#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
Huyo daktari yupo nyuma ya wakati. Udaktari ni fani kama fani nyingine. Kuna madaktari wazuri na wabaya. Wale ambao wana vyeti lakini hawajishughulishi na yanayoendelea Duniani.

Hiyo anayoisema huyo daktari ni falsafa ya mwanzo lakini baadaye WHO wamesema kuwa Covid 19 ni airborne disease. Na kwamba virus wale wakishatoka mdomoni mwa mwenye maambukizi wana uwezo wa kukaa hewani wakiwa wazima na bila ya kuanguka chini mpaka zaidi ya masaa manne.

Huyo daktari, kwenye huu ugonjwa mpya, ana utofauti mdogo sana na asiye na daktari. Yeye na sisi, wote tunafanya kusikiliza kwa wanaofanya utafiti. Hakuna utafiti unaofanyika Tanzania kiasi cha kuweza kusema kuna kitu wamekigundua tofauti na tunavyoelekezwa na taasisi kubwa duniani zinazofanya utafiti kuhusiana na ugonjwa huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msomi wa civics huyawezi Mambo ya science! Fanya kama unazipita tu hoja nyingine zisizokuhusu na kinyume chake piga kimya tu hutachekwa!
Uelimishweje uelewe kuwa covid anaenezwa kwa njia ya hewa? Usichoshe wengine hapa kwa ungumbaro wako!
Hapa nawasikiliza madaktari bingwa watatu kutoka wizara ya afya na ninaridhika sana na elimu wanayotoa.

Wewe endelea kupuliza mbege hapo migombani!
 
Nilitegemea majibu kumbe na wewe unaniuliza!
Toka ndani uende nje angalia upepo unavuma kuelekea wapi kama inatoka magharibi kuelekea mashariki basi wewe tema mate ikielekea uelekea inakotoka upepo alafu umsikilizs tena Daktari.
 
Corona inaambukizwa kwa njia ya hewa ila ni hadi mtu akohoe au apige chafya
 
Toka ndani uende nje angalia upepo unavuma kuelekea wapi kama inatoka magharibi kuelekea mashariki basi wewe tema mate ikielekea uelekea inakotoka upepo alafu umsikilizs tena Daktari.
Mkuu unanituma nifanye utafiti.......haya!
 
Msomi wa civics huyawezi Mambo ya science! Fanya kama unazipita tu hoja nyingine zisizokuhusu na kinyume chake piga kimya tu hutachekwa!
Uelimishweje uelewe kuwa covid anaenezwa kwa njia ya hewa? Usichoshe wengine hapa kwa ungumbaro wako!
mkuu huyo jamaa kama ashawahi kukuchukulia mke naomba umsamehe tu bure
 
Mimi siyo Daktari lakini mbona hizi vitu ni vidogo sana watu wanatakiwa watumie akili ya kawaida tu. Anaposema Corona inaambukizwa kwa njia ya Mate..kamasi na machozi je amesema vinasafiriaje kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kama siyo hewa.
Sasa mkuu hapa umeshakiri kuwa wewe sio Daktari sasa akili gani tena inatakiwa itumike.Mbona simple tu kuelewa kuwa ugonjwa unasambaa kwa njia ya majimaji ambapo ndio virusi vinaishi.We meza kama ilivyo mkuu
 
Lugha gongana!

Hotuba ya leo ya Mheshimiwa Rais imeiibua mambo ya kutofautiana na Viongozi wengine ambapo sasa Sijui tufuate yapi???!!

- Waziri mkuu kasema watu tukae ndani,
Mheshimiwa Rais kasema tupige kazi.

- Naibu waziri wa Afya kasema tusifukuzie tutaunguza mfumo wa upumuaji,
Mheshimiwa Rais kasema tufukuzie kwasababu joto kali, Corona virus anakufa!

- RC Dar anasema watu wa mikoa wasije Dar, Mheshimiwa Rais kasema waje tu maana ndio sehemu kubwa ya biashara na mapato ya Nchi.

- Waziri Afya anasema waliopona 11,
Mheshimiwa Rais kasema wamepona zaidi ya 100.

- Waziri Afya anaahidi kupuliza dawa za kuulia virus (Fumigation) kupulizwa maeneo yote muhimu ya Jamii huku RC Dar akisimamia zoezi hilo kikamilifu kwa mkoa wa Dar kupuliziwa huku akimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapa dawa hizo mkoa wake,
Mheshimiwa Rais amemuagiza IGP na TAKUKURU kufanya uchunguzi kwa walioagiza kupuliza dawa hizo kwasababu ni upuuzi mtupu na Corona Virus hauawi kwa kupuliziwa dawa!

#### Hayo ni machache kati yaliyojiri kwenye hotuba yake, fikiria hali ya hao Viongozi na matamko yao siku zijazo zitakuwaje??!
Anza kufuatilia takwimu zao ukipinganisha na zilizopita!
Fuatilia pia matamko ya kitaalam kuhusiana na kujikinga na Corona virus!

Tanzania ni yetu sote 💪🏾 🇹🇿

Stay Home
Stay safe
Jikinge na ugonjwa wa COVID-19 🙏🏾
 
vinatoka virus ambavyo kama mtu yupo karibu akivuta hewa vinamuingia katika mapafu
na virusi hivyo hukaa hewani mda mrefu kwa hiyo kama ukipita sehemu hiyo kisha ukavuta hewa pia utaambukizwa
Kwa mujibu ya maelezo ya dokta haiko hivyo!
 
Mimi siyo Daktari lakini mbona hizi vitu ni vidogo sana watu wanatakiwa watumie akili ya kawaida tu. Anaposema Corona inaambukizwa kwa njia ya Mate..kamasi na machozi je amesema vinasafiriaje kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kama siyo hewa.

Watu wakawekwa kwenye utupu je kuna uwezekano wa mate kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine iwapo wanasimama mita 6?

Tunaposema small particles je hajui kua zinasafirishwa kwa njia ya.hewa?
Nafikiri point yake ni korona sio airborne.
 
Karibu katika mjadala mzuri sana wa kuelimisha unaoendelea sasa hivi katika Luninga ya ITV, kipindi ni Malumbano ya hoja.

Up dates;
Bwashee, katika uhalisia wake virusi hivi hujulikana kama "airborne in its transmission" kwa lugha ya Kiingereza. Kwa hiyo basi njia ya hewa ni mojawapo yenye kuweza kuvisafirisha virusi hivi vikiwa ndani ya kitu cha hali ya maji maji kama vile mate, machozi na kohozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom