Afrika kila kitu kilichelewa .
Utumwa
Ukoloni
Uhuru
Haki za Binadamu
Demokrasia
Utawala Bora.
Maendeleo
Sasa Korona imechelewa kuingia Afrika kwa nia njema kabisa na kwa msaada wa Mungu.
Yote ni ili tujifunze kwa wenzetu ili tusifanye makosa lakini tunafanya makosa Yale Yale mabaya kuliko waliotangulia.
Tumuombe Mungu atupe majawabu kwa Ugonjwa huu na pia tuchukue Tahadhari.
Mabasi yanajazana watu bila kuvaa maski watu wanapigiana Chafya na kukohoa kwenye mabasi.
Stand zinafurika watu bila kuvaa maski.
Eti watu wasivae mpaka waugue na wakivaa wazitoe kila baada ya masaa manne.
Sasa unajiuliza kama wanaona kuna sababu ya kuibadili inakuaje kwa ambaye hajavaa kabisa ?
Wanataka kumfurahisha nani?
Au ni ili watu wasihisi gharama ya maski. Kwa nini watu wasikate vipande vya mashati na khanga wakafunika midomo na pua zao ili wasipigiane Chafya?
Au hata wavae hijabu za kininja ? Lengo ni kupunguza maambukizi endapo yatakuja kwa wakati usiojulikana .
Afrika tubadilike kwa kujifunza kwa wenzetu. Kila kitu kimechelewa kwetu lakini hatujifunzi zaidi ya kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa faida ya madaraka.
Sent using
Jamii Forums mobile app