Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,206
- 18,549
Kwanza tuombe Mungu hii homa isitufikie.
Pili Ulaya wameshaanza kuzungumzia baadhi ya match kuchezwa bila mashabiki kwa hofu ya kuambukizwa hii homa.
Kwa jinsi ninavyoona kitakuwa kisingizio valid kwa serikali kubakia madarakani na kuchelewesha uchaguzi.
Au uchaguzi utafanyika bila campaign.
Haya yote yatategemea maambukizi yamefikia wapi.
----
Pendekezo: Kutokana na mlipuko wa Corona, uchaguzi mkuu 2020 uahirishwe.
Pili Ulaya wameshaanza kuzungumzia baadhi ya match kuchezwa bila mashabiki kwa hofu ya kuambukizwa hii homa.
Kwa jinsi ninavyoona kitakuwa kisingizio valid kwa serikali kubakia madarakani na kuchelewesha uchaguzi.
Au uchaguzi utafanyika bila campaign.
Haya yote yatategemea maambukizi yamefikia wapi.
----
Pendekezo: Kutokana na mlipuko wa Corona, uchaguzi mkuu 2020 uahirishwe.
Salamu ndugu Watanzania wenzangu, poleni na hekaheka za kujiokoa na balaa hili, afya zetu imara ndio kipaombele chetu namba moja.
Mwaka huu agenda kuu kitaifa ni uchaguzi mkuu, pamoja na mambo mengine, naomba tujikite kwenye hili kwa uzito wake.
Uchaguzi mkuu ni mchakato ambao huchukua muda mrefu hadi kukamilika, kuanzia maandalizi ya awali kabisa [mtu binafsi], na hata kitaasisi kama vyama vya siasa, hadi kufikia kupiga kura Oktoba 25 ambapo ni kilele kwa mwaka huu.
Katika kipindi hiki chote, wahusika [wagombea] huzunguka huku na kule na hutumia namna mbalimbali kujiandaa ikiwemo kutafuta wadhamini au hata wataalamu [waganga] ili kujiweka sawa.
Hii inaweza kuhusisha watu kwa makundi kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na mlipuko wa balaa hili, lakini mgombea kwa maslahi yake binafsi hashindwi kusafiri [hata ikibidi kwa siri] kwenda maeneo hatarishi ilimradi tu kutimiza azma yake.
Hii inaweza kuwa sehemu ya kuwezesha maambukizi na kusambaa kwa ugonjwa huu, hapo bado vikao vya ndani vya chama na baadae mikutano ya hadhara ili kunadi sera [kampeni] ambayo hukusanya watu wengi [mafuriko] kusikiliza na kuchambua sera.
Kwa hali ilivyo sasa nchini na duniani kote, hatuwezi kujua hili janga litakuwa na madhara kiasi gani, hivyo tunawajibika kuchukua kila aina ya tahadhari ili kujilinda na kulinda afya za wengine.
Tunapozuia watu kujumuika na hata kusafiri, hatupaswi kubeza madhara ya uchaguzi, ambao kwa vyovyote vile ni lazima utahusisha ziara na mikusanyiko ya watu.
Kwa hayo machache, pamoja na maoni yenu yenye nia njema na kuboresha hoja hii, napendekeza uchaguzi mkuu uahirishwe hadi hapo hali itapoonekana kutengemaa.
Tulinde AFYA zetu, tuwalinde wenzetu, maendeleo hayana VYAMA.