Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Afadhali aisee maana watu wazima kidogo wanaweza kujikinga ila watoto ni mtihani.
 
Salary Slip,
..na MISAFARA YA JPM na mikutano yake na jinsi wanavyopokezana zile mics nadhani ipigwe marufuku mpaka balaa hili litakapopita.
 
1.Eti anasema watu wanashauriwa kuhairisha safari? Badala ya kusitisha safari.
2. Eti waendelee kupima watu airport instead ya kuzuia wageni kuingia.

Serikali yetu haijali wananchi wala haitutakii mema.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi Sina bando ya kumsikiliza youtube! Hivi amesema kama watawaajiri wataalamu wa afya japo kwa muda mfupi? Vipi kuhusu vifaa?
 
Waziri Mkuu hii ni hatua njema lakini haitoshi.

Mikusanyiko yote (pia vyuo vyote, matamasha, michezo, makanisani, misikitini nk) ya watu ilikuwa muhimu isitishwe na mipaka ya nchi kufungwa angalau 14 days. Kisha tuone upepo tokea hapo.

Enyi wenye dhamana mnayo nafasi ya kuitendea mema nchi hii sasa. Mkiiacha nafasi hii historia itakuwapo kuwahukumu.

Simamisheni miradi ya maendeleo tupambane na adui yetu huyu kwanza.

Wenzetu wamefanya hivyo, kwa nini kigugumizi hiki kwenu?
 
Wale wa boarding bora wabaki huko maana wanaweza kupata wakiwa njiani kuelekea kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…