Kwa hali ilivyo, nilidhani serikali ingekuja na mwongozo wa kujilinda na corona badala ya kuhamasisha watu kusali, ikiwa viongozi wa serikali wanapoingilia mamlaka ya dini kama wao wasivyotaka kuingiliwa kwenye siasa.
Rais ni kiongozi wa serikali na sio kiongozi wa imani wa dhehebu lolote nchini, kutoa siku tatu na kusababisha mikusanyiko naona ni kushindwa kwa majukumu yake kama serikali.
Kazi ya serikali haipo katika imani bali katika kuwalinda raia wake kwa vitendo. Kama serikali ilitakiwa ije na miongozo namna ya kuwalinda watu wake mfano uvaaji wa mask, gloves, usafi, mazuio ya safari, mikusanyiko na nk.
Nachodhani ingekuwa ni lazima kwa wakazi wa Dar kuvaa mask na kunawa mikono, kufunga wakazi wa mji huo kutosafiri nje ya mji huo, vyombo vya usafiri kupulizwa dawa, abiria kuvaa mask muda wote.