COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

Hali iliopo sasa ni sawa na mgonjwa wa Ukimwi anaejua kuwa anapaswa kubugia ARV ili aendelee kudumu ila kwa makusudi anaamua kujifanya ana wazimu na kuendelea na maisha yake bila kugusa dawa akitegemea maombi yatamlinda!
 
apo ndo mtihan.na kwa maana hiyo data za hawamu hii hazija kamilikaaaa full stop tuzubir data sahihi.
Kweli, maana hizi wanatuliza upepo uliovuma zaidi ila ni vizuri hapo baadaye watuchanganulie ili tujue huku mikoani hali ikoje ili tuwe na tahadhari zaidi, maana ugonjwa huu bila ukweli hali itakuwa mbaya sana.
 
Kweli, maana hizi wanatuliza upepo uliovuma zaidi ila ni vizuri hapo baadaye watuchanganulie ili tujue huku mikoani hali ikoje ili tuwe na tahadhari zaidi, maana ugonjwa huu bila ukweli hali itakuwa mbaya sana.
ummy sijui wame mpban alikuwa anatwambia vizur pamoja na mikoa yake ili na maeneo mengine wazid kutilia mkazo tusije ukakuta mkoa ambao hukutegemea una 50 sasa assume huo mkoa x hawajijui ni HATARI SANA
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa rai kwa Watanzania, kuacha kutoa taarifa za uzushi za vifo kuwa kila kifo kinachotokea kinasababishwa na Virusi vya Corona.

Hayo ameyabainisha leo Aprili, 29, 2020, wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa maambukizi ya Virusi vya Corona hapa nchini, ambapo amesema visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona vimeongezeka na kufikia 480, baada ya hii leo kutangazwa visa vipya 196, kati ya hivyo Bara ni 174 na Zanzibar ni 22.

Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa idadi ya wagonjwa waliopona nayo imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 167, Zanzibar wakiwa 36 na Bara ni 83, huku idadi ya vifo navyo ikiongezeka na kufikia 16.
 
Serikali ndo inasababisha habari potofu zisambae.serikali ipaswa kutoa taarifa sahihi Na kwa wakati 24/7
 
Tukipata vipimo vile vya Senegal vya TZS 2300 kila anayejisikia atakuwa anajipima mara moja kwa wiki ili kama amepata maambukizi aanze kupambana nao mapema kabla mwili haujaanza kuonyesha dalili ambazo hupelekea kifo
Unaweza nipa link ya hicho kifaa au ni cha kienyeji??
 
Duuuuh! Tunaongoza EA kwa sasa! Wacha tu nchi majirani watutenge maana tunasambaza hili gonjwa makusudi sasa! Kama hatuchukui hatua proven na WHO na wataalamu wabobezi maana yake tunafanya makusudi mazima kulisambaza!

Hiki kiburi sijui kinatoka wapi! Ewe Mola wetu tuepushe na balaa hili.
Usikate tamaa mkuu,kama kweli dhamila ya kuokoa jamii ipo,hilo linawezekana. Endapo tu serikali itatambua umhimu wa wananchi wake, hatua ya kwanza ya kukabiliana na maambukizi,ilishindikana.

Hivyo basi,kwa sasa,pazeni sauti ya kujisalimisha mwenye dalili,maana kuwasaka itakuwa ngumu. Pia,sijui huko karantini kukoje,hapa tu kikubwa serikali ikubali kushughulikia kila hitaji la mgonjwa au yeyote aliyepo karantini. vipimo viongezeke.

Maana kwa idadi hiyo,asikudanganye mtu wagonjwa wasiojulikani watakuwa zaidi ya mara mbili hiyo idadi
 
Una uhakika na hizo taarifa. Na wewe je umeshuhudia hayo makumi ya wanaokufa.?
Swali naomba unijibu.

Once a legend said "If you are good at something, never do it for free"
Hawezi kujibu swali Hilo...naye amesikia tu...very disturbing....binafsi nachukia uzushi na kutisha watu...ukisema watu wanakufa makumi kwa makumi wakati huna uhakika ni mbaya Sana na huko kutisha watu....ni kweli watu wanakufa lakini makumi kwa makumi hiyo hapana,..
 
Hebu na wewe tuambie ni nini kimewafanya wakae kimya siku zote hizo???

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila serikali na utendaji wake, hawawezi kufanya kama anavyofanya fulani, hata wewe nyumbani kwako una taratibu zako na maamuzi yako mkuu.

Mkuu kama wewe unawaamini hao BBC kuwa ndio wana data sahihi za wagonjwa kana kwamba wao ndio wanapima watu au ndio wamiliki wa hospital zetu basi sawa hiyo ni Imani yako mkuu na hukatazwi endelea tu kuwaamini mkuu.
 
Kama ni corona hii iliyopo duniani, hata wa kwenu watakufa na hasa wewe tena maiti yako itachukuwa muda kuonekana. Kwa kuwa unaishi kama digidigi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi dadangu, mbona unarukia treni kwa mbele?! Post haikuhusu wewe, sasa how come unatoa povu?! Niliyem-tag haja-mind, unakuja ku-mind wewe?! Au ni mumeo?! Au meachika au umeletewa nyumba ndogo na kwahiyo stress zako za kuachwa unazileta JF?!

Kama baada ya kuachwa umeamua kutafuta bwana, tafuta staili nyingine na sio kurukia rukia wanaume hovyo kima wewe!
 
Hahaha nadhani Mimi unayeniita mpuuzi naelewa zaidi kuliko wewe...sitaweza kufafanua zaidi ila ufahamu hivyo....
Kwani unadhani tatizo lenu ni kutoelewa?! Mnaelewa sana ila tu mnajitoa ufahamu wengine kwa kutetea matumbo yenu, wengine kwa sababu za kisisasa tu, na wanaokera zaidi ni wale walioapa kutetea kila kitu kwa sababu tu Rais ni Msukuma mwenzao kama ambavyo Gwajima alivyopata kuhamasisha watu kufanya hivyo simply because Magu ni Msukuma mwenzao!
 
Ningekua mimi ndie nina maamuzi ya kuliende hili,nisingetangaza kifo wala maambukizi,jitihada zingekuwa katika kuwaelimisha watu kuhusu huu ugonjwa.Hakuna tija katika kutangaa vifo wala idadi ya wagonjwa.Kuna malaria yanaua,kuna magonjwa mengine yanaua kila kukicha,kwanini tulazimike kuagaza corona_
Jambo lolote lile takwimu ni sahihi, na ukumbuke hizi takwimu zinatumiwa mpaka na WHO, EU ama AU katika kufanya maamuzi ya kutoa msaada pale utakapoitajika kwa nchi inayokuwa imeelemewa. Usifikiri inatangazwa tu kama fashion na pia ikigundulika kuna udanganyifu uwezekano wa kupigwa vikwazo na mataifa wafadhili ni mkubwa.
 
Chige,
Unawachukia wasukuma?! Na wengine wakichukia kabila lako wewe na watu wake itakuwaje?! Epuka migogoro ya dini na ukabila...ni hatari Sana...Kuna nchi na jamii zimesambaratika kwa mambo hayo...

Tanzania tuna bahati hatuna migogoro ya dini na ukabila inayojitokeza wazi...hata wakati wa Mwalimu Nyerere wako wachache waliokuwa wakisema upenyoni watu wa mkoa wa Mara wanapendelews...but coming to the point ya Corona hakuna anayebisha kuhusu hatari ya Corona...ila baadhi yet hatpendi exaggerations na lawama zisizo na maana..

Watu wamekaa mkao wa kulaumu tu mamlaka Kila kukicha...yaani watu wamekaa kuangalia makosa tu..halafu hata uzalendo haupo kabisa..eti watu wanaisifu Kenya sijui Mara Rwand na kadhalika...na Wala hawajui kinachoendelea huko Rwanda, Kenya na kwingineko kuhusu maoni ya raia wa huko..

Relatively Tanzania we are doing better katika vita hivi ila Tatizo ni mzaha wetu sisi wanachi...katika mitaa mingi ya Dar watu wanafanya mzaha kwa kutozingatia maslekezo..ingewekwa lockdown hapa Nina hakika malalamiko yangekuwa ya kutisha...
 
Back
Top Bottom