Uchaguzi 2020 Corona virus: Uchaguzi 2020 kuahirishwa?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Kwanza tuombe Mungu hii homa isitufikie.

Pili Ulaya wameshaanza kuzungumzia baadhi ya match kuchezwa bila mashabiki kwa hofu ya kuambukizwa hii homa.

Kwa jinsi ninavyoona kitakuwa kisingizio valid kwa serikali kubakia madarakani na kuchelewesha uchaguzi.

Au uchaguzi utafanyika bila campaign.

Haya yote yatategemea maambukizi yamefikia wapi.

----
Pendekezo: Kutokana na mlipuko wa Corona, uchaguzi mkuu 2020 uahirishwe.

 
Tutatengeneza app za simu au mfumo kama wa m-pesa, au kuangalia namba yako ya nida watu watavote, kampeni tutachagua vituo viwili vya tv watu watamwaga sera zao hapo.

Kisha kwenye kujumuisha matokeo, upinzani utaita wadukuzi kutoka urusi wafanye kama kwa Trump, huku chama tawala wakijidhatiti na wataalamu kutoka Israel.

Hatimaye mshindi atatangazwa UCHAGUZI LAZIMA
 
Tabutupu,
Haiwezi kuathiri na kikubwa kama hapa kwetu ni jambo la kuomba mungu isije sababu kwakweli ule ugonjwa hauna utani.
 
Corona virus ni tishio kwa ustawi wa binadamu kila sehemu.Kuna uwezekano mkubwa wa kufuta michezo ya Olimpic huko Japan.
 
Ukimwi umekolea sana siku hivi, je umeona watu wamepu gua guesthouse? Uchaguzi ni kama kawaida.
 
Tabutupu,
Mda wote mnawaza Corona tu, nani kakwambia corona inaenea kila mahali, huyo kirusi ni kiumbe kama wewe ili aishi anategemea hali joto, anaenea nchi za baridi kipindi cha baridi kali lkn kwenye maeneo yenye joto hawezi kuishi. Kwa hiyo achana na hayo mawazo yako.
 
Yanini kuitabiria nchi matatizo,mada haina logic hii yafaa kufutiliwa mbali
 
Corona haichagui wala haibagui,inaweza anzia jumba jeupe,tena wakiwa kwenye kikao cha baraza la wakubwa.Wakiugua wote na wakatangulia,uchaguzi hautafanyika?
Iwe kweli basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…