Corona: Wazee na wenye magonjwa mengine tupaze sauti

Corona: Wazee na wenye magonjwa mengine tupaze sauti

Kwani kasema yeye binafsi hajilindi!? Tunataka kuona serikal inawajibika kwa upande wake lkn sio kupiga propaganda majukwaani. Serikal za nchi zingine zinaagiza chanjo kwa sasa, swala la kujua chanjo ni salama au la ni la serikal yenyewe. Kama inashindwa kutambua chanjo ni salama basi haina uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani. Au tuamini yale wasemayo baadhi kuwa serikali haitaki kutoa pesa?
Jiwe hana pesa, anachowaza ni pesa tuuuuuuu, sasa tutaisha na pesa ataikosa ataongoza wafu
 
wewe baki nyumbani kwani unalazimishwa kutembea ukifa asala yako au ya jiwe mbona mnakua na akili ya nyumbu jiwe mnaona alisomeki afu mnaanza kulalamika .STAY HOME.
Ni sauti ya walikuwa na sautj
 
Acha kujitia ujuaji wakati mwenye akili za ng'ombe ni wewe! Hivi katika mazingira haya ng'ombe wewe, walio hatarini wajiepushe vipi?..
Kwa hiyo wwe unataka Nchi yote ipigwe lockdown!? Mi naona hivi, tuendelee hivi hivi,ukitaka vaa Barokowa wwe vaa, na Kama uchumi unakuruhusu pia waweza jipiga lockdown wwe na watu wako unaoweza kuwapa amri Kama Watoto wako!! Mwisho wa siku Maisha lazima yaendelee kwa hali yoyote ile tunaopitia kama Wanadaamu!!
 
Jana tumemzika kigogo wa BOT (Joachim Sayi Nsunga) RIP, huko Dutwa Bariadi, Simiyu. Huyu bwana alikuwa mhasibu mkuu BOT makao makuu, Dodoma.
BOT imehamia Dodoma lini? Makao makuu si yako Dar es salaam? Anakuwaje Mhasibu mkuu Dodoma wakati makao makuu yako Dar es salam ambako ndiko mhasibu mkuu anapaswa kuwapo? Huyo hakuwa kigogo wala mhasibu mkuu

Mleta mada muongo
 
Maisha ni wewe mwenyewe. Hakuna wakukuambia fanya mazoezi au kula hiki au kunywa hivi. Ni wewe tu ujipiganie mwenyewe.

Japo wanaondoka pia wa umri wa kati tena wengi mno wanaondoka.

Jana kanisani nilivaa barakoa pekee yangu, kwani watu wote hawajui kuwa kuna ugonjwa, si wanazarau tu, unataka viongozi wakuambie vaa barakoa, its up to you jitunze my friend.

Viongozi wa kanisa wanakazia kuwa DAMU YA BWANA YESU YATOSHA, ila Neno linasema WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.

Jilinde, elewa ulikuja duniani mwenyewe na utaondoka mwenyewe.
 
wewe baki nyumbani kwani unalazimishwa kutembea ukifa asala yako au ya jiwe mbona mnakua na akili ya nyumbu jiwe mnaona alisomeki afu mnaanza kulalamika .STAY HOME.

Ni mjinga peke yake asiye jua kuwa hata tulio hatarini tunalazimishwa kutobakia nyumbani. Anayekwambia tunatoka kutembea ni nani mburula wewe?

IMG_20210214_214251_251.jpg

Hivi nyumbu nyie msioweza kuona mbele ya pua zenu ni lazima kweli kutoa maoni hata kwa msiyoyajua?

Hata aibu hamna jamani?

What a disgrace?
 
Yaleyale ya “TRUMP” haaa corona ni hoax, ni fake news za chama cha upinzani!!akadharau wana sayansi, akadharau dawa mpaka kasema disinfectant injection ingefaa kutibu korona, mara chloroquine inatibu mpaka watu wakawa wamekufa laki nne wakati anaondoka madarakani!!! Let us face the reality, napongeza wanasayansi ambao angaa wamekuja na NIMRICAF ila wapige hatua zaidi tupate vaccine(chanjo) yetu wenyewe, made in Tanzania!!!

Wamarekani tayari wana chanjo tatu(moderna, Johnsons & Johnsons, Pflizer) UK wanayo moja, Russia wana moja(Putink!!!), China wana moja, Australia wana moja, why not Tanzania wakati tumesoma vyuo walivyosoma hao yaani WaTz wengi wasomi wamesoma Russia, China, Scandinavian Countries, East and West Germany, Canada USA Italy France, Turkey, Japan, let alone vyuo vya Africa(Tanzania included) vipi tunashindwa kutoa vaccine yetu?

Kwa kuunganisha wataalamu wetu coupled with good political will, it can be done let us play our part. After all we have Rais mzalendo, Dr Magufuli.
 
BOT imehamia Dodoma lini? Makao makuu si yako Dar es salaam? Anakuwaje Mhasibu mkuu Dodoma wakati makao makuu yako Dar es salam ambako ndiko mhasibu mkuu anapaswa kuwapo? Huyo hakuwa kigogo wala mhasibu mkuu

Mleta mada muongo

Kwamba kigogo huyu alikuwa ni wa hazina na si BOT hakuondoi uzito wa mada na kuwa eti sasa ndiyo hakufa kwa changamoto za kupumua.

Kwamba kuuzunguka msiba huu kulikuwapo na upotoshaji kama yale ya ajali ya nane nane kuhusiana na wapi marehemu alikuwa akifanya kazi hakutusimamishi sisi kuainisha uhalisia kuwa kuna kigogo wa fedha kwa majina kamili yaliyotolewa, katutoka.

Kigogo wa mahakama kuu Mwanza tunayeelekea kumzika Kagera naye umemsikia? Au naye unataka uzi mahsusi kumhusu?
 
Corona sio poa mpk mzee wangu Hali mbaya tatizo ilo ilo la upumuaji
 
Maisha ni wewe mwenyewe. Hakuna wakukuambia fanya mazoezi au kula hiki au kunywa hivi. Ni wewe tu ujipiganie mwenyewe...

Ninakushukuru sana kwa mchango wako na kujali kwKo. Nipende kukufahamisha kuwa ninayapambania maisha yangu na ya wapendwa wangu kweri kweri (in jpm's words).

Ninalalamika hivi kwani ninaona wazi kuwa pamoja na jitihada zangu binafsi mimi na wapendwa wangu, tunalipa tunasokomezwa kwa makusudi kunako kifo pasipo kuwa na uhalali wowote. Kama hivi:
IMG_20210214_214251_251.jpg

Ninajinasua vipi na wapendwa wangu kwenye hili. Ni wazi kuwa ninaachwa bila njia bali kuukumbatia ushauri kuwa "sasa basi, liwalo na liwe?"

Si heri nife nikipambana na wanaonilazimisha kufa sasa, kuliko kufa sasa kibudu huu nikihangaika kama punda kuwatafutia wao kodi?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kwani kasema yeye binafsi hajilindi!? Tunataka kuona serikal inawajibika kwa upande wake lkn sio kupiga propaganda majukwaani. Serikal za nchi zingine zinaagiza chanjo kwa sasa, swala la kujua chanjo ni salama au la ni la serikal yenyewe. Kama inashindwa kutambua chanjo ni salama basi haina uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani. Au tuamini yale wasemayo baadhi kuwa serikali haitaki kutoa pesa?

Sasa Serikali ndio imeshikilia huo msimamo wake katika hali hiyo tunafanya nini???, tusubiri tu serikali tusitafute njia ya kufanya individually or collectively !? ?----angalia watu leo hawavai barakoa, hawatumii senitizer nk, sasa utailaumu serikali kwa ujinga wa watu tusiojitambua kwamba kuna Corona na tunapaswa kujilinda???

Sisi Watz ni mazwazwa kwani kila siku jamaa na ndugu zetu wanakufa kwa corona (imebadilishwa jina pneumonia) kinachofuatia ni sisi pia.

Badala ya kujadili mbinu za kukabiliana nayo tunajadili kuhusu Serikali isiyosikia !!!, huko ni kupoteza muda.
 
Mkuu hayupo mwenye uelewa aliye kaa kusubiri juhudi za serikali ya jiwe na kudra za mwenyezi Mungu pekee. Hivi sisi ambao haya ya mikusanyiko pia yanatuhusu:

View attachment 1702714

Nayo tunaiepuka je ndani ya mazingira magumu ambayo serikali inatuwekea?

Katika mikusanyiko kama hiyo vaa angalau barakoa ili kujilinda, ukivaa barakoa nani atakukamata???!
 
Mkuu, hii ni vita ya mtu mmoja mmoja japokuwa ni vita ngumu...
Mkuu, kuchukua hatua mtu mmoja mmoja tatizo lake ni kuwa ugonjwa wa kupumua utapanua wigo na utaweka kambi ya kudumu nchini.

Kukiwa na mapambano ya wengi dhidi ya huo ugonjwa, utatokomezwa fasta
 
Mkuu, kuchukua hatua mtu mmoja mmoja tatizo lake ni kuwa ugonjwa wa kupumua utapanua wigo na utaweka kambi ya kudumu nchini.

Kukiwa na mapambano ya wengi dhidi ya huo ugonjwa, utatokomezwa fasta

Hayo mapambano ya wengi bado hayajapata BARAKA kutoka juu!;, je tukae tu?? au tuendelee kuomba hizo baraka hadi lini??--- hiyo ni sawa na kumpigia gitaa beberu.

Shida Watz ni mazwazwa, hatuna hamasa, hatujitambui na tumejaa ujinga na woga, wewe unadhani kama kila mtu mmoja mmoja tukiamua kuvaa barakoa nk, nani atatuzuia??!---- tatizo ni Watz na sio Serikali.
 
Covid 19 ipo na inaua ndugu zetu, achana na siasa uchwara zinazo ndelea, wala usipoteze nguvu zako na muda wako kubishana na mamluki na vibaraka humu ndani. Take care of your ndugu na jamaa na family yako. Hawa walioko madarakani wameamua kuacha watu wafe tu. Kazi yao ya maana ni kukusanya Kodi baasi
 
Kaulize Dutwa kwenye msiba wa kigogo huyu.

Uliza kote nakopita.

Nimepaza sauti dhidi ya gonjwa hili baya kuliko jina lako tangia day 1:

Ulipendelea nipazie wapi ili usikie wewe?
Kwa hiyo ww huvai barakoa, hujitengi na mikusanyiko isiyo ya lazima!!!
kama ni hivyo utakuwa taburalasa
 
Ninakushukuru sana kwa mchango wako na kujali kwKo. Nipende kukufahamisha kuwa ninayapambania maisha yangu na ya wapendwa wangu kweri kweri (in jpm's words).

Ninalalamika hivi kwani ninaona wazi kuwa pamoja na jitihada zangu binafsi mimi na wapendwa wangu, tunalipa tunasokomezwa kwa makusudi kunako kifo pasipo kuwa na uhalali wowote. Kama hivi:

Ninajinasua vipi na wapendwa wangu kwenye hili. Ni wazi kuwa ninaachwa bila njia bali kuukumbatia ushauri kuwa "sasa basi, liwalo na liwe?"

Si heri nife nikipambana na wanaonilazimisha kufa sasa, kuliko kufa sasa kibudu huu nikihangaika kama punda kuwatafutia wao kodi?

Au nasema uongo ndugu zangu?
Mi nakushauri wwe beba wapendwa wako mkaishi huko unakoona Serekali zao zinachukua hatua sahihii kwenye ugonjwa wa Corona,msije mkafa bure alafu mkailaumu Serekali ya Magufuli bure!!
 
Back
Top Bottom