Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Atasimama Nasi Wakati Wote Huu Wa Corona Virus Diseases 19
 
Kwa nini kuna kigugumizi kwenye kufunga mipaka au kulazimisha 14 days isolation kwa yoyote anayeingia? Hivi ukifunga shule huku umeruhusu watu kuingia hovyo nchini kuna faida gani? Kwenye inshu ya Corona serikali imekuwa legevu sana.
 
Watanzania sijui tukoje, Ulaya penye nyezo zote zinazowezesha watu kujikinga wamefunga mikusanyiko zote.
Huku bado tunasuasua kwa kufunga shule na michezo ila tunaacha magulio...soko kubwa kama kariakoo..vyuo vyote vya kati na juu,..Usafiri wa anga na majini.
 
Vikifungwa nitafurahi Sana, nitapata muda wa kusafiri hapa na pale ikiwemo kwenda Arusha kumjulia hali yule Mama mwenye umri wa miaka 46 anayekaa Sakina ambaye kwa Sasa amewekwa karantini na serikali. Lazima nimjue maana kujulikana dunia nzima kwa muda wa siku moja si haba. Jamani umaarufu unatafutwa hauji tu kama kifo
Online tutorials kibongo bongo bado! Ni kheri vyuo vifungwe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vyuo vikuu vingefungwa pia,kwa sababu kuna baadhi ya wanafunzi na ma -lecturer hutokea nje ya nchi ,naona kama itakuwa ni hatari zaidi kuliko kuwaacha na kuendelea na masomo.
 
Tunashukuru kwa hatua hizi zinazo chukuliwa, lakini ni wazi kuwa tumechelewa uwezekano wa kuzuia huu ugonjwa ulikuwapo Kama tungechukua hatua mapema.

Tusiishie hapa tu nadhani mkizuia safari watu kutoka na kuingia nchini itakuwa vyema zaidi, japo athari za kiuchumi zitakuwa kubwa zaidi ukizingatia nchi yetu ni Importer na si exporter.
 
Sio kuiga nchi hili ni suala la kufikiri tu kwa mfano Uganda ilianzisha Karantini kwa raia wanaotoka nchi za Category 1 yaani China Italy na Iran karantini ya siku 14
Huo ulikuwa ni uamuzi wa Uganda bila kuiga nchi nyingine
Karantini nchi nyingi zinafanya... Ila hiyo hoja yako practically haipo.
 
Back
Top Bottom