Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Kumbe watu mko waoga eeh [emoji1787]

Majuzi hapa kuna watu walikuwa wanajidai eti corona ni mafua tu.

Sasa hivi washaanza kujiharishia baada ya kusikia kirusi kishatia timu.

Kwanza si ajabu kilikuwepo muda wote tu ila watu hawajui.
Ni kweli mkuu kumbuka tupo dunia ya tatu huku
Mambo mazito yanatushinda hili la covid 19 si lakuja na marungu na magari ya kuwasha
Ni mtihani huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania yathibitisha kuwa na kisa kimoja cha virusi vya corona
  • 16 Machi 2020
Sambaza habari hii Email Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter

Tanzania imethibitisha kisa kimoja cha virusi vya corona.
Mnamo tarehe Machi,15, msafiri huyo aliiingia Tanzania majira ya saa kumi jioni.
Mgonjwa aliyetangazwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, ambaye aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la Rwanda.
Msafiri huyo aliondoka nchini tarehe 3,Machi 2020 ambapo kati ya tarehe 5-13 Machi alitembelea nchi za Sweden na Denmark na kurudi tena Ubelgiji.
Msafiri huyo alipita uwanja wa ndege wa KIA.
Waziri Ummy Mwalimu amesema msafiri huyo alipofika KIA alifanyiwa ukaguzi na maafisa wa afya na kuonekana kutokuwa na homa.
Baadae alianza kujisikia vibaya akiwa hotelini na kwenda hospitali ya mkoa ya rufaa ya Mount Meru Arusha.
Taarifa zaidi kukujia...
 
KAMA ILIVOKUWA KWA IRAQ PIA LIBYA WALISHINDWA KUWASHIKISHA ADABU SAADAM NA GADAFI NASI TUMESHINDWA KUHISHIKISHA ADABU CCM NA MATENDO YAO MAOVU SASA ANATUSHIKISHA ADABU WOTE, ASANTENI CCM
 
Cc Pascal Mayalla
Kwenye uzi wako ule asubuhi nakumbuka niliandika huenda wish ya technically ikawa granted. Here we are.
Uzembe umesababisha haya yote.
Unajiuliza kwa nini mipaka haikufungwa toka mwanzo??
Halafu mtu anakuja kukurupuka na kusema mbio za mwenge kapiga marufuku.

Tahadhari kubwa kuliko zote ilikuwa ni kufunga mipaka.
Tufunge mipaka yetu haraka

Pia ni vyema kuwaweka karantini na kuwapima watu wote waliokutana na mgonjwa.
Waanze na wafanyakazi wa viwanja vya ndege, hoteli aliyofikia nk
 
Badaya ya kufunga viwanja vya ndege,bado sijui wanasubiri nini kitokee.
 
Corona ilishaingia Tanzania ilikuwa swala la muda tu kutangaza sisi sio Kisiwa.

Hizi nchi za kijamaa zina Siri sana, Mungu atunusuru isisambae zaidi.
Tanzania sio nchi ya kijamaa. Tutapona huu ugonjwa kama tutakuwa wazi, open government yaani. Tukificha ficha data, ati kulinda utalii,tutakoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…