Nzelu za bwino
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 400
- 484
Maombi hayambadilishi Mungu bali umbadilisha mtu. Kwa nini tusijadili sana ili la mtu kubadilika?Hii nukuu ya maneno yaliyotolewa na mchungaji PETER MSINGWA ambayo ninayatolewa ufafanuzi wa kina kwani moja moja yanabeza wito wa ulitolewa na Rais ili kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha janga la Corona
“maombi huwa hayambadilishi Mungu, maombi yanapaswa yambadilishe muombaji aache njia zake mbaya, ili mapenzi ya Mungu yatimie katika maisha yake”- Mchungaji PETER MSIGWA
NAOMBA NIFAFANUE KIDOGO ULICHOZUNGUMZA;
Kwanza, NI KWELI MAOMBI HAYAMBADILISHI MUNGU...kwa maana hajawahi kubadilika ni ni Yeye Yule, JANA na LEO na HATA MILELE (Waebrania 13:8).
Lakini maombi yanaweza kubadilisha mabaya (magonjwa/vifo/njaa/ukame n.k) yaliyotokana na maovu yetu tuliyoyafanya. Tuone baadhi ya Mifano ya kwenye Biblia;
Mfano wa 1: MUSA AKIWAOMBA MSAMAHA KWA AJILI YA WANA WA ISRAEL
Kutoka 32:9-14 “Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu? ........GEUKA KATIKA HASIRA YAKO KALI, UGHAIRI UOVU HUU ULIO NAO JUU YA WATU WAKO. Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele. NA BWANA AKAUGHAIRI ULE UOVU ALIOSEMA YA KWAMBA ATAWATENDA WATU WAKE.”
Tutazame mambo mawili hapo;
i. GEUKA KATIKA HASIRA YAKO KALI, UGHAIRI UOVU HUU ULIO NAO JUU YA WATU WAKO.
ii. NA BWANA AKAUGHAIRI ULE UOVU ALIOSEMA YA KWAMBA ATAWATENDA WATU WAKE.” (And the LORD repented “nachem in Hebrew” of the evil which he thought to do unto his people). Neno “nachem” linamaanisha –to be sorry, console oneself, regret.
“aYiNächem y'hwäh al-härääh ásher DiBer laásôt l'aMô"
Maombi ya mtu yeyote mwenye haki au aliyekuwa na dhambi akaamua kumgeukia Mungu, Mungu huponya na kumuondoa katika uangamivu. Hivyo, hatuombi kwa ajili ya kumbadilisha Mungu bali kubadilisha kile kibaya kilichokuwa kitupate au kilichotupata kutokana na uovu/dhambi zetu.
“Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa (Zaburi 107:6)”
Mfano wa 2. MAOMBI YA MUSA NA HARUNI KWA MUNGU DHIDI YA GHADHABU YA BWANA KWA WANA WA ISRAEL
Hesabu 16:43-48“Na Musa na Haruni wakaenda hapo mbele ya hema ya kukutania. Naye Bwana akanena Na Musa, Na kumwambia, Ondokeni kati ya mkutano, ili niwaangamize mara moja. Wao wakapomoka kifudifudi. Musa akamwambia Haruni, Haya, shika chetezo chako, ukatie moto ndani yake, moto wa madhabahuni, kisha utie na uvumba juu ya moto, ukakichukue haraka, wende nacho katika huo mkutano, ukawafanyie upatanisho; kwa kuwa ghadhabu zimetoka kwa Bwana; hiyo tauni imeanza. Basi Haruni akakishika chetezo kama Musa alivyonena, akapiga mbio akaenda katikati ya mkutano; na tazama, tauni ilikuwa imeanza kati ya watu; akatia uvumba juu ya moto na kufanya upatanisho kwa ajili ya hao watu. Akasimama kati ya hao waliokufa na hao waliokuwa wakali hai; tauni ikazuiwa.”
Tauni (ugonjwa) iliwapiga wana wa Israel, MUSA na HARUNI wakaamua kumuomba Mungu, na Tauni ikazuiliwa baada ya kuuwa watu 14,700 ukiendelea kusoma mstari wa Hesabu 16:49. Leo PETER MSIGWA unakatisha watu tamaa kuomba kwa maombi yanambadilisha muombaji wakati maombi yana uwezo wa pia kubadili mambo yaliyojitokeza katika jamii kama Corona.
MFANO WA 3. NINAWI DHIDI YA UNABII WA
YONA
YONA 3:4-10 “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
Je, MSIGWA hapa Mungu hakubadili kusudio lake baada ya maombi ya watu wa Ninawi wakiongozwa na Kiongozi/Mfalme/Rais?
Mch. PETER MSIGWA, Mtumishi wa Mungu hebu acha kuchanganya siasa na masuala muhimu ya Kiroho. Kama Mchungaji ungekuwa mstari wa mbele kuwaongoza na kuwafundisha watu kutumia nafasi ya maombi Kitaifa ambayo Mhe. Rais Dkt. JOHN MAGUFULI ametangaza.
Siyo kuonesha watu kwa maombi yanayofanyika si kitu, wala hayawezi kusababisha Mungu akafanya jambo jipya Tanzania kufuatia CORONA. Je, Mungu anachagua magonjwa ya kuponya? Hakuna linalomshinda Mungu.
TANZANIA TUENDELEE KUMUOMBA MUNGU KWA MAANA YEYE NDIYE NGOME YETU NA TUMAINI LETU
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS WETU DKT. JOHN POMBE MAGUFULI
1 Chronicles 21:15 Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, Bwana akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa Bwana akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Jeremiah 26:19 Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha Bwana, na kumwomba Bwana awafadhili; naye Bwana akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Na sisi tungetenda mabaya makuu juu ya roho zetu.
Amos 7:3 Bwana akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana.
Amos 7:6 Bwana akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.
Acts 7:42 Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
1 Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme.
2 Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.
3 Bwana akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana.
4 Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukavila vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu.
5 Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, acha, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.
6 Bwana akaghairi katika jambo hili pia. Jambo hili halitakuwa, asema Bwana MUNGU.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mfano kuweka mazoea ya kunawa maji tiririka kwa sabuni.
2.kujizuia kushiriki mikusanyiko isiyo ya lazima kama vile kucheza bao nk.
3.kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
4.kutoa taarifa kwa mamlaka husika unapo muona mtu mwenye viashiria vya mambukizi.
5.kubadilika kitabia kwa binadamu kumesaidia mataifa mengi kupunguza maambukizi ikiwemo Italy, I spania, marekan, afrika kushiriki nk.
6.kwani ni sisi tusibadilike maana sio vibaya kuiga mazuri kwa faida yetu na vizazi vyetu.