CPA ni hitaji la kisheria la uhasibu na wala sio maarifa/ skills alizonazo mtu. Kuipata kwake ni kweli ni kwa kubahatisha. Kwa kuwa NBAA wanatoa maswali ya mitumba kutoka ACCA CMA etc, kufaulu kwake ni kwa kubahatisha pia kama umewahi kuliona swali la aina hiyo mahali na una uwezo wa kugandamizia (kukariri swali na majibu) vinginevyo nishida kufaulu mtihani wake. Waalimu wanaokutungia mtihani sio wanaokufundisha (kama inavyotakiwa katika elimu), hivyo hawajui kitu gani kimefundishwa, wao .pia wanabahatisha tu.Mwalimu akibahatisha 1/2 mwanafunzi atabahatisha 1/4
Master is an international academic qualification. Inatambulika duniani kote. CPA (T) inatambulika Tanzania tu. Hutapanda cheo kuwa Accountant officer ii mpaka uwe na CPA. Bachelor Degree ya uhasibu inakupa cheo cha Accountnt ii-i, basi zaidi ya hapo uwe na CPA. Kinachoipa nguvu CPA ni sheria sio ujuzi na maarifa anayokuwa nayo mwenye CPA. Matangazo ya kazi yanaweka CPA kama mojawapo ya sifa muhimu ili uajiriwe katika nafasi nyingi za uhasibu.
Hitimisho langu ni kuwa ukitaka kutambulika kama mhasibu na uweze kupandishwa cheo (Tanzania) katika fani ya uhasibu sharti uwe na CPA hata kama huna kitu kichwani. CPA haitoi wahasibu wazuri,inatoa good claimers. Ukitaka maarifa na ujuzi wa kazi Master,s inafaa, lakini hutapanda cheo chochote katika fani ya uhasibu. Uamuzi ni wako, kusuka au kunyoa