Corona: Misiba mitaani imekuwa mingi mno. Hii siyo kawaida

Corona: Misiba mitaani imekuwa mingi mno. Hii siyo kawaida

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na mabwana takwimu ni muhimu kwa binadamu kuweza kujitathmini au hata kuchukua tahadhari mahsusi.

Jana Baraza la maaskofu TEC limetoa takwimu zao. Ndani ya siku 60 zilizopita kanisa katoliki peke yake limepoteza Mapadre 25 na Masista 60. Wapumzike kwa amani waja hawa wa mola.

Mapadre na Masista hawa, hawakuweza kujilinda na ugonjwa huu. Vivyo hivyo hata kwa madaktari wetu kadhaa bingwa, sembuse sisi kwenye ma dala dala, ma ferry, masoko na magulio?

Za katoliki ni takwimu za kuwahusu vigogo wao huko tu. Vipi kuwahusu waumini wa kawaida? Vipi huko KKKT? Vipi waislam? Vipi walokole? Vipi serikalini? Vipi uswahilini? Nk.

IMG_20210304_212127_511.jpg


Mitaani tunakopaona, hali ni tete sana. Imekuwa bandika bandua misiba misiba tu.

Pana hatari kuwa tunaweza kuwa tunapoteza watu wengi labda kuliko hata huko tunakoaminishwa bila takwimu za kwetu kuwa huko wao ni zaidi mno.

Kwamba hali hii ya vifo ingeweza kudhibitiwa kwa serikali kufanya wajibu wake tu, ni jambo la kufikirisha sana:

IMG_20210304_213802_073.jpg


Kwamba taathimini ya uchaguzi mkuu iliyotoka leo inanyooshea kidole uhalali wenu?

Ni vyema mngejitoa kimasomaso mkatambua kuwa nyie kama wawakilishi wetu mnalazimika kuzisikiliza sauti zetu.

Kutozisikia sauti zetu kunatufanya kuyakumbuka yale mabegi meusi ya kura ambayo tungependa mno kuyasahau.

Ninawasilisha.
 
Mimi kwa sasa simu ikilia tu najua tayari, simu za misiba zimekuwa nyingi sana kuliko Ukimwi wa miaka ya90.

Mimi mwenyewe nikijsikia dalili za mafua tu nakosa raha kabisa naanza kuwaza kuwafikiria Watoto wangu hawa wadogo na usingizi sipati.
 
Watu wenye uzito mkubwa (obesity) wapo hatarini zaidi kufa kwa korona kuliko wengine Most virus deaths recorded in nations with high obesity levels: analysis nchi zenye vifo vingi zaidi ndo nchi zenye watu wenye uzito mkubwa kupindukia! Asilimia kubwa ya wanaokufa hapa bongo naona ni watu wenye vitambi au umri mkubwa au vyote, tufanye mazoezi ndugu zangu.
 
Tunatishana Sana!
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Kutisha au kutishwa maana yake nini?

Unatishwa vipi na taarifa za ukweli ewe mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Kwenye red si wajibu wako?

IMG_20210304_213802_073.jpg


Ukweli haujawahi kutisha. Sana sana ukweli ni mchungu. Ukweli huuma na msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
watu wenye uzito mkubwa ( obesity ) wapo hatarini zaidi kufa kwa korona kuliko wengine Most virus deaths recorded in nations with high obesity levels: analysis nchi zenye vifo vingi zaidi ndo nchi zenye watu wenye uzito mkubwa kupindukia ! Asilimia kubwa ya wanaokufa hapa bongo naona ni watu wenye vitambi au umri mkubwa au vyote, tufanye mazoezi ndugu zangu

Wenye umri mkubwa unawashauri vipi?

Maalim wala balozi hawakuwa na vitambi wala hawakuwa na obesity.

Ni wajibu wa jamii na serikali kuwahami walioko hatarini zaidi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kijana mvaa kaunda suti mpeni barakoa ya mgonjwa aende kwa wakubwa awaambukize atakuwa shujaa wa Taifa
 
Kwa sasa Taifa letu limeelekezwa kwenye mrengo wa ushirikina halafu anasingiziwa Mungu

Raisi wetu mpendwa aukubali tu mrengo wa kisayansi huku kungamia kwa Watanzania wasiokuwa na hatia kunatisha
Mrengo gani wa kisayansi?
 
Binafsi sina yeyote ninamjua ambae amefariki kwa Covid-19 kuanzia phase 1 mpaka sasa Phase 2
 
Mimi kwa sasa simu ikilia tu najua tayari simu za misiba zimekuwa nyingi sana kuliko za Ukimwi wa miaka ya90.

Mimi mwenyewe nikijsikia dalili za mafua tu nakosa raha kabisa naanza kuwaza kuwafikiria Watoto wangu hawa wadogo na usingizi sipati.
Hapa nipo kwenye msiba wa rafiki yetu baada ya kufariki kwa changamoto ya upumuaji na kesho mida ya saa saba marehemu anatarajiwa kusafirishwakuelekea Mbeya kwa maziko. Nashukuru wahudhuriaji wamechukua tahadhali zote za kujikinga na Corona kwa kuvaa barakoa na kukaa mbalimbali kila sehemu kukiwa na ndoo za maji tiririka.

Mungu aliepushe taifa letu katika hii kadhia ambayo viongozi wetu baada ya kusa wafariji wakuu wamegeuka kuwa wauwaji. Narudia tena kusma kula wamegeuka kula wauaji
 
Back
Top Bottom