Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Kuna watawala kadha wa kadha walipokabiliwa na hatari na maadui ambao hawana uwezo nao, walitumia njia hii ya kumwomba Mungu na Mungu akawapigania na kuwashindia. Naamini hata sasa, Mungu aweza (ikiwa ni mapenzi yake) kupigana upande wetu dhidi ya Corona na tukapata ushindi
Enzi za hizo utawala,kama umependa kumuingiza Mungu,kulikuwa na maovu kama ya leo? Alikupa akili uweze kuchambua lipi jema,lipi baya. Kwa hiyo,mtasubili na Corona ndo aje aamue nini chakufanya? Utasubili sana
 
Serikali inachapa watu vibokonusiku kwenye mabar kwa kutumia askari wakati hawajatangaza lolote, watangaze tu kufunga hayo Mabaa na lockdown ifuatie baadae ugonjwa hauna aibu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
thats the bold and strong move, huku tukizingatia tahadhari zitolewazo ndio njia pekee itakayoyuvusha katika hili. Tukisema tunapambana we are doomed!

Naimani wote watu 50+mill tutakutana 31 dec kusherehekea mwaka mpya tukiwa wazima wa afya tele. Tupambane na hofu ndio mbaya zaidi
Kweli tupu. Wao wanataja magari, wengine farasi lakini sisi tutataja jina la Mungu wa majeshi. Tutavuka salama.
 
Mimi nnachokiogopa ni kwamba Watanzania ukishawaambia swala hili tuliweke mikononi kwa Mungu, wao hua wanaacha kila kitu na kuanza kutegemea Mungu atawasaidia.

Mifano imejaa:
- tuna watu wengi tu badala ya kufanya kazi wao wanajazana makanisani kuombewa ili wawe matajiri
- badala ya kusoma wao wanaenda kusali ili wafaulu mitihani
- badala ya kwenda hospitali wao wanashinda kwenye maombi ili wapone magonjwa nk.

Kwa akili hizi tutegemee kabisa watu wengi sasa wataacha kufuata maelekezo ya wataalamu, na kuanza kufuata maelekezo ya jiwe ya kuomba huku wakidhani kwamba hicho ndio kitakachowaokoa na corona.

Kuomba Mungu kunatakiwa kuende sambamba na elimu ya kujikinga, hatua za kuzuia maambukizi, ongezeko la huduma na vifaa-tiba nk.
 
Hili suala si la mzaha tunahitaji sana kuwa karibu na mungu wetu, yeye ndie atatupa njia ya wokovu pamoja na jitihada zetu
Siku zote tunatakiwa kuwa karibu na Mungu wetu. Na kumtanguliza ktk kila jambo. Tusisubiri tunapopata majanga ndio tukumbuke kuwa kuna Mungu. Hapo ni sawa na kujifunza kuogelea wakati unazama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jambo zuri.
Mimi naamini sana katika MUNGU muweza wa yote

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Siku zote tunatakiwa kuwa karibu na Mungu wetu. Na kumtanguliza ktk kila jambo. Tusisubiri tunapopata majanga ndio tukumbuke kuwa kuna Mungu. Hapo ni sawa na kujifunza kuogelea wakati unazama.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna tofauti kati ya kumtegemea Mungu na kumtegea Mungu sisi tunamtegea na itatucost sana....


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nanukuu maneno ya baba wa taifa kwamba nchi hii haina dini ila watu mmoja mmoja ndio wana dini, hivyo si vema kuwaambia watu waswali na kusali wakati nchi ina watu wengi wapagani na wenye chuki na dini lazima tutofautishe utawala na dini maana kama nchi hatuna dini ndio maana hata wapagani kama wakina Kingunge walituongoza bila shida hatukuangalia dini zao.

Dini isitumike kama kichaka cha kubweteka na kushindwa kujikinga na serikali kushindwa kubeba jukumu lake la kupambana na corona kwa kununua vifaa.

Hv mpaka muone watu wanaanza kuanguka misikitini na makanisani na kufa ndio muone huu ungonjwa upo serious? endeleeni kuwakusanya watu outcome yake mtaona
 
Nanukuu maneno ya baba wa taifa kwamba nchi hii haina dini ila watu mmoja mmoja ndio wana dini, hivyo si vema kuwaamia watu waswali na kusali wakati nchi ina watu wengi wapagani na wenye chuki na dini lazima tutofautishe utawala na dini maana kama nchi hatuna dini ndio maana hata wapagani kama wakina kingunge walituongoza bila shida hatukuangalia dini zao.
Kwani kasema nchi hii inadini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom