#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
Inaonekana kuvaa mask ni mtihani mkubwa sana kwa watanzania, napita huko barabarani naona watu wawili au mmoja waliovaa mask, wengine tunajua Corona ipo, ila na sisi tupotupo tu, tunasubiri tusikie leo wameambukizwa wangapi, tushtuke kidogo, tupige kelele zetu, tumuachie Mungu, then maisha yaendelee, hatuchukui tahadhari yoyote.

Sijui tukoje!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mizaha na kuchukulia powa mambo kama haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki mbili zimepita madaktar wetu kutoka wizara ya afya walitutangazia kuwa haina haja ya kuvaa facemasks kwasbb Coronavirus haienei Kwa njia ya hewa Ila kama ukiona dalili za Corona unaweza kuvaa mask ili kujilinda mwenyewe na wengine.......
Dr MAKONDA nae alituhasa tunawe mikono mara Kwa mara na sabuni inatosha sasa leo tuchukue ushauri wa Nani?
Ugonjwa ni mpya bado haujapatiwa details za kutosha,
Hiyo tegemea updates nyingi zaidi.
 
nikiwa natoka kwangu kuelekea kwenye mizunguko yangu huwa navaa mask, cha ajabu wabongo huwa wananiangalia kwa jicho kali wakihisi kama najiendekeza au naringa.

yaani huku uswahili kwetu ukivaa kale kamask wabongo wanakuangalia kwa jicho la husda sana.
 
Najiuliza hawa watu milioni 1 walioambukizwa korona WATAPONA KWELI?..
na mwisho wa corona ni lini?.
HUU mwaka watu wengi tuliamini utakuwa mzuri lakini kinachotokea ni balaa NA VILIO.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Wiki mbili zimepita madaktar wetu kutoka wizara ya afya walitutangazia kuwa haina haja ya kuvaa facemasks kwasbb Coronavirus haienei Kwa njia ya hewa Ila kama ukiona dalili za Corona unaweza kuvaa mask ili kujilinda mwenyewe na wengine.......
Dr MAKONDA nae alituhasa tunawe mikono mara Kwa mara na sabuni inatosha sasa leo tuchukue ushauri wa Nani?
Wale madokta ni taka taka kabisa. Kirusi kinakaa kwenye hewa na watu wanatakiwa kuvaa mask
 
Inaonekana kuvaa mask ni mtihani mkubwa sana kwa watanzania, napita huko barabarani naona watu wawili au mmoja waliovaa mask, wengine tunajua Corona ipo, ila na sisi tupotupo tu, tunasubiri tusikie leo wameambukizwa wangapi, tushtuke kidogo, tupige kelele zetu, tumuachie Mungu, then maisha yaendelee, hatuchukui tahadhari yoyote.

Sijui tukoje!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuvaa mask huko Asia ndiyo wamezoa ndiyo maana sasa hawaoni tabu yeyote ila tuliyobakia hali ni tofauti.
 
Huu ugonjwa umepiga dunia bila kujitayarisha.
Mask ni muhimu lakini mask zipo kidogo sana inatakiwa kubadirisha mask kila masaa 4.
Marekani ,Ulaya hawakujitayarisha kutengeneza mask za kutosha walikuwa wanategemea China.
Pia kunahitajika kukinga macho,inaonekana eneo lolote la binadamu lililo wazi ni mali ya Corona virus.
 
hizo mask tukivaaa dunia nzima zitatoshaa?
Ndo maana nchi tajiri Kama marekani zinahangaika kuagiza,kutengeza,kuiba na kudhulumu mask,kwasababu sio ishu ya kitoto hiyo.
Mwathirika akikohoa,virusi vinabaki in aerosol form hewani masaa nane,,maana yake mtu akipita Hilo eneo hata baada ya nusu saa anaweza vuta hivyo virusi.hata asipovuta mtu hivyo virusi vitatua popote na kusurvive kwa masaa kadhaa,
Ndo maana kule Wuhan,walikuwa wanapulizia madawa kila Kona,kila chocho,
 
Mask ndio mpango mzima, China walianza huu mtindo kwa muda mrefu sana kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya kutokana na wingi wao. Je, tutajifunza nini kutoka kwao? Je, viwanda vya Tanzania vipo tayari kuchangamkia utengenezaji wa mask? Hili ni soko kubwa sana huko tuendako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom