Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Boss Clemence Mwandambo Imani inaenda na Matendo ... Imani bila Matendo Ni Batili.

Nampongeza Mh. Rais kwa kuwa Upande wa Imani.

WaTanzania na Wananchi wote tuzidi kuchukua taadhari, Corona Inaua.


Nimeyapenda maneno haya, watanzania tuingie kwenye maombi, hakika tutashinda hii vita inayotukabili, hii vita ya korona, ni Mungu pekee anayeweza kutushindia, raisi wetu ameonyesha njia, tusimame kwa imani tusonge mbele Mungu ataliponya taifa. Hakika Mungu atajidhihirisha na dunia itashangaa. Watanzania tuungane bila kujali dini wala siasa.
View attachment 1421261
 
Truth Teller,
Siyo muhimu sana kuonana naye. Huu ugonjwa ulianzia China December 2018 na leo ni April 2020. Tuliambiwa sisi Mungu anaipenda nchi yetu hauwezi kuingia. Tukaambiwa na tunaendelea kuambiwa tukachape kazi.

Kama tumeiweka pembeni sayansi na njia walizotumia wengine tumezikataa ni sawa. Mungu wetu alipaswa kuwa North Korea aliyefunga mpaka kuanzia December mwaka jana.

Sisi tumeamua kuitamani fedha zaidi kisha kumwachia Mungu alinde afya zetu. Bado watu wapo wanakesha kwenye vilabu vya pombe, wanakusanyika misikitini, makanisani, masokoni na kwingineko.

Mungu anaweza kuamua kutusikia lakini akashindwa namna ya kutusaidia. Hii naigananisha na mtu anakunywa sumu kisha anamwomba Mungu amsaidie asife.
 
G Sam,
Angesa tukatambike ningemwelewa Wataliano Wenyewe wamesusiwa na YESU Siku hizi Tatu nitafanya matambiko Yakutia sad aka ya Dani na NYAMA ILA SITAKUSANYA WATU
 
Kukusanya wdatu ni kuongeza maambukizi.Mtu anaweza kuomba hata kama anatembea barabarani.
 
Kwa hiyo ni moja ya mikakati yake ya "Do nothing" dhidi ya corona kwa hiyo mkakati wake wapili ni kwenda kulundikana kwenye nyumba za ibada na kupigiana chafya hahahaa

Kwa huyu tuliingia choo cha kike
Strange kuna majitu yanaimba mapambio!
 
Baada ya siku tatu mnaanza kupukutika, sali siku tatu muombe kusaehewa dhambi maana kifo kinapamba moto!
 
G Sam,
Na kwa wasio sali itakuwaje?

Je, hii itakuwa ni kwetu tu, Tanzania, au kwa nchi zote duniani hata kule kwa mabeberu? Yaani, sisi tusali, halafu na wao wafaidike kwa sala zetu?

Au sisi ni 'special' sana, vipenzi wa Mungu, tukisali na kuomba tutasaidiwa; lakini wale wengine, kati yao waliosali sana haikufua dafu!

Hapa nadhani tunalishwa saikolojia tu hakuna la ziada!
 
Ile hali iliyotokea maeneo ya Dar na kwingineko saa 12 jioni hakika ilikuwa fikirishi. Kwa wale wasomaji wa biblia Genesis 8 Ile Rainbow ilikuwa na maana kubwa hasa wakati huu wa hili janga la Corona. Tumuombe kwa Imani zetu.
 
Ile hali iliyotokea maeneo ya Dar na kwingineko saa 12 jioni hakika ilikuwa fikirishi. Kwa wale wasomaji wa biblia Genesis 8 Ile Rainbow ilikuwa na maana kubwa hasa wakati huu wa hili janga la Corona. Tumuombe kwa Imani zetu.
achana na thinking ya kienyeji as if you have not gone to school.Kwanini ukitupa jiwe linarudi chini, MUNGU KAPENDA!
 
Hi ni dalili ya kukata tamaa
Inawezekana.

Lakini usisahau kuwa inaweza kuwa sehemu ya kulaza watu akili. Taifa linapokuwa na wajinga wengi hata mbinu za kilaghai hufanya kazi.

Kwa mfano namsoma mkuu 'Barakoa' hapo na kutikisa kichwa. Tupo wengi sana wa aina hii ndani ya nchi yetu!
 
Inawezekana.

Lakini usisahau kuwa inaweza kuwa sehemu ya kulaza watu akili. Taifa linapokuwa na wajinga wengi hata mbinu za kilaghai hufanya kazi.
Matatizo ya kisayansi yanahitaji ufumbuzi wa kisayansi na matatizo ya kiimani yanahitaji ufumbuzi wa kiimani.
 
Back
Top Bottom