Kabla ya yote nikiri mimi ni miongoni mwa ninaomheshimu Magufuli na serikali yake pia nafurahishwa na jinsi alivyo mwepesi kwenye kufanya maamuzi mbalimbali bila ya kusita.
Kutokana na mlipuko wa Corona, dunia nzima inajaribu kujilinda kwa kufunga mipaka au kulazimishwa watu kutengwa kwa siku 14 baada ya kuingia kwenye mipaka yao. Inacho shangaza Tanzania tunahangaika na kuzuia mikusanyiko, kufunga shule wakati mipaka tumeiacha wazi. Kilichopo airports zote duniani ni temperature screening kwa kutambua udhaifu wa hili ndio maana nchi nyingi zimeamua kufunga mipaka au kulazimishwa wanaoingia wote kutengwa.
Kwanini kuna kigugumizi kwenye hili, hivi tunazuia UMITASHUMITA na mbio za Mwenge huku mipaka tumeiacha wazi tu, hizi ni akili gani, viongozi wetu wanaelewa risk wanayotuweka, hata tukisema wanalinda soko la Utalii ila ukweli hakuna watalii kwa kuwa karibia nchi zote za Ulaya na Marekani ambazo tunategemea watalii wengi zipo katika hali ya dharura, tunataka hadi ugonjwa uingia mtaani ndio tufunge mipaka?
Wapo ambao wanafikiri kufunga mipaka ni kuzuia pia bidhaa kutoka nje, si kweli, tunaweza kufunga mipaka huku tunaruhusu bidhaa kuingia kwa utaratibu maalum, Uarabuni wanategemea chakula chao chote kutoka mataifa mengine na wamefunga mipaka, hivi tunasubiri hadi ugonjwa uingie mtaani uathiri hadi watu wanaotegemea kufanya kazi asubuhi wapate mlo wa mchana tuwaambie wajifungie ndani? Naamini wahusiki wanapita humu, wajue tumechoka ulegelege wao kuchukua maamuzi ya kufunga mipaka, athiri zote zitazokuja ugonjwa ukisambaa tutawabebesha wao.