CPA(T) v/s MASTERS

CPA(T) v/s MASTERS

anza na mastaz coz ni rahisi kuipata kuliko cpa pia mastaz kimtaa inasifika hata ukifa kaburini wakiwa wanasoma historia fupi ya marehemu utauza mbaya japokuwa utakuwa tayari kuliko CPA ambayo mtaani hata hawaijui wanaweza fikilia ni jina lingine la unesi au mtu wa monchwari.

Haha haha, hii yako kali aisee
 
Wazee CPA ni kama leseni ya uhasibu sio academic, ndio maana inaitwa certified public accountant (Tanzania) pia kuna ya Kenya CPA(K). Hata ukiwa na master ya uhasibu kama hauna CPA hutambuliki kitaaluma kwa kuwa sio registered, utaratibu ni wa kidunia na upo kwenye professionals zote, Udaktari, kwa mfano ukigraduate muhimbili medicine 5years. Usipoenda interniship ya 1year km daktari mwanafunzi huwi daktari pia Engineers wakimaliza degree ya 4yrs kama asipofanya mitihani ya Bodi ya maengineers ERB bado hatàmbuliki kwahiyo master ina nafasi yake na CPA ina nafasi yake hazina uhusiano, ni kama ilivyo kwa Lawyers ukimaliza degree ya sheria 3yrs usipoenda 1yr. School of Law bado hutambuliki na wanachama certified.
 
CPA ni hitaji la kisheria la uhasibu na wala sio maarifa/ skills alizonazo mtu. Kuipata kwake ni kweli ni kwa kubahatisha. Kwa kuwa NBAA wanatoa maswali ya mitumba kutoka ACCA CMA etc, kufaulu kwake ni kwa kubahatisha pia kama umewahi kuliona swali la aina hiyo mahali na una uwezo wa kugandamizia (kukariri swali na majibu) vinginevyo nishida kufaulu mtihani wake. Waalimu wanaokutungia mtihani sio wanaokufundisha (kama inavyotakiwa katika elimu), hivyo hawajui kitu gani kimefundishwa, wao .pia wanabahatisha tu.Mwalimu akibahatisha 1/2 mwanafunzi atabahatisha 1/4
Master is an international academic qualification. Inatambulika duniani kote. CPA (T) inatambulika Tanzania tu. Hutapanda cheo kuwa Accountant officer ii mpaka uwe na CPA. Bachelor Degree ya uhasibu inakupa cheo cha Accountnt ii-i, basi zaidi ya hapo uwe na CPA. Kinachoipa nguvu CPA ni sheria sio ujuzi na maarifa anayokuwa nayo mwenye CPA. Matangazo ya kazi yanaweka CPA kama mojawapo ya sifa muhimu ili uajiriwe katika nafasi nyingi za uhasibu.
Hitimisho langu ni kuwa ukitaka kutambulika kama mhasibu na uweze kupandishwa cheo (Tanzania) katika fani ya uhasibu sharti uwe na CPA hata kama huna kitu kichwani. CPA haitoi wahasibu wazuri,inatoa good claimers. Ukitaka maarifa na ujuzi wa kazi Master,s inafaa, lakini hutapanda cheo chochote katika fani ya uhasibu. Uamuzi ni wako, kusuka au kunyoa

kama ukikariri unafaulu basi ukielewa utafaulu zaidi...
 
kwenye fani ya uhasibu CPA siyo kitu cha kuuliza, muhimu uwe nayo. ukiweza ukaamua kufanya ACCA, mimi ndo napigika nayo kumalizia. kila la kheri!!
 
Academically-Masters
Professionally-CPA
 
Naomba kujuzwa mambo mawili;

1.Vigezo vya Kujiunga na Chama cha Wahasibu(TAA)
2.Sheria inayomlazimisha Mtu kuwa na CPA(T) ndiyo aruhusiwe kuanzisha Auditing/Accounting Firm.
 
nashauri apige masters kwanza ndio afikirie CPA japo inategemea pia na position yako hapo ulipo inahitaji nini sana
 
Back
Top Bottom