COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani? Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani? Kwanini waseme uongo huu waachwe?

Wamarekani wapambane na matatizo yao ya corona .mauaji ya weusi na China
 
Kwani nao wanalock down
Poleni Sana kwa Msiba Uliosababishwa na "UGONJWA FULANI UNAOKUMBA MADEREVA WA NCHI JIRANI"

Juzi tu ameitwa balozi wao kwa kuzusha mambo na leo wamezusha tena wakati covid TZ nzima wagonjwa ni wanne tu waliofariki ni 21.
 
Tutaendelea kupambana na maisha sisi sio wakufa kama wazungu
 
USA apambane na hali yake, ya kwetu atuachie wenyewe.
Me namwamini waziri wa Afya kuliko huyo balozi wao.
 
Jpm ameikimbiza corona hadi imeisha ,nyie mnalialia humu
Du nilisahau cheo kimoja
(1) mganga mkuu Wa serikali - anafanya kazi nzuri tu ya kutoa takwimu za walioparamia mahospitali kumbe wazima
Kuna haja sasa ya kuanzisha cheo cha
(1) mtendaji mkuu Wa mochwari serikalini - itakuwa kazi yake ni kutaja idadi ya wateja waliopo mochwari na chanzo cha vifo vyao na hiki cheo kitakufaa wewe miss USSR nakuona unafaa sana kwa utaalamu wako Wa kuvalisha wig. Kina Dada sasa kila mtu anaekufa akiletwa mochwari utamvalisha wig kwa gharama ya serikali ili watu wasiogope kifo na wewe ili usiache taaluma yako ya saloon attendant
 
Umeambiwa mara ya kwanza unatoka nje ya mada na kweli unaendelea kutoka jamaa hajakueleza watu waache kufanya kazi ila wewe unaongelea km watu wamezungumzia wasifanye kazi sababu ya Corona. Usi C&P wanayosema kina Kabudi kwa ajili ya propaganda fuatilia nn kinachojadiliwa hapa Kwenye huu uzi.
 
Baada ya kutokea maandamano kule okwao USA mbona vifo havijaongezeka...!!?

Labda ubalozi wao hapa tz wanazo taarifaa ambazo Ni tofauti na takwimu za serikali juu ya Corona.. ndio maana Pascal Mayalla Ana hoja...
Pascal Mayalla (Njaa) hana hoja anatafuta kuteuliwa ilu agange njaa yake. Kila nchi, Tanzania ikiwemo, hushauri wananchi wake wakiwa nje ya nchi zao wajisajili kwenye ubalozi wao ili waweze kusaidiwa ikibidi. Tanzania ilituma ndege ya Magufuli I India kuleta Wabongo walioliokuwa huko kwa shughuli zao mbalimbali. Kuna Wamarekani wengi hapa kwa shughuli mbalimbali anayejua wingi wao ni Ubalozi wa Marekani wenye jukumu la kuwalinda.
 
Wewe hapo mhafidhina ndugu zako wangapi wameugua na kufa. Tuwekee hapa vyeti vya vifo na majina yao. Maana huo ndio ushahidi pekekee zaidi ya hapo ni unafiki kama walivyo ubalozi wa Usa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…