CORONA: RC Makonda atoa mwongozo kwa wananchi wa mkoa Dar es Salaam na wageni

CORONA: RC Makonda atoa mwongozo kwa wananchi wa mkoa Dar es Salaam na wageni

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa DSM ametoa mwongozo rasmi wa kudhibiti uwezekano wa virusi vya Corona kuingia mkoani Dsm.

Mambo muhimu ni pamoja na vyombo vya usafiri kutojaza abiria kupita uwezi wake kisheria.

Vyombo vya kunawia kuwekwa katika stendi zote na majumbani

Kuepuka kusalimiana kwa mikono na kukumbatiana.

Pawapo na umbali wa futi 6 kati ya mtu na mtu wakati wa maongezi

Mh Makonda atafanya ukaguzi maalumu baada ya siku tatu kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake

NB: Nitaweka tangazo la RC Makonda hapa.
 
Nimemsikia Mkulu anaongea Jana badala ya kuwa serious yeye analeta utani. Wakati nchi kama Kenya, Namibia na RSA Marais wao wamehutubia mataifa yao na Koa miongozo kwetu inabidi tumsikilize Makonda. Tena hana jipya zaidi ya Yale tunayoyajua ya WASH.
 
Upuuzi mtupu ugonjwa hauwez kuzuia kijinga eti kwa kuweka vifaa vya kunawia wakati hata kwa hewa tu unasambaa imagene wanaopanda daladala mbagala kkoo duh tuombe Mungu tu na kudhibiti mipaka hatuwez kupambana na huu ugonjwa ukiingia.
 
Mbona hajaweka kuvaa mask, si inaambukizwa kwa njia ya hewa pia?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapana mkuu. Haiambukizwi kwa njoa ya hewa. Ujinga (kukosa maarifa) katika jambo hilo ni mkibwa sana. Sijui unafikiri mask inazuia hewa? Huyo alovaa anapumuaje sasa??

Vidudu vya corona vilo katika mate na kamasi. Ndio maana contact na vitu hivo inaambukiza
 
futi 6 kwenye maongezi ya mtu na mtu…🤣🤣🤣🤣🤣
Kuna muvi inaotwa Five feet apart, Romantic Drama..Inahusu teeneger wawili walikua na ugonjwa fulani ambao ulikua ni virusi.

So hao wenye ugonjwa huo hawakutakiwa kusogeleana zaidi ya urefu wa futi 5. Bahati mbaya wagonjwa hao wawili wakapendana sana sana walikua wanatembea wameshika mti wa fagio. Imagine mtu unampenda sana ila hutuhusiwi kumsogelea..Walikua wanaishi Hospital.

Mwisho kabisa Me alikufa, Maana yule girl alizama kwenye barafu wakiwa kwenye matembezi usiku so ikabidi amsogelee kwenda kumvuta
 
Hivi vijidudu vitaanza kuangusha serikali za nchi na kuleta mapinduzi ya kijeshi hasa nchi ambazo tayari hazikuwa politically stable, mark my words.
 
Tatizo ni pale wanapoongea sanaaaa...

Serikali inabidi ianze kufanya baadhi ya jitihada ikiwemo kuanza kusafisha vyombo na magari ya usafiri wa umma kwa kemikali maalumu...

Kuzuia ndege na meli zinazotoka maeneo/nchi fulani...

Waweke vituo vya upimaji vya hiyari ikiwepo na maeneo tengefu kwa wataobainika kuwa na maambukizi,badala ya kusubiri hadi isemekane mtu au watu fulani wanashukiwa kuwa na maambukizi...

Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dar na mingine yoyote ya mipakani inapaswa iwekwe chini ya programu ya ukaguzi wa hali ya juu pengine ikilihusisha jeshi ili ku screen kila mtu anayeingia...

Naamini mikoa ya mwanzo kupata maambukizi itakuwa ni hiyo niliyotaja, haswa Arusha na Kilimanjaro...
 
Back
Top Bottom