Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Wakuu huyu waziri yuko serious kweli anasema mgonjwa anaendelea vizuri.. Kwamba wana dawa za kutuliza corona

Kumbe kwetu hatuna utaratibu wa kuwatenga wasafiri ndani ya siku kumi na nne kisha kuwaacha baada ya kujidhihirisha hawana dalili za ugonjwa

Ila bado tuna nafasi ya kupambana Hata kama tumelose ...serikali itilie mkazo kwenye vifaa tiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu tusihamishe magoli hapa, kuna watu wanapaswa wawajibike, huyo mgonjwa aliingia na hakuwekwa karantini, kama angekaa karantini tusingekuwa tunamzungumzia leo. Watu wanafanya kazi kwa mazoea, uongozi wa airport uwajibike, waziri wa afya awajibike.
Wote hao jiwe ndie anaewapa maelekezo, inaitwa one man show, so anaetakiwa kuwajibika zaidi ni mr jiwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well said,maana kuna watu hapa wanakuwa kama wamepata sababu ya kuilaumu serkali,wakati serikali iko kuhakikisha nchi inakuwa salama,tuwe watulivu,huku tukisubiria tamko la serikali ni jinsi gani tuendelee kuchuka tahadhari badala ya kutoa lawama...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana atuokoe na hili zahama, maana kwa utayari wetu kukabiliana na huu ugonjwa ni wa mashaka

Kila mtu achukue tahadhari
 
Lakn na huyo Marekani si ashapata wagonjwa??

NB sikupingi point yako

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Mpumbavu weye nawe unatoa wasaa!
Maajabu
 
Yametimia sasa

Hii nji kwa Usanii imeshindikana...!
Walikuwa wanakataa hakuna mgonjwa nji iko salama na Bado hawataki kutaja majina ya Hospitality zilotengwa kwa Wagonjwa wa Corona...!!
Mficha MARADHI MUSIBA utamwumbua tu.....!
 
Lakini kama haujafa utaona tu.

Bado zikafahamika mkuu nipo kwenye tusubiria zamu yangu. Wenye dhamana tulijaribu kuwaambia wakawa busy segerea.

Sisi kama sisi tungefanya nini, ya rabhi siye na wanetu mashuleni.

Mliombwa tuweke siasa pembeni. Mkaombwa hata msitishe miradi ya ma SGR na stigglers gorge. Mkaombwa muahirishe kodi. Msitishe misongamano, msimamishe ndege toka marais athirika. Nini nifanye?

Ukweli ni kuwa mmeweka maisha ya watu rehani.
 
Wakulaumiwa lazima awepo , haiyumkiniki nchi kubwa zenye maendeleo makubwa wajikinge na corona alafu sisi tusubirie kama tunatolewa kafara. Mungu atusaidie tu kwa maana sijaona nchi yenye masihara na mapuuza kama hapa tz.
Kwann mipaka haikufungwa, huu utalii unamaana gani zaidi ya maisha ya watanzania.

AISEE !!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja ya comment bora kabisa, tulichopanda ndo tumevuna. Wenzetu uwanja wa ndege watu wanawekwa sehemu maalumu kwa wiki mbili then ndo waruhusiwe waondoke.

Sisi kwetu walaaa, tunaona nchi za wenzetu ni kama wehu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…