Hawa watu wanafanya kazi za hatari sana. Lakini licha ya mlipuko wa Corona bado wanaendelea kufanya kazi vile vile yaani business as usual. Hawana vifaa Kinga (PPE), hawatumii sanitizer Wala distancing yeyote from Uchafu wanaouzoa au ubeba.
Inawezekana Hawa Ni watu ambao pengine wanaonekana hawana umuhimu wa kulindwa lakini nahisi Ni watu ambao wanaweza kuusambaza huu ugonjwa kwa urahisi sana.
Hii Ni kwa sababu watu Hawa ndiyo wanaobeba Uchafu masaki au huko ushuani halafu wanakuja kuishi uswahilini.
Tunaomba wenye mamlaka wawatolee Hawa watu tamko.