Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Wakuu huyu waziri yuko serious kweli anasema mgonjwa anaendelea vizuri.. Kwamba wana dawa za kutuliza corona

Kumbe kwetu hatuna utaratibu wa kuwatenga wasafiri ndani ya siku kumi na nne kisha kuwaacha baada ya kujidhihirisha hawana dalili za ugonjwa

Ila bado tuna nafasi ya kupambana Hata kama tumelose ...serikali itilie mkazo kwenye vifaa tiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu tusihamishe magoli hapa, kuna watu wanapaswa wawajibike, huyo mgonjwa aliingia na hakuwekwa karantini, kama angekaa karantini tusingekuwa tunamzungumzia leo. Watu wanafanya kazi kwa mazoea, uongozi wa airport uwajibike, waziri wa afya awajibike.
Wote hao jiwe ndie anaewapa maelekezo, inaitwa one man show, so anaetakiwa kuwajibika zaidi ni mr jiwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ndio mgeni CORONA keshaingia Tanzania.Lakini nafikiri hatutakiwi kupanic.Maana HAMAKI ni mbaya kuliko ugonjwa wenyewe.Tuendelee kujikinga huku tukiomba hili nalo lipite.Mbona hata EBOLA ilitingisha lakini nayo ilipita.
Mungu ibariki Dunia
Mungu ibariki Africa
Mungu ibariki Tanzania.
Well said,maana kuna watu hapa wanakuwa kama wamepata sababu ya kuilaumu serkali,wakati serikali iko kuhakikisha nchi inakuwa salama,tuwe watulivu,huku tukisubiria tamko la serikali ni jinsi gani tuendelee kuchuka tahadhari badala ya kutoa lawama...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana atuokoe na hili zahama, maana kwa utayari wetu kukabiliana na huu ugonjwa ni wa mashaka

Kila mtu achukue tahadhari
 
Hatari.

Wakati wengine wanazuia watu kuingia nchini kwao nchi kubwa kama Marekani sisi tukajidai eti tuna vipimo uwanja wa ndege, marekeni wao hawana vipimo uwanja wa ndege? Marekani alizuia watu kutoka ulaya kuingia kwake sisi tukajifanya tuko vizuri kuliko Marekani.

Ccm hawana malengo mazuri na afya za watanzania. Sasa subiri tuipate fresh.

Wenzetu kila anaeingia toka nje ya nchi huwekwa karantini siku 14 hadi hali iwe sawa, sisi watu wanaibuka wakipimwa airport hakuna dalili wanaondoka kwenda makwao. Ni cases ngapi zimetokea kama za jana? Maana bado watu wako kwenye window period. Ulaya ni risk area watu wanatoka huko tunawaacha tu bila kuwaweka kwenye karantini.

Tulichokua tunakitafta tumekipata
Lakn na huyo Marekani si ashapata wagonjwa??

NB sikupingi point yako

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Kupitia hili tangazo na comments za wanajf, nimegundua kati ya forums zote duniani,hii ni forum ambayo imejaa watu wanapenda kuchukulia mambo kisiasa zaidi.Mbaya zaidi kuna kikundi cha watu wapumbavu na hayawani wanaodhani Covid-19, ipo kwaajili ya kuwakomboa wao,na kutimiza matakwa yao ya kisiasa.Watu wa aina hiyo wanaofurahia utawapata Jf tu, na sio kwenye platform nyingine za kijamii.Narudia tena Huo ni upumbavu na upunga wa hali ya juu.Na kama haya madudu mnayo yaandika humu, ndo yale yaliojaa mioyoni mwenu,Anapokaa sizonje mtapasikia tu.
Mpumbavu weye nawe unatoa wasaa!
Maajabu
 
Yametimia sasa

Hii nji kwa Usanii imeshindikana...!
Walikuwa wanakataa hakuna mgonjwa nji iko salama na Bado hawataki kutaja majina ya Hospitality zilotengwa kwa Wagonjwa wa Corona...!!
Mficha MARADHI MUSIBA utamwumbua tu.....!
 
Lakini kama haujafa utaona tu.

Bado zikafahamika mkuu nipo kwenye tusubiria zamu yangu. Wenye dhamana tulijaribu kuwaambia wakawa busy segerea.

Sisi kama sisi tungefanya nini, ya rabhi siye na wanetu mashuleni.

Mliombwa tuweke siasa pembeni. Mkaombwa hata msitishe miradi ya ma SGR na stigglers gorge. Mkaombwa muahirishe kodi. Msitishe misongamano, msimamishe ndege toka marais athirika. Nini nifanye?

Ukweli ni kuwa mmeweka maisha ya watu rehani.
 
Wakulaumiwa lazima awepo , haiyumkiniki nchi kubwa zenye maendeleo makubwa wajikinge na corona alafu sisi tusubirie kama tunatolewa kafara. Mungu atusaidie tu kwa maana sijaona nchi yenye masihara na mapuuza kama hapa tz.
Kwann mipaka haikufungwa, huu utalii unamaana gani zaidi ya maisha ya watanzania.

AISEE !!
Suala hili la COVID-19, halina mtu wa kulaumiwa.
Hasira na woga, hazitafanya lolote lile kwenye hili tuepuke.

Huu virusi hivi vinaambukiza bila hata dalili yoyote kwa muathirika. As a matter of fact, kama una afya njema unaweza ukaambukiza wengine bila kujua mwenyewe kama ulikuwa nao.

Airport za mataifa yote duniani zinapima dalili tu kwanza, ndio maana wanashauri watu wanaojihisi kuumwa baadae, waji-isolate. Upimaji wa virusi wenyewe hufanyika katika maabara chache zilizotayarishwa. Hivyo wanadhaniwa peke yake ndio hupimwa. And this is world wide; due to unlimited resources. Kuna nchi kama S.Korea wamejitahidi kidogo kwenye upimaji, containment haijawezekana.

Kwa lugha nyepesi, haiwezekani kuzuia ugonjwa huu kuingia katika nchi yoyote ile unless mmejifungia na mmesimamisha shughuli zoote; which is realistically impractical.

Yaani, kinachofanyika na nchi zote duniani ni kufupisha uharaka wa maambukizi; ili huduma za kiafya zisizidiwe.
Maana hata nchi zenye huduma za kiwango cha juu, hazina uwezo wa kuhudumia mlipuko wa uambukizaji wa haraka namna hii.
Ndio maana hakuna nchi tajiri iliyoweza kuukwepa ugonjwa huu.

Acha niuseme ukweli:
People will die.
Most will survive.

Hatukuwa tayari (kidunia) ku-face epidemic(now pandemic) ya namna hii.

Pray, kwa sababu there will be tears.


Sent using LF Electromagnetic Waves

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ummy anajipa moyo ati ni imported case. Kwani ugonjwa ungefika vipi bila ya kutoka nje ya nchi.

Maonyo yote hawakuyasikia sasa majuto ni mjukuu.

Ati sasa wakawatafute waliokutana na mgonjwa. Si hao tu hata na waliokutana na waliokutana na waliokutana na... ... waliokutana na mgonjwa. Hiyo chain ndiyo inawapa taabu ulaya.

Acha tuone sasa sote yetu macho.
Moja ya comment bora kabisa, tulichopanda ndo tumevuna. Wenzetu uwanja wa ndege watu wanawekwa sehemu maalumu kwa wiki mbili then ndo waruhusiwe waondoke.

Sisi kwetu walaaa, tunaona nchi za wenzetu ni kama wehu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom