CORONA: RC Makonda atoa mwongozo kwa wananchi wa mkoa Dar es Salaam na wageni

CORONA: RC Makonda atoa mwongozo kwa wananchi wa mkoa Dar es Salaam na wageni

Mkuu wa mkoa wa DSM ametoa mwongozo rasmi wa kudhibiti uwezekano wa virusi vya Corona kuingia mkoani Dsm.

Mambo muhimu ni pamoja na vyombo vya usafiri kutojaza abiria kupita uwezi wake kisheria.

Vyombo vya kunawia kuwekwa katika stendi zote na majumbani

Kuepuka kusalimiana kwa mikono na kukumbatiana.

Pawapo na umbali wa futi 6 kati ya mtu na mtu wakati wa maongezi

Mh Makonda atafanya ukaguzi maalumu baada ya siku tatu kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake

NB: Nitaweka tangazo la RC Makonda hapa.

Tuwekee tangazo la Mkuu wa Mkoa
 
Labda serikali yetu imefanya utafiti kuwa Tanzania hatuwezi kuathirika sana na gonjwa hilo kwa kutumia wataalamu wake wabobevu kina daktari kingwangala
 
Labda serikali yetu imefanya utafiti kuwa Tanzania hatuwezi kuathirika sana na gonjwa hilo kwa kutumia wataalamu wake wabobevu kina daktari kingwangala
Kigwangalla hajawahi kupractice udaktari bwashee!
 
“Wamiliki wote wa Mabasi makubwa na madogo ya kubeba abiria yanayoingia, kutoka na yaliyopo DSM, Boti za mwendokasi,Treni/TAZARA, Uongozi wa Standi ya Mabasi Ubungo n.k, nawasihi waweke sehemu za kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na kwa sabuni ili kujikinga na corona”- Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda @baba_keagan

“Katika kujikinga na virusi vya corona nawaomba abiria wote kabla ya kupanda na wakati wa kushuka katika vyombo vya usafiri, wasafishe mikono yao kwa dawa maalaum ya kutakasia mikono (Alcohol based Hand Rub Sanitizer)” - RC MAKONDA

“Kila taasisi ihakikishe uwepo wa dawa ya kutakasia mikono (Alcohol based Hand Rub Sanitizer), utekelezaji ukamilike kwa 100% ndani ya siku tatu kuanzia March 16, vyombo vya usafiri viepuke kujaza abiria zaidi ya uwezo (msongamano wa abiria ktk vyombo hivyo ni marufuku)”- RC MAKONDA

“Naelekeza uwepo wa ndoo za kunawia mikono zenye maji yanayotiririka na uwepo wa dawa za Kutakasia mikono kwenye hoteli, gesti, kumbi za starehe, Benki zote, ATMs, Bar, Clubs’, SuperMarkets/Malls, maduka, maeneo ya Ibada, Taasisi na Kaya zote n.k, ili kujikinga na corona”- RC MAKONDA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... mbona hajataja mwendokasi? Ni kwa bahati mbaya au makusudi? Najaribu kuwaza kituo kama Kimara sijui utaratibu wa kunawa utakuwaje mida ile ya asubuhi!
 
Malengo ni mazuri. Je, watekelezaji (wakiwemo watumiaji - raia ) watazingatia usafi kweli?
 
Malengo ni mazuri. Je, watekelezaji (wakiwemo watumishi - raia ) watazingatia usafi kweli?
Hilo ndio la kulitazama,inabidi kila raia awetayari kujihadhari kisha ndiyo hizo juhudi zitakuwa na maana.

Mi naamini kuna raia wengi ambao bado mitazamo yao ni kama huo ugonjwa ni wahukohuko tu,hivyo hawaoni umuhimu wa kuchukua tahadhari
 
Makonda sijawahi kumkubali kutokana na matamko yake yasiyo tekelezeka najua hata hayo hayatotekelezwa
 
Hilo ndio la kulitazama,inabidi kila raia awetayari kujihadhari kisha ndiyo hizo juhudi zitakuwa na maana.

Mi naamini kuna raia wengi ambao bado mitazamo yao ni kama huo ugonjwa ni wahukohuko tu,hivyo hawaoni umuhimu wa kuchukua tahadhari
Unaweza kumlazimisha ng'ombe kwenda mtoni, lakini hauwezi kumlazimisha kunywa maji.
 
Huyu jamaa huwa nadharau Sana matamko yake, sijawahi kumuamini
 
Tatizo kubwa ni mwendo kasi na dala dala, unasema watu wakae mita sita wakiwa wanongea wakati kwenye mwendokasi ni kita sifuri inaingia akilini kweli?
 
Back
Top Bottom