COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani? Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani? Kwanini waseme uongo huu waachwe?

COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani? Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani? Kwanini waseme uongo huu waachwe?

Wamarekani wapambane na matatizo yao ya corona .mauaji ya weusi na China
Mambo kama haya ni kawaida sana katika vita ya kiuchumi, Marekani yupo kimasilahi kupitia siasa zake.
Ujasusi unaeleza watu wabaya hujivika ngozi za kondoo, wema upendo na kusaidia hasa misaada kwa jamii au Taifa japo nyuma ya pazia ni watu hatari sana ( USA).

Ukweli ambao wengi hawaufahamu ni kuwa wamarekani wengi wana maisha magumu sana hasa kwenye public services kama vile hospitali na Mashule huduma zao ni mbovu tena mbovu sana tofauti na private services.(wapo vizuri wamiliki ni hao mabepari wanao tupa misaada).
zaidi wanatumia vyombo vya habari kam BBC. N.k kusambaza propaganda kwa mataifa kama yetu kwao hakuna uhuru wa vyombo vya habari kuripoti matatizo ya kwao (hili lipo wazi).

Kwa akili za kawaida sio kwamba USA wanatupa msaada bali wanataka kunufaika kupitia misaada na mikopo wanayotoa.
Hiki USA wanacho kifanya, mkuu Pascal Mayalla ni ajenda za kisiasa( wanatuchafua kisiasa) hapa sio corona kuna mambo yao
No mercy under capitalism.
 
Kwani nao wanalock down
Poleni Sana kwa Msiba Uliosababishwa na "UGONJWA FULANI UNAOKUMBA MADEREVA WA NCHI JIRANI"

Juzi tu ameitwa balozi wao kwa kuzusha mambo na leo wamezusha tena wakati covid TZ nzima wagonjwa ni wanne tu waliofariki ni 21.
 
Tutaendelea kupambana na maisha sisi sio wakufa kama wazungu
Takwimu za kidunia zinasema kuwa wastani wa 5% ya watu waliombukizwa Corona ndio hufariki. (Yaani katika kila kifo kimoja cha mgonjwa wa Corona basi nyuma yake kuna watu 19 waliopata Corona na hawajafa, yaani wako fit mtaani).

Kwa hapa Tz, karibu kila siku kuna at least mtu mmoja mwenye umaarufu wa kati ambaye amefariki (kwa ugonjwa unaelezwa na ndugu zake wa karibu kuwa ni COVID).

Sasa hapo ndipo utajua tupo wapi na tunakwenda wapi.
 
USA apambane na hali yake, ya kwetu atuachie wenyewe.
Me namwamini waziri wa Afya kuliko huyo balozi wao.
 
Jpm ameikimbiza corona hadi imeisha ,nyie mnalialia humu
Du nilisahau cheo kimoja
(1) mganga mkuu Wa serikali - anafanya kazi nzuri tu ya kutoa takwimu za walioparamia mahospitali kumbe wazima
Kuna haja sasa ya kuanzisha cheo cha
(1) mtendaji mkuu Wa mochwari serikalini - itakuwa kazi yake ni kutaja idadi ya wateja waliopo mochwari na chanzo cha vifo vyao na hiki cheo kitakufaa wewe miss USSR nakuona unafaa sana kwa utaalamu wako Wa kuvalisha wig. Kina Dada sasa kila mtu anaekufa akiletwa mochwari utamvalisha wig kwa gharama ya serikali ili watu wasiogope kifo na wewe ili usiache taaluma yako ya saloon attendant
 
Wewe unawamini wamarekani kwa taariafa wanazo zitoa?
Lini umefanya tafiti kubaini ukweli wa kinachosemwa na ubalozi wa marekani
Usitake kubisha vitu ambavyo havina ukweli mkuu. Corona isiwe sababu ya watu washindwe kuendelea na maisha mengin
Siasa inagusa vitu vingi, kama utakuwa unajitambua basi utakuwa umeelewa
Umeambiwa mara ya kwanza unatoka nje ya mada na kweli unaendelea kutoka jamaa hajakueleza watu waache kufanya kazi ila wewe unaongelea km watu wamezungumzia wasifanye kazi sababu ya Corona. Usi C&P wanayosema kina Kabudi kwa ajili ya propaganda fuatilia nn kinachojadiliwa hapa Kwenye huu uzi.
 
Baada ya kutokea maandamano kule okwao USA mbona vifo havijaongezeka...!!?

Labda ubalozi wao hapa tz wanazo taarifaa ambazo Ni tofauti na takwimu za serikali juu ya Corona.. ndio maana Pascal Mayalla Ana hoja...
Pascal Mayalla (Njaa) hana hoja anatafuta kuteuliwa ilu agange njaa yake. Kila nchi, Tanzania ikiwemo, hushauri wananchi wake wakiwa nje ya nchi zao wajisajili kwenye ubalozi wao ili waweze kusaidiwa ikibidi. Tanzania ilituma ndege ya Magufuli I India kuleta Wabongo walioliokuwa huko kwa shughuli zao mbalimbali. Kuna Wamarekani wengi hapa kwa shughuli mbalimbali anayejua wingi wao ni Ubalozi wa Marekani wenye jukumu la kuwalinda.
 
Kila mtu anajua Corona ipo sana Tz, watu wanaugua kimya kimya na kuzikana kimya kimya pia. Serikali ilichokifanya ni kusitisha kutoa taarifa rasmi (ili kuhalalisha harakati za kimaisha ziendelee) lakini wakati huo huo taarifa za reja reja zikiendelea kuzagaa mitaani.

Hivyo ubalozi wa USA yuko sahihi kwa 100%, na hakuna ajabu yoyote kwa USA kutoa taarifa zenye lengo la kulinda raia wake waliopo hapa Tanzania. Ndio kazi iliyemleta Tanzania, na analipwa kwa kodi za wamerekani. Hatuwezi kumpangia cha kusema wala kufanya juu ya raia wa nchi yake.

Na sisi balozi wetu wa Tz aliyepo kule USA anapaswa kutoa taarifa za kulinda raia wa Tz waliopo huko USA au wanaotaka kwenda USA (ikiwezekana wasiende kabisa!) maana huko Corona ipo na kuna ghasia za maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi. Bahati mbaya balozi wetu huko USA yuko usingizini tu. Hajui anachotakiwa kufanya, sijui anasubiri kuambiwa na kina Bashiru au Pole Pole kitu cha kufanya
Wewe hapo mhafidhina ndugu zako wangapi wameugua na kufa. Tuwekee hapa vyeti vya vifo na majina yao. Maana huo ndio ushahidi pekekee zaidi ya hapo ni unafiki kama walivyo ubalozi wa Usa.
 
Back
Top Bottom