Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

@"Salary Slip,
Katikati ya wiki iliyopita alituhakikishia kuwa serikali imesambaza wataalamu nchi mzima kuidhibiti Corona! Lugha ya wataalamu wa kuidhibiti Corona sijawahi kuisikia popote zaidi ya Tanzania, chini ya wiki Corona hii hapa.
 
Shida yetu ni kwamba hoja huwa tunazipuuza
Kuna hoja zinafaa zitekelezwe kabla ya tukio na zingine baada ya case kuwepo nchini.... Kabla ya corona kuingia kinachotakiwa kufanyika ni labda kuzuia safari au sivyo kuandaa karantini... Lakini huwezi kufunga shule na vyuo kabla tatizo halijaingia nchini kaka...kuilaumu serikali kisa haijafunga taasisi za elimu kabla mdudu kutua ni kuionea.
 
Bars, restaurants na night clubs bado viko wazi Shule tu ndo zinafungwa?.😳

Itafikia pahala mikusanyiko yote itapigwa pini, kaeni mkao wa kula.

Ila siasa bana...hata nchi nzima kukiwa na total lockdown, bado kuna watu wataoilaumu serikali tu.

Wapo wataosema hakuna haja hiyo na wapo wataosema hiyo haitoshi!
 
Kabla ya yote nikiri mimi ni miongoni mwa ninaomheshimu Magufuli na serikali yake pia nafurahishwa na jinsi alivyo mwepesi kwenye kufanya maamuzi mbalimbali bila ya kusita.

Kutokana na mlipuko wa Corona, dunia nzima inajaribu kujilinda kwa kufunga mipaka au kulazimishwa watu kutengwa kwa siku 14 baada ya kuingia kwenye mipaka yao. Inacho shangaza Tanzania tunahangaika na kuzuia mikusanyiko, kufunga shule wakati mipaka tumeiacha wazi. Kilichopo airports zote duniani ni temperature screening kwa kutambua udhaifu wa hili ndio maana nchi nyingi zimeamua kufunga mipaka au kulazimishwa wanaoingia wote kutengwa.

Kwanini kuna kigugumizi kwenye hili, hivi tunazuia UMITASHUMITA na mbio za Mwenge huku mipaka tumeiacha wazi tu, hizi ni akili gani, viongozi wetu wanaelewa risk wanayotuweka, hata tukisema wanalinda soko la Utalii ila ukweli hakuna watalii kwa kuwa karibia nchi zote za Ulaya na Marekani ambazo tunategemea watalii wengi zipo katika hali ya dharura, tunataka hadi ugonjwa uingia mtaani ndio tufunge mipaka?

Wapo ambao wanafikiri kufunga mipaka ni kuzuia pia bidhaa kutoka nje, si kweli, tunaweza kufunga mipaka huku tunaruhusu bidhaa kuingia kwa utaratibu maalum, Uarabuni wanategemea chakula chao chote kutoka mataifa mengine na wamefunga mipaka, hivi tunasubiri hadi ugonjwa uingie mtaani uathiri hadi watu wanaotegemea kufanya kazi asubuhi wapate mlo wa mchana tuwaambie wajifungie ndani? Naamini wahusiki wanapita humu, wajue tumechoka ulegelege wao kuchukua maamuzi ya kufunga mipaka, athiri zote zitazokuja ugonjwa ukisambaa tutawabebesha wao.
 
Serikali inapaswa kuchukua hatua zaidi ya hizo zikiwemo;
kufunga sehemu za umma kama mabenki, vyuo, masoko makubwa kama kariakoo, mlimani city, makanisa nakadharika.
 
Ila siasa bana...hata nchi nzima kukiwa na total lockdown, bado kuna watu wataoilaumu serikali tu.

Wapo wataosema hakuna haja hiyo na wapo wataosema hiyo haitoshi!
Hilo ni kweli. Hata hivi sasa serikali bado inakuwa reactive instead of being proactive. Given the fact hili suala limefahamika well in advance na tv etc wanazo. Nadhani serikali inaenda taratibu kwasababu wanafahamu janga litakaloukumba uchumi wetu kutokana na hatua hizo mfano Total lockdown.

Na tunapoelekea hilo halikwepeki, kwahiyo waliokuwa wakilalamika vyuma vimekaza, wajindae maana vinaenda kupata kutu kabisa.
 
Kuna hoja zinafaa zitekelezwe kabla ya tukio na zingine baada ya case kuwepo nchini.... Kabla ya corona kuingia kinachotakiwa kufanyika ni labda kuzuia safari au sivyo kuandaa karantini... Lakini huwezi kufunga shule na vyuo kabla tatizo halijaingia nchini kaka...kuilaumu serikali kisa haijafunga taasisi za elimu kabla mdudu kutua ni kuionea.
Huyu mdudu anasambaa kwa haraka sana na tumeshuhudia anavyovamia nchi hadi nchi sasa tungojee mpaka aingie aanze kuleta madhara katika jamii?

Tuliposikia Kenya na Rwanda zimepata maambukizi tungetakiwa tuchukue tahadhari
 
Safi sana hii tahadhali.nashauri pia kwenye usafiri wa gari abiria wasisimame wakae levo siti mana wakisimama kugusana ni rahisi,hili mnalionaje wadau? mabaa nayo yafungwe watu wakilewa wanagusana hovyo huko
 
Hongera serikali kwa kuchukua hatua za haraka baada ya Corona kuingia nchini. Hatua zingine ziendelee kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanaotoa huduma hizi hospitalini, vifaa vya kuzuia maambukizi hasa sekta binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila siasa bana...hata nchi nzima kukiwa na total lockdown, bado kuna watu wataoilaumu serikali tu.

Wapo wataosema hakuna haja hiyo na wapo wataosema hiyo haitoshi!
Waswahili wana nongwa hawa si mchezo!

Maambukizi ya corona hayazuiliki hata ufunge haja kubwa! Tunachoweza kufanya ni kupunguza tu ukubwa wa athari!

Hebu fikiri tu kuhusu zile daladala pale Dar es salaam! Jinsi watu wanavyosongamana na kugombaniana kama mandondocha!

Corona is unstoppable given the situation! Hata ufunge kitu gani, miingiliano haiepukiki hata iweje!

Habari njema ni kwamba corona sio ugonjwa hatari kihivyo. Ni hofu tu za hawa waswahili wajinga wajinga wasio na ufahamu.
 
Back
Top Bottom