala si ndege kuja, bali haiwaingii akilini ni vipi watu na akili zao timamu wanaweza kufikiria kuendesha maisha wakimchukulia Corona kama mshikaji wao tu.
Wengine wa karibuni wanaotukimbia tena ni hawa hapa:
Kenyans in Tanzania to be evacuated on Monday
Eeh mola wetu Farao alisalimu amri katika somo la kumjulisha mkuu alikuwa nani.
Hebu ukawaguse hawa viongozi wetu wakajue wanayo dhamana katika kuyahami maisha ya watu wao. Wakaweze kutambua maisha ya binadamu katu hayawezi kufananishwa na rupia.
Sasa unataka tuchukue hatua zipi zaidi ya elimu inayotolewa kujikinga dhidi ya Corona?
Unatakaje sasa?
Acheni unafiki wazee, hii nchi ikifungwa hata wiki tu zaidi ya 80% ya watanzania hoi hata mlo wa siku moja haupatikani tutaanza kukabana kupata hata kopo la unga tu.
Huwezi kukaa ndani ukaangalia watoto wako wanakufa kwa njaa utalazimika kutoka liwalo na liwe hiyo ndo itakua kauli yako huku ukimtusi Rais wazi wazi.
Usijilinganishe na wale waheshimiwa wanaohimiza tuweke karantini nchi ilihali hawatatoa hata kilo ya unga kwa mwananchi wa manzese
Sent using Jamii Forums mobile app