Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Km unaweza kupimwa na isionekane wangapi wanayo lkn haikuonekana wakat wanaingia nchini?

Hii hatar sana...
 
Hapa dawa yake ni kufunga mipaka
Yote,
Tanzania imethibitisha kisa kimoja cha virusi vya corona. Mgonjwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda Air.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy Mwalimu, Mwanamke huyo alitoka Ubelgiji na alikuwa anaishi kwenye nyumba ambapo kuna mwanaume alipata virusi vya corona, baadae aliamua kurudi nchini na alipopimwa uwanja wa KIA alionekana mzima hana maambukizi kisha akaamua kujitenga na kujiweka karantini yeye mwenyewe na kukaa hotelini.

Baadae mwanamke huyo alianza kujisikia vibaya na kuamua kwenda hospitali ambapo alipopimwa akathibitika kuwa na virusi vya Corona.



View attachment 1389929

View attachment 1389983



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tamko la Mboye limewatoa pangoni mikutano ya kisiasa kushinei
unamaanisha mbowe na chadema yake serikali na ccm wanamuogopa maana nusu saa mbowe kawaambia wanachama wake watafanya mikutano kwa lazima nusu saa tena baadae ummy anatoa tahadhari coona imeshaingia tanzania
 
Kumbe watu mko waoga eeh 🤣

Majuzi hapa kuna watu walikuwa wanajidai eti corona ni mafua tu.

Sasa hivi washaanza kujiharishia baada ya kusikia kirusi kishatia timu.

Kwanza si ajabu kilikuwepo muda wote tu ila watu hawajui.
Watu wanashangaza sana, walikuwa wanasema humu, mara mtu mweusi kuogopa mafua ni uzembe.

Sasa kimetangazwa watu wamepanic kama wote.


Beggars can't be choosers
 
Waziri wa afya Ummy mwalimu kupitia waandishi wa habari muda huu amethibitisha kutokea kwa kisa kimoja cha mgonjwa wa corona,mgonjwa huyo ni raia wa Tanzania amegundulika kuwa na corona baada ya kuwasili akitokea ubelgiji kwa ndege ya Rwandan air,:source Azam media

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya mbowe kutangaza atafanya mikutano ndio mnatangaza Kuna mgonjwa wa korona?
 
Sasa si tutengane mikoa hii? wa Arsuha arusha, hakuna kutoka, au mpaka wasambaze, ila ni too late, wapuzi hawa walishaambiwa wazuie ndege kuja nchini hawasikii.
Ona sasa kishanuka.
 
Hii story ya ummy imekaa kiuongo uongo kabisa.
Kwanza why vipimo vya airport visisome na mtu amejihisi kabisa
Halafu after few hours hospital nyingine ndo ione tatizo lake
So inamaana kuna ambao hvy vipimo vya airport viliwaacha wapite na ni wagonjwa??? Ina maana hhvy vipimo ni magumashii??
Hii habari ni ya uongo 100% ni tangazo la kisiasa. Ukitaka kujua hilo subiri ifike mkutano wa mbowe watasema hakuna kukusanyika kisa korona. But makanisani watu wataenda misikitini wataenda na mzee baba atawakusanya atawahutubia....hapo ndo mtajua kuwa hii ni kamba km ya dokta shika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom