Corona: Misiba mitaani imekuwa mingi mno. Hii siyo kawaida

Corona: Misiba mitaani imekuwa mingi mno. Hii siyo kawaida

watu wenye uzito mkubwa ( obesity ) wapo hatarini zaidi kufa kwa korona kuliko wengine Most virus deaths recorded in nations with high obesity levels: analysis nchi zenye vifo vingi zaidi ndo nchi zenye watu wenye uzito mkubwa kupindukia ! Asilimia kubwa ya wanaokufa hapa bongo naona ni watu wenye vitambi au umri mkubwa au vyote, tufanye mazoezi ndugu zangu
Endelea kujidanganya ,Amo Blaze,Cpwaa walikuwa Mabonge Nyanya na wazee? Umuhimu kuwa na kinga imara regardless u mzee,bonge au kimbaumbau.
 
Naona kasi ya kutetea msimamo wa boss wao umepungua. Kutetea misimamo ya jiwe unatakiwa uikane elimu uliyokuwa nayo kwanza.

Wamekuwa wapole. Ni wazi kuwa si nyungu, maombi wala zile juice za NIMRI zinazohitajika bali kuchukua hatua stahiki na chanjo haviepukiki tena.

Tusipoamka mbona tunasererekea kwenye yale ya kina Melinda na Bill Gates?
 
Sawa mkuu, nimerekebisha pale juu
Kuweni na huruma na maisha ya watu.

Gharama ya kuepuka vifo hivi ni chanjo ambayo ni bure na kuwahami walioko hatarini zaidi ambapo kunahitaji utashi wa serikali tu.

Mnanufaika nini na vifo hivi kuukumbatia upotoshaji huu mnaouendekeza?
 
Wenye umri mkubwa unawashauri vipi?

Maalim wala balozi hawakuwa na vitambi wala hawakuwa na obesity.

Ni wajibu wa jamii na serikali kuwahami walioko hatarini zaidi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Nimemshamgaa sana huyu jamaa,nilitaka nimtajie watu waliokufa bila kuwa na vitambi,Ila nilipoona jina lake japo juu,HUNIJUI SIKUJUI,nkaamua kupiga kimya.
 
Tunatishana Saana, embu tuacheni tupumue

Kufa haitakuja izoeleke hata siku moja, lakini tuseme wazi kwamba, Iko namna Mungu anafanya juu yetu

Takwimu hizi za Katoliki, ni kubwa Sana, lkni kwamba ni kubwa ukilinganisha na za wapi,

Hili janga, achilia mbali takwimu hizi, Mimi bado naona hatujafikia mahali ambapo wenzetu walikuwa na wamefikia, kwamba ndani ya masaa 24 zaidi ya watu Elfu tatu, lkn hapa tunazunguzia wasitani wa kila siku pengine ni watu watatu Hadi watano, kama tu takwimu ya Kanisa ambalo linabeba theruthi ya watu wote linapoteza mtu mmoja mmoja per day!!

Maana yake ni mhimu kusema Mungu wetu anafanya kitu juu ya maombi yetu ingawa ni kweli tumepoteza Watanzania wenzetu, ndugu zetu n.k lakini hatuwezi kuacha kuusema wema wa Mungu kwetu, na tuna muda mfupi ujao tuagane na Corona kabisa

Kwa Mungu liko tumaini

Acheni kudanganya watu ambao hawawezi kukokotoa uhalisia tokea katika takwimu zilizopo wakioanisha na kinachitokea mitaani?

Ni nia yenu kuyasubiria ya kina Melinda na Bill Gates ndipo sasa hatua zianze kuchukuliwa au hadi pale ule Mbuyu utakapoguswa?

Ikumbukwe kuwa kuambiwa ukweli siyo kutishwa.
 
Nimemshamgaa sana huyu jamaa,nilitaka nimtajie watu waliokufa bila kuwa na vitambi,Ila nilipoona jina lake japo juu,HUNIJUI SIKUJUI,nkaamua kupiga kimya.

Ujinga ni mzigo nao kama ilivyo kwa kuni hutwikwa kichwani.
 
Shida wakichelewa kuleta chanjo,wakaacha maambukizo yakawa mengi,basi hiyo chanjo itaangamiza watu wengi,maana mwenye maambukizi huwezi kumchanja tena,chanjo itamuua kwa kuwa chanjo itaa activate ugonjwa zaidi.
 
Wewe ni mwongo! Huko mitaani hauishi pekee yako!! Hali si tete kama unavyodai. Tena halo ya mwaka huu ni nzuri sana ukilinganisha na mwaka jana!! Umelenga kuleta hofu na taharuki zisizo na sababu!! Umeshindwa kwa jina la Yesu!!
Waambie waliokutuma kuwa tumegonga mwamba!
 
Wamekuwa wapole. Ni wazi kuwa si nyungu, maombi wala zile juice za NIMRI zinazohitajika bali kuchukua hatua stahiki na chanjo haviepukiki tena.

Tusipoamka mbona tunasererekea kwenye yale ya kina Melinda na Bill Gates?
Naona labda kina Melinda na mumewe waliongea yale kwasababu wameona mbele kuliko sisi kwa reflection wanayoipata kutoka kwa viongozi makaidi kama....... I reserve other words
 
Naona labda kina Melinda na mumewe waliongea yale kwasababu wameona mbele kuliko sisi kwa reflection wanayoipata kutoka kwa viongozi makaidi kama....... I reserve other words
Kwa maneno ya wale na kwa Tanzania ilitakiwa ata 70% ya wakazi wa Dar es Salaam tuwe tumeshafariki.
 
Raisi watu mpendwa aache kuchukua ushauri wa mtu hatari kama Msukuma Nchi yetu ina vichwa vilivyosomea maswala ya pandemics
Uwezo wa Msukuma unaishia kwenye kuoga dawa na kuchanjwa chale.
 
Màneno yapi walioysema? Nikiwasema kuwa mna kasoro wanamifunhia

Tanzia: Padri Wilfrid Dinho Wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Afariki Dunia.
 

Tanzia: Padri Wilfrid Dinho Wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Afariki Dunia.
Poleni sana Ndugu jamaa na marafiki
 
Back
Top Bottom