Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

yote umeandika poa, ila umeharibu ulipoingiza mambo ya vyama kwa swala la kiafya kama hili, usiweke siasa kwenye uzi mzuri kama huu uliouanzisha, ili tuchangie kuhusu hatima yetu inakuwaje kiafya...
Hii serikali imezembea hapa tukubali.kwanza bado foreigners wanaingia ,pili hawawekwi karantini ni wanapita Kama mama juma kafungulia kuku asubuhi. Sasa tutapona kwa mpango huu? Serikali wako busy kuhakikisha Chadema haifanyi mkutano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu waziri wa afya ni MD au ana level nyingine ya juu??
Ni lawyer, walau angekuwa na ka MD, asingezingua hivi. Ninakumbuka maneno ya Prof mmoja Muhas Enzi hizo, aliyekuwa anawashauri Madaktar kujiingiza kwenye siasa. Hii ingesaidia kuondokana na watu wasiojua medicine kuongoza wizara ya afya. Madudu kama haya yangepungua.
 
Ameandika bwana Kitale: Corona sasa imekosea niia. Imeingia kwenye nchi ambayo kila mtu ni mtaalamu wa afya.

Nikiwa nimefungiwa hapa Deutschland. Basi Niko very social kwa majungu ya watanzania wenzangu wenye sifa ya kuwa na maneno mengi na best ideas bila kufanya kazi.

Nimefurahi sana kusoma ukweli huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote mmesikia taarifa ya leo ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Ukiacha nyuzi zingine zinazohoji mambo mbalimbali kuhusu taarifa ile kama timing yake nk, kuna maswali ya msingi yanayohitaji majibu kuhusu taarifa yenyewe.

Kwanza, je huyo mgonjwa alishuka KIA peke yake na kama kulikuwa na abiria wengine walioshuka naye, je wameshatafutwa na kufanyiwa vipimo vyovyote?

Pili, huyo anayesemekana ni baba mwenye nyumba aliyesema ana Corona alipofikia huyo mama huko Ubelgiji ni raia wa wapi? Mara ya mwisho kuja Tanzania ni lini?

Ninaamini kama Waziri, majibu ya maswali haya angeweza kuwa nayo katika ile press conference.

Nikijibiwa haya maswali, nitaenda zangu kulala kwa amani.
 
Uandishi wako ni kama una COVID-20
Ameandika bwana Kitale: corona sasa imekosea niia. Imeingia kwenye nchi ambayo kila mtu ni mtaalamu wa afya.

Nikiwa nimefungiwa hapa Deutschland [emoji629]. Basi Niko very social kwa majungu ya watanzania wenzangu wenye sifa ya kuwa na maneno mengi na best ideas bila kufanya kazi.

Nimefurahi sana kusoma Ukweli huu.




Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni heri ukaenda kulala maana inaweza kufika asubuhi na jibu hukuweza kupata boss wangu.
 
Hii story ya Ummy haijakaa sawa. Nakataa kuikubali! Wasije kuwa wamemdaka mke wa mtu kwa sababu zingine halafu wanatuambia habari za corona.

Hii movie nahisi kama nimeshaiona.
 
Huu ni msiba mzito sana sana. Tujiulize airport ina usalama kiasi gani?

Kama airport zinapitisha watu wa Corona Virus vipi huku boda Namanga, Siral nk?

Haya ndio mambo muhimu ya kujiuliza, aliopanda nao kwenye basi to hotel wako wapi?

Je wamesalimika na ugonjwa? Vipi huko majumbani mwao wanapoishi ndugu zao wamesalimika?

Pale ndipo mtasikia tumepoteza 100 kwa siku kama Italy

Lord have mercy on us
 
Back
Top Bottom