Corona: Misiba mitaani imekuwa mingi mno. Hii siyo kawaida

1. Sio kweli kwamba takwimu za vifo vya Corona zingetolewa watu wasingekufa kwa ugonjwa huo. Marekani na nchi zingine zilizoendelea wanatangaza kila siku na vifo vinaongozeka. Takwimu zinahitajiwa na Wanasayansi kwa ajili ya utafiti na kuchukua hatua zinazopaswa. Kutangaziana vifo hakumsaidii mwananchi wa kawaida, bali kunamuongezea hofu ambayo inapelekea matatizo mengine. Hakuna ushahidi kwamba huko wanakotangaza vifo kila siku, hilo limesaidia wananchi kuongeza umakini katika kujikinga na Corona. Ila kuna ushahidi wa ongezeko la matatizo ya afya ya akili (mental health) na mengineyo yanayoendana na hofu, wasiwasi n.k.

2. Hakuna ushahidi kwamba hadi leo sisi tuna vifo vingi saaaana vinavyotokana na COVID-19, kuliko zinatangaza takwimu za vifo kila siku. Ila kuna ushahidi kwamba bara la Afrika halijaathiriwa sana na Corona kama ilivyo kwa mabara mengine. Hadi sasa vifo vilivyoripotiwa Afrika nzima si zaidi ya 120,000 ukilinganisha na ukilinganisha na karibu vifo 2,600,000 ulimwenguni. Kumbuka sio rahisi kuficha vifo kwa Waafrika kwa sababu kifo ni tukio muhimu la kijamii.

3. Hakuna nchi yoyote Afrika yenye uwezo wa kudhibiti kikamilifu maambukizi ya Corona. Ugonjwa huu ni mafua makali ambayo yanaambukiza kwa urahisi mno, kiasi kwamba hata wale ambao 'hygiene' yao iko vizuri sana bado wanapata maambukizi. Takwimu za maambukizi hapa Afrika sio sahihi, kuna uwezekano zaidi ya asilimia 70 ya watu walishaambukizwa na kupona. Aidha kuna uwezekano nchi nyingi za Afrika zinapika takwimu kwa sababu za kisiasa.

4. Je, tusichukue hatua zozote kujikinga? Hapana! Tuchukue hatua zinazowezekana kama kunawa, kukaa mbali na wengine ikiwezekana, kuvaa barakoa n.k, naamini zinapunguza kwa kiasi. Lakini tusiilaumu sana serikali maana haina uwezo wa kudhibiti maambukizi wala vifo vinavyotokana na COVID-19 hata kama ingependa kufanya hivyo. Kwenye janga hili, Tanzania na Afrika kwa ujumla inapona kwa neema ya Mungu tu. Hatuna uwezo wa kupambana COVID-19 hata kwa asilimia 1 ya ufanisi.
 
Kutisha au kutishwa maana yake nini?

Unatishwa vipi na taarifa za ukweli ewe mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Kwenye red si wajibu wako?

View attachment 1717458

Ukweli haujawahi kutisha. Sana sana ukweli ni mchungu. Ukweli huuma na msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Au nasema uongo ndugu zangu?

Mpaka damu imtoke masikioni ndio atasikia.
Hii mitano tena kazi tunayo.
 
1. Sio kweli kwamba takwimu za vifo vya Corona zingetolewa watu wasingekufa kwa ugonjwa huo. Marekani na nchi zingine zilizoendelea wanatangaza kila siku na vifo vinaongozeka. Takwimu zinahitajiwa na Wanasayansi kwa ajili ya utafiti na kuchukua hatua zinazopaswa. Kutangaziana vifo hakumsaidii mwananchi wa kawaida, bali kunamuongezea hofu ambayo inapelekea matatizo mengine. Hakuna ushahidi kwamba huko wanakotangaza vifo kila siku, hilo limesaidia wananchi kuongeza umakini katika kujikinga na Corona. Ila kuna ushahidi wa ongezeko la matatizo ya afya ya akili (mental health) na mengineyo yanayoendana na hofu, wasiwasi n.k.

2. Hakuna ushahidi kwamba hadi leo sisi tuna vifo vingi saaaana vinavyotokana na COVID-19, kuliko zinatangaza takwimu za vifo kila siku. Ila kuna ushahidi kwamba bara la Afrika halijaathiriwa sana na Corona kama ilivyo kwa mabara mengine. Hadi sasa vifo vilivyoripotiwa Afrika nzima si zaidi ya 120,000 ukilinganisha na ukilinganisha na karibu vifo 2,600,000 ulimwenguni. Kumbuka sio rahisi kuficha vifo kwa Waafrika kwa sababu kifo ni tukio muhimu la kijamii.

3. Hakuna nchi yoyote Afrika yenye uwezo wa kudhibiti kikamilifu maambukizi ya Corona. Ugonjwa huu ni mafua makali ambayo yanaambukiza kwa urahisi mno, kiasi kwamba hata wale ambao 'hygiene' yao iko vizuri sana bado wanapata maambukizi. Takwimu za maambukizi hapa Afrika sio sahihi, kuna uwezekano zaidi ya asilimia 70 ya watu walishaambukizwa na kupona. Aidha kuna uwezekano nchi nyingi za Afrika zinapika takwimu kwa sababu za kisiasa.

4. Je, tusichukue hatua zozote kujikinga? Hapana! Tuchukue hatua zinazowezekana kama kunawa, kukaa mbali na wengine ikiwezekana, kuvaa barakoa n.k, naamini zinapunguza kwa kiasi. Lakini tusiilaumu sana serikali maana haina uwezo wa kudhibiti maambukizi wala vifo vinavyotokana na COVID-19 hata kama ingependa kufanya hivyo. Kwenye janga hili, Tanzania na Afrika kwa ujumla inapona kwa neema ya Mungu tu. Hatuna uwezo wa kupambana COVID-19 hata kwa asilimia 1 ya ufanisi.

Umejichanganya vilivyo kwenye bandiko lako. Haieleweki kwa nini ukweli ulete hofu badala ya kuwa ukweli utaleta umakini zaidi.

1. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa kuwadanganya watu kuwa ugonjwa haupo wakati upo haiwasaidii kujikinga nao. Bali ni wazi kuwa uwepo wa taarifa sahihi kunasaidia watu kuchukua tahadhari zaidi.

2. Ushahidi wa kiwango cha vifo kwetu unataka uupate vipi wakati kwa makusudi taarifa zinafichwa? Wewe hujasikia ugonjwa huu ukibatizwa majina tokea changamoto za kupumua, pneumonia, kujisikia vibaya, mafua, kubana mbavu, ajali nk?

3. Hakuna nchi Afrika yenye uwezo wa kuudhibiti ugonjwa huu? Hii si kweli. Kwenye red kuna husika:

IMG_20210304_213802_073.jpg

4. Hatua tunazochukua ni zile tu tunazo ziweza, una maana ni kama hizi za latra za kukaa mita moja stendi na kushonana kama magunia kwenye madala dala na ma ferry?

IMG_20210214_214251_251.jpg

Kwanini msimamo huu ni muafaka sana kwenu?

IMG_20210218_173848_589.jpg

Si mseme tu kuwa mmetutelekezea janga na mnaukimbia wajibu wenu. Kuwa wenye kufa shauri yetu na wenye kuishi shauri yao?

Kama yamewashinda si mpishe wengine waongoze vita hivi? Kwa nini kutusakizia na kututelekezea vifo vinavyoweza kuepukika?
 
Hapa nipo kwenye msiba wa rafiki yetu baada ya kufariki kwa changamoto ya upumuaji na kesho mida ya saa saba marehemu anatarajiwa kusafirishwakuelekea Mbeya kwa maziko. Nashukuru wahudhuriaji wamechukua tahadhali zote za kujikinga na Corona kwa kuvaa barakoa na kukaa mbalimbali kila sehemu kukiwa na ndoo za maji tiririka.

Mungu aliepushe taifa letu katika hii kadhia ambayo viongozi wetu baada ya kusa wafariji wakuu wamegeuka kuwa wauwaji. Narudia tena kusma kula wamegeuka kula wauaji
alikuwa mtu mzima?
 
Hakuna siku ambayo sijahudhuria mazishi, hali inatisha kwa kweli
 
nadhani korona ipo zaidi huko DSM, mikoani hakuna misiba mingi Kama inavyosemwa
 
Haiwezi kuwa sawa na Dar lakini hata mikoani hali si hali.

Kuliko salama kunasemekana ni mkoa wa Lumumba tu ambako hata hivyo uongo ni mwingi zaidi.
 
Umejichanganya vilivyo kwenye bandiko lako. Haieleweki kwa nini ukweli ulete hofu badala ya kuwa ukweli utaleta umakini zaidi.

1. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa kuwadanganya watu kuwa ugonjwa haupo wakati upo haiwasaidii kujikinga nao. Bali ni wazi kuwa uwepo wa taarifa sahihi kunasaidia watu kuchukua tahadhari zaidi.

2. Ushahidi wa kiwango cha vifo kwetu unataka uupate vipi wakati kwa makusudi taarifa zinafichwa? Wewe hujasikia ugonjwa huu ukibatizwa majina tokea changamoto za kupumua, pneumonia, kujisikia vibaya, mafua, kubana mbavu, ajali nk?

3. Hakuna nchi Afrika yenye uwezo wa kuudhibiti ugonjwa huu? Hii si kweli. Kwenye red kuna husika:

View attachment 1717812

4. Hatua tunazochukua ni zile tu tunazo ziweza, una maana ni kama hizi za latra za kukaa mita moja stendi na kushonana kama magunia kwenye madala dala na ma ferry?

View attachment 1717813

Kwanini msimamo huu ni muafaka sana kwenu?

View attachment 1717815

Si mseme tu kuwa mmetutelekezea janga na mnaukimbia wajibu wenu. Kuwa wenye kufa shauri yetu na wenye kuishi shauri yao?

Kama yamewashinda si mpishe wengine waongoze vita hivi? Kwa nini kutusakizia na kututelekezea vifo vinavyoweza kuepukika?

Nilipoona tu mambo kuibiwa kura, nikajua post nzima ina jicho la kisiasa. Kwa mkao huo huwezi kuona mambo kwa mtazamo tofauti.
 
Umeyaona wapi hayo ya kuibiwa kura wewe mwenye macho ya mwewe?

Au kama kawaida yenu:

IMG_20210218_174254_207.jpg

Ulifika ukiwa umejiandaa kutuaminisha kuna siasa siyo misiba.

Looh!

Kwa hakika mko vizuri.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Alafu kuna takataka linajiita Dokta Abasi limevimbiwa cheo linasema watu wasitoe takwimu wala kusema lolote juu ya Corona lenyewe tu ndio limeambiwa na Mungu liseme kuhusu ugonjwa, ovyo kabisa yaani kipindi hiki watanzania wana tabu sana. Narrow minded plus local believer leadership yaani ni kuomba Mungu Sana bila hivyo hatuchomoki.Mimi huku ulaya sitoki hata kama tunaitwa nyani angalau kuna watu wanajielewa kwenye baadhi ya mambo.
 
Tuchukue Tahadhari!

Mapadri, watawa, kina Maalim, madaktari bingwa kadhaa, nk. Wote wameshindwa kuchukua tahadhari?

IMG_20210214_214251_251.jpg

Hapa kwenye red bila utayari wa serikali tunapenya vipi?

IMG_20210304_213802_073.jpg

Mchawi wetu yuko humo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Siku hizi unachagua uende msiba upi...kule wanazika pale wanaosafirisha...
 
Jah awe nasi ktk kipindi hiki kigumu. Atuvushe salama.
 
Mapadri, watawa, kina Maalim, madaktari bingwa kadhaa, nk. Wote wameshindwa kuchukua tahadhari?

View attachment 1717837

Hapa kwenye red bila utayari wa serikali tunapenya vipi?

View attachment 1717838

Mchawi wetu yuko humo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Sasa unangojea nini kujikinga? Huu ugonjwa ulo kila mamhali. Chukua tahadhari. Sasa inmlalamikia nani? Magufuli ndiy aliyeleta huu ugonjwa?
 
Kwa kweri hata tetemeko la Kagera hakuleta. Hapo kwenye red ulipata nafasi ya kupaona maishani mwako?

IMG_20210304_213802_073.jpg
IMG_20210304_213802_073.jpg

Hii nayo ulipata kuiona au kubwa bwaja kama bata tu jombi?

IMG_20210214_214251_251.jpg

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom