COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

Kinachoshangaza watu bado wanarundikana kwenye ma Bar kama vile huu ugonjwa hauwahusu,na kinachotisha ni kuwa kila alietajwa kwenye hiyo idadi ana watu wake aliowaambukiza,Mbombo ngafu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi bia tutakua tunapata wapi
 
Tunatakiwa tufanye maamuzi magumu maana tutaanza kudondoka kama panzi,nimemsikia mwandishi mmoja huko USA anasema walati USA wakifanya hesabu za kuongezeka kwa kujumlisha,ugonjwa ulikuwa ukisambaa kwa kuzidisha!

Yaani wao walikuwa wanafanya 100 +100 =200 kama kanuni ya ugonjwa lakini kiuhalisia wenyewe ugonjwa ulikuwa unafanya
100×100 =10,000!

Tuache masihara,tuchukue hatua kali hata kama zitakuwa mateso kwetu!
 
Ninashauri mikoa ya mwanza,dar, Kilimanjaro na tanga owe lockdown haraka iwezekanavyo,vinginevyo tunaelekea kubaya na mikoa itakayokuwa lockdown serikali iwapatie huduma ya maji naumeme bure kwa kipindi Cha miezi mitatu.

malori ya mizigo ndiyo yataruhusiwa kuingia na kutoka ndani ya mikoa hiyo kwa ajili ya kupeleka vyakula,pili magari ya private yataruhusiwa kutoka na kuingia kwa kibali maalumu na idadi ya watakaokuwa kwenye magari ya private isixidi watu wanne
 
Tatizo nyie watawala mnaona nyie ndiyo wenye akili sana na peke yenu ndiyo mnaweza kufanya good decision. Mpaka mnawaita wakosoaji wenu kua ni COVID-19.

Tumeshauri ila ndiyo hivyo..tangu tulipo sikia ugonjwa umeingia Afrika ulikua ni muda sahii wa kufunga mipaka na huduma ya usafiri wa anga wa kimataifa.

Mwisho: Rais Magufuli sasa jifunze kua sio kila anaeshangilia uamuzi wako yupo sahii nasi kila anaepinga au kushauri ata kama yupo upande mwingine sio adui.
 
Nilisema Mungu hadhihakiwi lolote apandalo mtu ndio avunalo. Sisi kama taifa nilisema nivyema tukamuogopa Mungu na tukajua Mungu amechoka na kile wanadam wanakifanya. watumishi wa Mungu wamekusanya sadaka nakuwasahau masikin, wajane na yatima.

Unaweza ona kama picha ila baada ya pasaka maambukizi yameongezeka haya ni majibu tosha Mungu anatutaka tutubu na zile sifa mnasifia watu kwa masilah yenu binafsi basi haya ndio majibu.

Tutubu Mungu anayaona yote haya tunayatenda na amechukizwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…