kwa ushauri wangu na experience ya ebola maana nilikua kwenye nchi ilioathirika na ebola
Bar na kumbi zote za starehe zifungwe.
viongozi mpaka wa ngazi za chini wapewe elimu ya kutosha ili waweze kuhamasisha watu kujua basics za kujikinga.
Kama vile wanavyotengeneza vipeperushi vya kampeni za uchaguzi wafanye hivyo hata kwenye kampeni ya corona.
vyombo vyote vya habari vizungumzie kuhusu corona na jinsi inavyoua na kuambukizwa , na wato idadi ya vifo nchi nyingine.
kila baada ya dakika 15-30 corona iongelewe ,watu wataogopa na kuanza kuchukua hatua ,lakini mpaka sasa sijaona ile serious kampeni kama ya kutafuta kura.
wahusika kama watasoma hapa wabuni mbinu mpya za kupambana na hii kimeta ya binadamu