LGE2024 CPA Makalla: Uimara wa Chama cha Siasa ni Nguzo Imara kwa Wananchi, Umoja Unajenga Imani

LGE2024 CPA Makalla: Uimara wa Chama cha Siasa ni Nguzo Imara kwa Wananchi, Umoja Unajenga Imani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa CCM-NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA makalla amesema uimara wa chama cha Siasa ni nguzo imara kwa wananchi kwani umoja unajenga imani kubwa kwao katika kuleta maendeleo.

Makalla ameeleza hayo leo Novemba 21, 2024 akizungumza katika kampeni na wananchi wa Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

Makalla amesema migongano na mafarakano katika vyama vya siasa kunavunja imani ya wananchi juu ya chama husika.

Aidha, amesema mabali na uzinduzi wa kampeni wamepokea mamia na maelfu ya wapinzani kurejea ndani ya CCM na kuwafanya wapinzani kuanza kukata tamaa na kukatisha safari yao kuelekea uchaguzi.

Amesema mikutano mikubwa iliyofanyika kuanzia jana imewepa imani kubwa kuwa CCM ina dhamana na watanzania na uzinduzi huo umetoa dira na muelekea wa CCM kwa wagombea juu ya ushindi wa chama hicho katika uchaguzi.

“Jana tumeanza kazi na safari ya kujakikisha CCM inashinda mitaa, vijiji na vitongoji tunafanya hivyo kwa sababu hili ni chama cha siasa na malengo yake ni kushika dola,” amesema Makalla.

Aidha, amesema kuwa hakushangazwa alipoambiwa Chama cha Demokrasia Na Maendeleo(CHADEMA) wamezindua kampeni katika wilaya hiyo wakiwa na watu 19 kwasababu anajua Kigamboni ni ngome ya CCM.

Amesema hali hiyo inaonesha kutokujiandia kwa baadhi ya vyama huku akifafanua maandalizi yalitakiwa kuanza na demokrasia ya kutafuta wagombea ndani ya chama.

Pia amewataka wagombea wa wilaya hiyo wasibwete kama ilivyoelezwa kuwa katika wilaya hiyo kuna mitaa 67 na CCM wameweka wagombea kote lakini CHADEMA hawakuwez akuweka wagombea katika mitaa tisa na kuwataka wakaze buti kwani kutakuwa na kura za ndiyo na hapana.


WhatsApp Image 2024-11-21 at 17.56.05.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-21 at 17.56.08.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-21 at 17.56.06.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-21 at 17.56.07.jpeg
 
Back
Top Bottom