Course gani nzuri katika Utumishi wa Umma upande wa ajira?

Course gani nzuri katika Utumishi wa Umma upande wa ajira?

Ngazi gani mzee?? Mi nakushauri chukua Human Resource Management. Hii course ni kiraka. Kiraka kweli kweli, kwa week hukosi sehemu ya kutuma maombi. So naweza sema kwa sasa ni moja ya course zilizokatika soko.
 
Hakuna course yenye uhakika wa ajira mkuu, punguza wenge. Kuna watu wamesoma Record management wanamaisha mazuri tu mtaani, maisha hayana formula
 
Soma hiyo records inatosha mengine utajiendeleza ukiwa ajirani
 
kwa ngazi ya certificate nmechaguliwa moja kwa moja lakini wametuambia tunaweza kubadilisha course kama tunataka
Okay!! Hapo nimekusoma vizuri. Sijajua HRM kwa ngazi za chini inafanyaje kwenye Labour Market, mara ya kwanza nilibase kwenye Degree.
 
Watu mnasoma ili kufuata soko la ajira badala ya kusoma kike kilichopo moyoni mwako. Ndio maana aftika tunapoteza muda tu hapa duniani tukifa hatuachi legacy yoyote kwenye jamii
"Aftika" ndo nini ?
 
Hahahahahah we soma chochote kile ila kwa hali ilivyo mtaani ningesoma uhasibu tu maana ndio naona ni kitu chepesi kuajirika hata ukiwa na diploma tu.
 
Kwanza soma unachekipenda toka moyoni mana itakutanua akili katika nyanja nyingi ukiwa unasoma muombe Mungu akutangulie pia kwanini umeeka mitazamo mingi sana kwenye kuajiriwa why usfikirie na kuja kujiajir pia but sina maana mbaya wala kutaka kukukatisha tamaa but nikwambia coz na mm nilikua na mentality iyo so ni kama wakati na soma niliiblock akili kutanuka which is so bad nimekuja kugundua mtaani but muhimu muombe Mungu wako tu
 
Ngazi gani mzee?? Mi nakushauri chukua Human Resource Management. Hii course ni kiraka. Kiraka kweli kweli, kwa week hukosi sehemu ya kutuma maombi. So naweza sema kwa sasa ni moja ya course zilizokatika soko.
Acha kumdanganya mwenzio
 
Hrm si bora ungesema maendeleo ya jamii au social work?
Pitia matangazo ya ajira (ukirelate na alichosema record management) kusanya then angalia mtu anaehitajika sifa zake. Kumbuka HRM ina uwanja mpana sana ukilinganisha hizo ulizotaja, kila sehemu unaingia. Kwa utawala/Uongozi HRM ndo iko vizuri.

Pitia matangazo ya kazi uone kama watakuambia tunahitaji Community Development au Social work... Kama yapo ni percentages ndogo sana boss.
 
tayali nimeshaweka matokeo kwenye post yangu
Records management ni course nzuri tu na ajira zake zipo katika taasisi za serikali na hata katiak sekta binafsi. Pia si course ngumu kwa kuisoma. Huko katika makampuni ya simu au TV kunatakiwa uwe na cousre nyingine kama vile mass communication , marketing nk. Nakushauri ukomae na course hiyo, pengine ukatoka. Kwa mawasiliano piga 0655 775518
 
Back
Top Bottom