Tatizo ni pale wanapoongea sanaaaa...
Serikali inabidi ianze kufanya baadhi ya jitihada ikiwemo kuanza kusafisha vyombo na magari ya usafiri wa umma kwa kemikali maalumu...
Kuzuia ndege na meli zinazotoka maeneo/nchi fulani...
Waweke vituo vya upimaji vya hiyari ikiwepo na maeneo tengefu kwa wataobainika kuwa na maambukizi,badala ya kusubiri hadi isemekane mtu au watu fulani wanashukiwa kuwa na maambukizi...
Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dar na mingine yoyote ya mipakani inapaswa iwekwe chini ya programu ya ukaguzi wa hali ya juu pengine ikilihusisha jeshi ili ku screen kila mtu anayeingia...
Naamini mikoa ya mwanzo kupata maambukizi itakuwa ni hiyo niliyotaja, haswa Arusha na Kilimanjaro...