Mimi nnachokiogopa ni kwamba Watanzania ukishawaambia swala hili tuliweke mikononi kwa Mungu, wao hua wanaacha kila kitu na kuanza kutegemea Mungu atawasaidia.
Mifano imejaa:
- tuna watu wengi tu badala ya kufanya kazi wao wanajazana makanisani kuombewa ili wawe matajiri
- badala ya kusoma wao wanaenda kusali ili wafaulu mitihani
- badala ya kwenda hospitali wao wanashinda kwenye maombi ili wapone magonjwa nk.
Kwa akili hizi tutegemee kabisa watu wengi sasa wataacha kufuata maelekezo ya wataalamu, na kuanza kufuata maelekezo ya jiwe ya kuomba huku wakidhani kwamba hicho ndio kitakachowaokoa na corona.
Kuomba Mungu kunatakiwa kuende sambamba na elimu ya kujikinga, hatua za kuzuia maambukizi, ongezeko la huduma na vifaa-tiba nk.