Mkuu inaonekana hunielewi ninachosema, narudia kusema hivi; kuendelea kuilaumu serikali hii inaposhindwa kutekeleza wajibu wake kwa raia walioipa dhamana kuwatumikia ni sawa na kazi bure, serikali iliisha kataa lockdown kipindi karibu dunia yote ikiweka lockdown (japo partial lockdown), kipindi hiki kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza serikali haitaki hata mtu atangaze kwamba Tz kuna Corona ila ipo Pneumonia sembuse kuchukua za kujilinda na Corona??!!---- yaani the "big boss" anasema; Corona hakuna, kama hakuna Corona how can you enforce an order for Corona that claimed doesn't exist??!!.
Ndiyo maana nikasema katika kipindi hichi cha vita ambapo serikali haitaki kutekeleza wajibu wake kila mtu achukue hatua individually kuanzia katika level ya nyumbani hadi nje ya nyumba; hakikisha nyumbani kwako watoto wananawa maji tiririka, mnatumia senitizer, angalau mnajifukiza na kutumia chai za tangawizi nk, unapotoka nje kutafuta riziki kwa ajili Mahitaji na kulipa kodi lukuki za serikali Vaa barakoa, tembea na sanitizer mara unapotoka katika mihangaiko unajipakaza senitizer mikononi, yaani tufanye ule utaratbu kama ilivyokuwa katika awamu ya Outbreak ya kwanza ya Corona ambapo tulijifunza namna ya kujilinda na Corona au tumeisha sahau??!!.
Huu sio wakati wa kulaumu serikali ni wakati wa kuhamashishana kutekeleza yale yote tunaweza kufanya kama raia tunojitambua kwani Governments Come and go but people remain, we have to take the required steps to remain alive as lives ought to continue.