Coronavirus: Safari zote za Hijja zapigwa marufuku kwa muda Saudi Arabia

Coronavirus: Safari zote za Hijja zapigwa marufuku kwa muda Saudi Arabia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali ya Saudi Arabia imezuia wageni wote wanaoingia nchini humo kwa safari za kidini, ikiwemo wanaotembelea miji mitakatifu katika dini ya Kiislamu - Makka na Madina.

Mamilioni ya watu huingia Saudia mwaka mzima kufanya ibada ya Umra, na wengi zaidi huingia kwa pamoja kufanya ibada ya Hija.

Tofauti na Hija, Umra hufanyika katika kipindi chochote cha mwaka, na kwa sasa marufuku hiyo inawalenga mahujaji raia wa nchi za nje wanaoenda kuitekeleza.

Bado haijulikani kama ibada ya Hija, ambayo inategemewa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai kama itaathirika na zuio hilo pamoja na kusambaa kwa Virusi vya Corona duniani.

Saudia pia imewapiga marufuku watu kutoka nchi zilizokumbwa na virusi hivyo kuingia nchini humo.

Mpaka sasa Saudia bado haina mtu ambaye amethibitika kuambukizwa virusi hivyo.

Makka, ndio mji ambao Mtume Muhammad alipozaliwa, na kuna msikiti mtakatifu zaidi. Madina ndipo alipofariki na kuzikwa.

Wizara ya mambo ya nje ya Saudia inasema marufuku hiyo ni ya muda - lakini wizara hiyo haijataja lini marufuku hiyo itaondolewa.

Watalii ambao si wa kidini ambao wanatoka katika nchi ambazo virusi vya corona vimethibitisha kuingia pia watakataliwa kuingia Saudia.

Saudi Arabia imeeleza kuwa toka mwezi Oktoba imetoa viza zaidi ya 400,000 za watalii kutoka nchi mbalimbali duniani.

Shirika la Afya Duniani (WHO) mapema wiki hii limeonya kuwa dunia inapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya corona.

WHO japo imesema kuwa ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika "awamu ya maandalizi".

Janga ni pale maambukizi ya ugonjwa yanaposambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika maeneo mengi ya dunia.

Visa zaidi vya virusi ambavyo husababisha ugonjwa kupumua Covid-19, vinaendela kujitokeza, huku milipuko ya ugonjwa huo ikibainika katika mataifa mengi zaidi ya Uchina mabapo ndipo ulipoanzia.

Mpaka sasa zaidi ya watu 2,700 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Toka Virusi vya Corona viripotiwe mwezi Disemba, zaidi ya watu 80,000 duniani, kutoka katika mataifa takribani 40 tayai wameshaambukizwa virusi hivyo. Wengi wao wakiwa nchini Uchina.

Iran (ambayo imetenganishwa na Saudia kwa mkondo mwembamba wa bahari) mpaka sasa imesharipoti vifo 19 - ambayo ni namba kubwa zaidi ya watu kwa mataifa ya nje ya Uchina.

Hata hivyo vifo hivyo vinatokana na wagonjwa 139, hali ambayo inawafanya madaktari wa magonjwa ya kuambukiza kuhofia kuwa nchi hiyo inaweza kuwa na wagonjwa wengi zaidi inaowaficha.

Barani Ulaya hali ni mbaya zaidi nchini Italia ambapo mpaka sasa watu 400 wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo kutoka watu 80 siku ya Jumanne. Watu 12 tayari wameshafariki nchini humo kutokana na mlipuko huo.

Kwa Afrika ni nchi mbili mpaka sasa zimethibitisha kuingia kwa ugonjwa huo. Algeria na Misri kila moja imeripoti mgonjwa mmoja.

Chanzo: BBC
 
Mungu kashindwa kuwanusuru watu wake na janga hili?

Hata wanaokwenda Hijja?

Huyo Mungu yupo kweli au ni hadithi za watu tu?
Acha kashfa wewe,

unajiona umekamilika kwa vile ubongo wako unakudanganya kwamba unaweza kufanya clear reasoning.

Ipo siku Mwenyezi Mungu atajidhihirisha kwako kwa njia ambayo itakustaajabisha.

Punguza kashfa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kashfa wewe,

unajiona umekamilika kwa vile ubongo wako unakudanganya kwamba unaweza kufanya clear reasoning.

Ipo siku Mwenyezi Mungu atajidhihirisha kwako kwa njia ambayo itakustaajabisha.

Punguza kashfa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa, hujajibu swali.

Pili, wanaosema Mungu yupo ndio wanaojiona wamekamilika, wana majibu ya kila kitu kwa kumjua Mungu. Mimi najua sijakamilika, ndiyo maana naeleza kutomuelewa kwangu huyo Mungu wenu.

Na bado hujanielewesha huyo Mungu wenu kashindwaje kuwanusuru watu wanaotimiza nguzo ya dini yake.

Unanisimanga na kuninyanyasa kwa kuuliza swali ambalo huwezi kujibu.

Kabla ya kuniambia ipo siku Mungu atajidhihirisha kwangu, kwanza thibitisha yupo.

Halafu nitajie siku hiyo ni tarehe ngapi, mwezi gani, mwaka gani, ili tuingoje, asipojidhihirisha turudi hapa kujadili zaidi.

Acha longolongo.

Thibitisha Mungu yupo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu kashindwa kuwanusuru watu wake na janga hili?

Hata wanaokwenda Hijja?

Huyo Mungu yupo kweli au ni hadithi za watu tu?
Mkuu hata mimi kuna muda huwa najiuliza kwa nini inakuwa hivi yaani baadhi ya vitu Mungu anashindwa kuzuia na uwezo anao.

Bado nasoma kile kitabu uliwahi weka hapa siku nyingi

'Philosophy of religion. An anthology'

Kwa kweli nimejifunza vingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hata mimi kuna muda huwa najiuliza kwa nini inakuwa hivi yaani baadhi ya vitu Mungu anashindwa kuzuia na uwezo anao.

Bado nasoma kile kitabu uliwahi weka hapa siku nyingi

'Philosophy of religion. An anthology'

Kwa kweli nimejifunza vingi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kile kitabu kimekusanya mambo mengi sana.

Kina maelezo si tu yanayopinga uwepo wa Mungu, bali pia yanayotetea uwepo wa Mungu.

Tatizo watu wengi kusoma ni shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran wame cancel Friday prayers.

Mungu kashindwa kuwanusuru watu wake wanaotaka kusali Ijumaa?

Kweli huyu Mungu yupo au ni hadithi za watu za uongo tu?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Flight moja imetua kutoka china straight to Kenya na wachina kama 200 eti na wenyewe watakaa siku 14 ndiyo waachiwe uraiani sa si ndo yale ya ile meli mki achiwa ana kutwa mmoja mmoja tayari ana corona na amesha ambukiza

Sent using Jamii Forums mobile app
Wachina Wameachiwa waende uraiani ila wameambiwa wajitenge wenyewe na Raia kwa siku 14.
Wameambiwa wajipe Self quarantine ya siku 14.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom